Swahili
- Ukurasa Kuu    - Kumi Juu    - Mada Mpya    - Salimisha Habari    - Tafuta    - Kiswahili Jukwaa    - Kiswahili Wanachama    - Tathmini    - Ujumbe wa Kibinafsi    - Tafiti    - Majarida    - Hadithi Archive    - Maudhui    - Viungo vya Wavuti    - Vipakuliwa    - Maswali ya Kawaida    - Tunapendekeze    - Orodha ya Kuingia   

EsinIslam Media Swahili: Waislamu Wanawake - maisha yao na Famili

Tafuta mada hii:   
[ Nenda nyumbani | Chagua Mada Mpya ]

Waislamu Wanawake - maisha yao na Famili

Elimu Ni Wajibu Kwa Mwanamke Wa Kiislamu - MIFANO YA WANAWAKE WATUKUFU
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

 Mfumo Na Muelekeo Wa Nyaraka Hizi Umechukuliwa Kutoka Kwa Kijitabu Kinachoitwa 

“Al-Mar’at Al-Muslimah Fiy Twalabil ‘Ilm”  

Elimu Ni Wajibu Kwa Mwanamke Wa Kiislamu - MIFANO YA WANAWAKE WATUKUFU 

 (Mwanamke Muislamu Katika Kutafuta Elimu)

Kilichochapishwa Na Daarul Arqam,  Chapa Ya Pili, 

MIFANO YA WANAWAKE WATUKUFU UMMUL MU’MININA ‘AISHAH BINT ABUBAKR AS-SIDDIQ: 

Alizaliwa mwaka wa 4 Baada ya Utume (614 BI). Babake alikuwa ni ‘AbdAllaah bin ‘Uthman bin ‘Aamir at-Taymi au Abu Bakr as-Siddiq bin Abi Quhafah. Mamake alikuwa Umm Ruman bint ‘Aamir bin ‘Uwaymir al-Kananiyah. ‘Aishah (Radhiya Allaahu ‘anha) alikuwa ni msomi, mwenye akili, uoni wa hali ya juu na uwezo wa kutatua mambo nyeti na mazito ya Dini. Alikuwa msitari wa mbele katika upokeaji wa Hadithi za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), nambari sita miongoni mwa Masahaba wote (Radhiya Allaahu ‘anhum). Amepokea Hadithi 2,220, miongoni mwa hizo 174 zikiwa ni Muttafaqun ‘alayhi, 54 katika al-Bukhari, 67 katika Muslim, na 2,017 katika vitabu vyengine vya Hadithi. Alikuwa mjuzi sana katika elimu za Qur’ani, Hadithi, Fikihi, Mashairi, Historia na Nasaba. Anahesabiwa miongoni mwa Mujtahid na jina lake linatajwabila ya shaka pamoja na yale ya Abu bakr, ‘Umar, ‘Athman, ‘Ali, Ibn Mas‘ud, Ibn ‘Abbas na Ibn ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhum). Alikuwa akitoa fatwa wakati wa Abu Bakr, ‘Umar na ‘Athman.  ‘Aishah (Radhiya Allaahu ‘anha) alikuwa na fadhila kubwa kuliko wanawake wote. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Ubora wa ‘Aishah kulinganisha na wanawake wengine ni kama ubora wa tharid kwa aina nyengine ya vyakula”.

(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
Waislamu Wanawake - maisha yao na Famili

Elimu Ni Wajibu Kwa Mwanamke Wa Kiislamu - HAJA YETU YA MWANAMKE MUISLAMU M
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

Mfumo Na Muelekeo Wa Nyaraka Hizi Umechukuliwa Kutoka Kwa Kijitabu Kinachoitwa 

“Al-Mar’at Al-Muslimah Fiy Twalabil ‘Ilm”  

Elimu Ni Wajibu Kwa Mwanamke Wa Kiislamu - HAJA YETU YA MWANAMKE MUISLAMU MWENYE MUAMKO 

Mwanamke Muislamu Katika Kutafuta Elimu)

Kilichochapishwa Na Daarul Arqam,  Chapa Ya Pili, 

HAJA YETU YA MWANAMKE MUISLAMU MWENYE MUAMKO 

Bila ya shaka, Ummah wa Kiislamu unahitaji wanawake wasomi wenye kufanya kazi ambao watasimama katikakujenga watoto watakaoshiriki katika muelekeo uliobarikiwa na muamko na kuelewa majukumu yao. Hamu yao ni kuzitakasa nafsi zao na za waume wao, watoto wao na kila kitakachorudisha katika Ummah wa Kiislamu nguvu na utukufu. 

Jambo hili ni wajibu liwe katika akili yake anapolala na kuamka na wala asiwe ni mwenye kushughulishwa na mambo mengi ya Maisha ambayo yamewasahaulisha kuhusu ndugu zao Waislamu na dini yao. Ni vizuri sana muamko wao uzinduliwe katika kutekeleza na kuwasaidia Waislamu wenziwao na Uislamu kwa nia mzuri, ikhlasi na kutaka ridhaa ya Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala).

(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
Waislamu Wanawake - maisha yao na Famili

Elimu Ni Wajibu Kwa Mwanamke Wa Kiislamu - DURU YA WANAWAKE WA MWANZO KATIK
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

Mfumo Na Muelekeo Wa Nyaraka Hizi Umechukuliwa Kutoka Kwa Kijitabu Kinachoitwa 

“Al-Mar’at Al-Muslimah Fiy Twalabil ‘Ilm”  

Elimu Ni Wajibu Kwa Mwanamke Wa Kiislamu - DURU YA WANAWAKE WA MWANZO KATIKA KUSOMA NA KUENEZA ELIMU 

(Mwanamke Muislamu Katika Kutafuta Elimu)

Kilichochapishwa Na Daarul Arqam,  Chapa Ya Pili, 

DURU YA WANAWAKE WA MWANZO KATIKA KUSOMA NA KUENEZA ELIMU 

 Hakika duru ya mwanamke Muislamu katika historia ya Uislamu, historia ya Da‘wah na historia ya mataifa na watu imesajili upeo wa ubora, utukufu na utakaso katika nyaraka. Sote tunajua na kuelewa yale aliyoyafanya Mama wa Waumini Bibi ‘Aishah bint Abubakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) katika kuhifadhi Hadithi nyingi pamoja na kuzisomesha. Huyu bibi mtukufu alikuwa anaulizwa maswali mengi na wakubwa miongoni mwa Masahaba (Radhiya Allaahu ‘anhum) katika mambo mengi ya dini. Historia ya Kiislamu imesajili kwa herufi za nuru na dhahabu majina ya Sahabiyat watukufu (Radhiya Allaahu ‘anhum) mfano wa Asmaa bint Abubakr, Umm ‘Atiyyah al-Ansariyah, Umm Kabshah Qadha‘iyah, Asmaa bint ‘Umays, Umm Sulaym bint Milhan, Umm Dardaa na fatimah bint Qays (Radhiya Allaahu ‘anha), wote walikuwa wapokezi na waalimu wa Hadithi za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
Waislamu Wanawake - maisha yao na Famili

Elimu Ni Wajibu Kwa Mwanamke Wa Kiislamu - ELIMU ANAZOPASWA KUSOMA MWANAMKE
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

 Mfumo Na Muelekeo Wa Nyaraka Hizi Umechukuliwa Kutoka Kwa Kijitabu Kinachoitwa 

“Al-Mar’at Al-Muslimah Fiy Twalabil ‘Ilm”  Elimu Ni Wajibu Kwa Mwanamke Wa Kiislamu - ELIMU ANAZOPASWA KUSOMA MWANAMKE (Mwanamke Muislamu Katika Kutafuta Elimu)

Kilichochapishwa Na Daarul Arqam,  Chapa Ya Pili,

ELIMU ANAZOPASWA KUSOMA MWANAMKE1 KUSAHIHISHA UFAHAMU MBAYA: 

Huenda wakaona baadhi ya watu kuwa mwanamke wa Kiislamu hana uwezo wa kusoma na kusomesha. Na kuwa kuna vikwazo vya kisheria ya dini ya Kiislamu vinavyozuia harakati zake katika jambo hili. Muono huu ni wa makosa unaotokana na ufahamu mbaya wa Uislamu, kwani Uislamu ni nidhamu kamili ya Maisha. Yule anayeangalia kwa kina hali ya mwanamke na harakati zake katika chimbuko la Uislamu na duru yake katika historia kuanzia hasa wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Makhalifa Waongofu (Radhiya Allaahu ‘anhum) ataona hayo. Kinachotakikana leo kutoka kwa mwanamke Muislamu ni kujinyanyua kwa kila njia ili atekeleze majukumu yake ya kihistoria na kuutengeneza Ummah. 

2 MASHARUTI YA MUAMKO: 

 Uislamu umempatia mwanamke na mwanamume amana ya Dini ambayo ni amana muhimu katika Maisha, bali ndio nguzo na msingi. Uislamu ulimjaalia kila mmoja ni mchungaji hasa katika kusahihisha na kuweka sawa ‘Aqiydah yake, ibadah zake, maadili yake na amali zake. Yule ambaye hatasoma hukumu za ‘ibadah na mafungamano na mahusiano na Allaah na mfumo wa utamaduni … na yule asiyesoma Misingi ya ‘aqiydah na asiye dhamini falsafa ya kweli na muelekeo wa jamii na ubora wa maadili na malengo ya maisha na misingi ya adabu, asiyesoma au kufundishwa haya na yote ni katika milango ya elimu na yenye kuondosha mateso ya ujinga na giza la hisia na maaddah ameingia katika dhambi la kupunguza. Na hapo ameitia nafsi yake katika kazi ya kubaki myuma katika ulimwengu na Akhera.

(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
Waislamu Wanawake - maisha yao na Famili

Elimu Ni Wajibu Kwa Mwanamke Wa Kiislamu - MSIMAMO WA UISLAMU KATIKA KUSOMESHA W
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

 Mfumo Na Muelekeo Wa Nyaraka Hizi Umechukuliwa Kutoka Kwa Kijitabu Kinachoitwa 

“Al-Mar’at Al-Muslimah Fiy Twalabil ‘Ilm”  

Elimu Ni Wajibu Kwa Mwanamke Wa Kiislamu - MSIMAMO WA UISLAMU KATIKA KUSOMESHA WANAWAKE 

 (Mwanamke Muislamu Katika Kutafuta Elimu)

Kilichochapishwa Na Daarul Arqam,  Chapa Ya Pili, 

MSIMAMO WA UISLAMU KATIKA KUSOMESHA WANAWAKE 1 WAJIBU WA KUSOMESHWA WANAWAKE:

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Kutafuta elimu ni faradhi (lazima) kwa kila Muislamu”. Tunaona kuwa mwanamke yumo ndani katika ujumla wa Hadithi kwani Muislamu anakuwa mume au mke na wote ni sawa. Yeyote atakaye ingia katika hukumu za kisheria ataona kuwa kwa hakika wanawake ni ndugu za wanaume wala hawana hukumu hasa kwao wao ila baadhi ya hukumu zinazotofautisha baina ya maumbile ya wanaume na wanawake. Asili ni kuunganisha sheria na ujumla wa maneno wala haijathubutu utofauti ila kwa dalili. Mwanamke ni sawa na mwanamume katika majukumu ya ibadah za kinafsi (Dhikri, Swalah, Swaumu, Zakah, Hajj, n.k.) na katika maadili na mahusiano (ukweli, uadilifu, wema, taqwa na adabu) na Maisha kwa ujumla (subira, hijrah, kinyume cha ukafiri, twaa, kuwa pamoja na kikundi cha Waumini, urafiki na usaidizi).

(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
Waislamu Wanawake - maisha yao na Famili

Elimu Ni Wajibu Kwa Mwanamke Wa Kiislamu - ELIMU ANAZOPASWA KUSOMA MWANAMKE
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

 Mfumo Na Muelekeo Wa Nyaraka Hizi Umechukuliwa Kutoka Kwa Kijitabu Kinachoitwa 

“Al-Mar’at Al-Muslimah Fiy Twalabil ‘Ilm”  Elimu Ni Wajibu Kwa Mwanamke Wa Kiislamu - ELIMU ANAZOPASWA KUSOMA MWANAMKE (Mwanamke Muislamu Katika Kutafuta Elimu)

Kilichochapishwa Na Daarul Arqam,  Chapa Ya Pili, ELIMU ANAZOPASWA KUSOMA MWANAMKE 1 SEHEMU YA ELIMU: Elimu katika Uislamu ina sehemu na daraja ambayo haijapatiwa na dini nyengine yeyote. Hii tunaiona wazi katika aya tukufu inayosema, “Soma kwa jina la Mola wako Aliyeumba”. Kama alivyosema tena Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala),  “Sema: ‘Je, wanaweza kuwa sawa wale wanaojua na wale wasiojua?” Dini ambayo maagizo yake ya kwanza ni kusoma na elimu ni dini ambayo inataka wafuasi wake wawe msitari wa mbele katika kusambaza elimu. Huu kwa hakika ni mfumo wa Mola, Ambaye ameifanya elimu kuwa faradhi (lazima) kama ilivyokuja katika Hadithi. Imepokewa na Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema, “Kutafuta elimu ni faradhi kwa kila Muislamu”. Lafdhi ya Muslim (Muislamu) ina makusudio ya wanaume na wanawake kwani imewachang’anya wote bila kubagua.

(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
Waislamu Wanawake - maisha yao na Famili

Elimu Ni Wajibu Kwa Mwanamke Wa Kiislamu - UTANGULIZI
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

 Mfumo Na Muelekeo Wa Nyaraka Hizi Umechukuliwa Kutoka Kwa Kijitabu Kinachoitwa

Elimu Ni Wajibu Kwa Mwanamke Wa Kiislamu - UTANGULIZI

“Al-Mar’at Al-Muslimah Fiy Twalabil ‘Ilm”  (Mwanamke Muislamu Katika Kutafuta Elimu)

Kilichochapishwa Na Daarul Arqam, Chapa Ya Pili,

1.0 UTANGULIZI 

 Sifa zote njema anastahiki Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala), ambaye Ameumba wanadamu, Akawaongoza na Kuwafundisha kwa kutumia kalamu. Akawaongoza pia kwa yale wasio yajua. Swalah na salamu zimshukie yule Aliyetumwa kuwa rehema kwa walimwengu Nabii wetu Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na juu ya ahli zake na swahaba zake na waliomfuata miongoni mwa watu.

(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
Waislamu Wanawake - maisha yao na Famili

Fadhila Za Hijaab: Hijaab ni ‘Iffah (Stara), Hijaab ni Twahara (Utakaso), Hijaab
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

Imefasiriwa na Salwa Muhammad
Fadhila Za Hijaab: Hijaab ni ‘Iffah (Stara), Hijaab ni Twahara (Utakaso), Hijaab Ni Ngao, Hijaab ni Taqwah (Ucha Mungu), Hijaab Ni Iymaan, Hijaab ni Hayaa, Hijaab ni (Ghiyrah) Ghera

Hijaab ni tendo tiifu kwa Allaah na kwa Mtume Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala) kasema katika Qur-aan;

{{Haiwi kwa Muumini mwanamume wala Muumini mwanamke kuwa na khiari katika jambo, Allaah na Mtume Wake wanapokata shauri katika jambo lao. Na mwenye kumuasi Allaah na Mtume Wake basi hakika amepotea upotofu ulio wazi.}} Al-Ahzaab: 36

Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala) pia kasema;

{{Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasionyeshe uzuri wao isipokuwa unaodhihirika. Na waangushe shungi zao (juyuubihinna) juu ya vifua vyao}} An-Nuur: 31(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
Waislamu Wanawake - maisha yao na Famili

Makatazo Ya Kishari’ah Kwa Wanawake – 7
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

Imekusanywa Na: Abu Faatwimah

Makatazo Ya Kishari’ah Kwa Wanawake – 7

Katazo La Kujipiga piga Na Kuchana Nguo Wakati Wa Msiba
Msiba ni katika Sunnah na mitihani ya uhai, Allaah Anasema:

“Na bila shaka Tutakujaribuni kwa kitu katika khofu na njaa na upungufu wa mali na nafsi na mazao. Na wabashirie wenye kusubiri.” [Al-Baqarah 2: 155].

Pia Allaah Anasema:
“Kila nafsi itaonja mauti. Na hakika mtalipwa kikamilifu ujira wenu Siku ya Qiyaamah. Basi atakayewekwa mbali na Moto na akaingizwa Jannah kwa yakini amefuzu. Na maisha ya dunia si lolote ila ni starehe ya udanganyifu.” [Aal-‘Imraan 3: 185].(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
Waislamu Wanawake - maisha yao na Famili

Makatazo Ya Kishari’ah Kwa Wanawake – 6
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

Imekusanywa Na: Abu Faatwimah

Makatazo Ya Kishari’ah Kwa Wanawake – 6

Katazo la Kuingia katika Hammamaat [sehemu za kuogea zilizojengewa kama vile mahodhi mabwawa na kadhalika na kuruhusiwa kutumiwa na kila mtu].

Jamii nyingi huweka sehemu ambazo huwa zinaruhusiwa kutumiwa na kila mtu kwa malengo tofauti kama vile mabustani, maduni na kadhalika; pia hutenga sehemu nyingine ili zitumike kwa malengo maalumu; kama vile sehemu za kuogea au kuogolea, au sehemu za kuumika, au sehemu za kukandwa, au sehemu za kutengenezwa nyuso au nywele, au sehemu za kupambwa, au sehemu za kubadilisha mavazi au kujilinga, au sehemu za kupumzika, au sehemu za kufua nguo na kadhalika.

(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
Waislamu Wanawake - maisha yao na Famili

Simu Katika Shari'ah Ya Kiislamu - 2
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

Imekusanywa Na: Sulaymaan ‘Iysa

Simu Katika Shari'ah Ya Kiislamu - 2

(4) Dakika na muda wa maongezi

Kipimo chake ni maneno ya kiusuli yasemayo:
•Kila sehemu pana mazungumzo husika•Na kila mazungumzo yana kipimo husika•Katika kipindi cha nyuma kidogo na mpaka sasa baadhi ya mitandao ya simu imekuwa ikitoa ofa ya kuongea muda mrefu kwa gharama ndogo, na mtu bila kujali kuwa huu ni wakati wa kazi au usiku watu wamelala na kadhalika, anarefusha mazungumzo kisa na mkasa ni kwamba leo ana ofa ya kuongea bure masaa 24 au 12 kwa thamani ndogo ya vocha alizoingiza katika simu yake.

(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
Waislamu Wanawake - maisha yao na Famili

Simu Katika Shari'ah Ya Kiislamu - 1
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

Imekusanywa Na: Sulaymaan ‘Iysa

Simu Katika Shari'ah Ya Kiislamu - 1

BismiLlaahir Rahmaanir Rahiym

Simu katika lugha ya kiarabu inaitwa “HAATWIF” au “AL-JAWWAAL” au “TILFUUN” vyovyote iwavyo simu ni chombo kitumikacho kwa ajili ya kuwasiliana.

Uislamu upo pamoja na wakati (Yaani haujapitwa na wakati kama wanavyodhani wasioujua Uislamu au maadui wa Uislamu kadhalika. Wakati upo na Uislamu.) Tazama watu wakisema nani wa kwanza kufika mbinguni? (si kwenye sayari kama tunavyosikia na kuona katika vitabu). Basi jawabu si mwengine bali ni Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Vile vile wakisema ni nani wa kwanza kufanyiwa upasuwaji? Basi jibu si mwengine bali ni Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam); bali kafanyiwa upasuaji mara mbili.

(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
Waislamu Wanawake - maisha yao na Famili

Zichume Sifa Kumi Njema - Sifa Ya Kumi (Ya Mwisho) Wanaume Na Wanawake Wanaomdhu
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

Zichume Sifa Kumi Njema - Sifa Ya Kumi (Ya Mwisho) Wanaume Na Wanawake Wanaomdhukuru sana Allaah

Anasema Allaah سبحانه وتعالى:
إِنَّ الْمُسْلِمِينَ وَالْمُسْلِمَاتِ وَالْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ وَالْقَانِتِينَ وَالْقَانِتَاتِ وَالصَّادِقِينَ وَالصَّادِقَاتِ وَالصَّابِرِينَ وَالصَّابِرَاتِ وَالْخَاشِعِينَ وَالْخَاشِعَاتِ وَالْمُتَصَدِّقِينَ وَالْمُتَصَدِّقَاتِ وَالصَّائِمِينَ وَالصَّائِمَاتِ وَالْحَافِظِينَ فُرُوجَهُمْ وَالْحَافِظَاتِ وَالذَّاكِرِينَ اللَّهَ كَثِيرًا وَالذَّاكِرَاتِ أَعَدَّ اللَّهُ لَهُم مَّغْفِرَةً وَأَجْرًا عَظِيمًا ﴿35﴾
((Hakika
Waislamu wanaume na Waislamu wanawake, na Waumini wanaume na Waumini wanawake, na watiifu wanaume na watiifu wanawake, na wasemao kweli wanaume na wasemao kweli wanawake, na wanaosubiri wanaume na wanaosubiri wanawake, na wanyenyekevu wanaume na wanyenyekevu wanawake, na watoao sadaka wanaume na watoao sadaka wanawake, na wanaofunga wanaume na wanaofunga wanawake, na wanaojihifadhi tupu zao wanaume na wanawake na wanaomdhukuru Allah kwa wingi wanaume na wanawake, Allah Amewaandalia msamaha na ujira mkubwa)) [Al-Ahzaab:35]

(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
Waislamu Wanawake - maisha yao na Famili

Makatazo Ya Kishari'ah Kwa Wanawake - 5
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

Imekusanywa Na: Abu Faatwimah
Makatazo Ya Kishari'ah Kwa Wanawake - 5

Katazo La Kumsifia Mwanamke Wa Nje Kwa Mumewe
Tabia ya kupenda kuelezea, kusifia na kuhadithia kila kitu ni moja kati ya tabia na desturi walizonazo wanawake wengi; hivyo basi tabia hiyo wakati mwingine huwapelekea kujisahau na kuanza kuelezea au kutoa wasifu wa wanawake wenziwao si kwa mashoga zao tu, bali hata kwa waume zao pia, wakijisahau kuwa jambo kama hilo ni katika yeye kupelekea kushitua na kuamsha hisia fulani kwa waume zao na kusababisha mengi katika akili, mwili na mioyo yao.(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
Waislamu Wanawake - maisha yao na Famili

Makatazo Ya Kishari’ah Kwa Wanawake - 4
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

Imekusanywa Na: Abu Faatwimah

Makatazo Ya Kishari’ah Kwa Wanawake - 4

Katazo La Kutokuwa Na Shukurani [Kukanusha] Ihsaan

Huu dada yangu Muislamu ni uwanja mwingine wenye hatari kubwa, na kwa bahati mbaya ni kuwa wengi miongoni mwa wanawake kwa masikitiko makubwa wameuingia na kuamua kuwa ni katika sehemu zao za kuishi na kutafuta kuridhiwa au kupewa ruhusa ya kwenda watakapo hata kama ni kwenye maasi na pasipo mridhia Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
Waislamu Wanawake - maisha yao na Famili

Makatazo Ya Kishari’ah Kwa Wanawake - 3
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

Imekusanywa Na: Abu Faatwimah 

Makatazo Ya Kishari’ah Kwa Wanawake - 3

Katazo La Kujizuilia Kulala [Kustarehe] Na Mume Anapomuhitaji
Huu dada yangu katika iymaan ni uwanja wenye hatari kubwa, na wengi miongoni mwa wanawake kwa visingizio visivyokuwa na misingi wameuingia na kugaragara ndani yake; hivyo imewawajibikia kwa hilo laana ya Malaika wa ar-Rahmaan kwa kuwa waume zao hawakuridhika nao bali walighadhibika nao.

(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
Waislamu Wanawake - maisha yao na Famili

Makatazo Ya Kishari’ah Kwa Wanawake - 2
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

Imekusanywa Na: Abu Faatwimah
Makatazo Ya Kishari’ah Kwa Wanawake - 2

Makatazo yaliyothibiti maalumu kwa waumini wa kike ni kama yafuatayo:

Katazo La Kuunganisha Nywele

Tendo hili kwa huzuni kubwa limekuwa ni katika yenye kuonekana kuwa ni miongoni mwa mapambo, bali ni pambo lisiloepukika kwa kila mwenye kutaka kujiremba hasa kwa wenye kutaka kuolewa; wawe hawana nywele au wenye nywele ngumu/fupi au hata wenye nywele za singa; yote kutaka kuiga na kujifananisha na kudanganya, kwa kuwa tuko mbali na yaliyopokelewa kutoka kwa Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu kuunganisha nywele.

(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
Waislamu Wanawake - maisha yao na Famili

Makatazo Ya Kishari’ah Kwa Wanawake - 1
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

Imekusanywa Na: Abu Faatwimah
 
Makatazo Ya Kishari’ah Kwa Wanawake - 1

Kila sifa jema inamstahikia Allaah Aliyetukuka Muumba wa ulimwengu na walimwengu wake, Swalah na Salamu zimfikie kipenzi cha Waislamu Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Sahaba zake kiraam (Radhiya Allaahu 'anhum) na kila anaewafuata kwa ihsaan mpaka Siku ya Mwisho.
Shari’ah, amri, makatazo na kanuni ni katika taratibu ambazo jamii haiwezi kiziepuka ikitaka kuwa na uadilifu, amani, usalama na uhuru kwa wana jamii wake.(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
EsinIslam The Muslim World Portal For Islamics, News, Fatwas, Audios, Videos, Muslim News, Quranic Islamic Articles, Radio, Audio Quran, TV Channels, Fatwa Rulings, Muslim News Newspapers Magazines Headlines Articles Forums Schools, Universities, Colleges, Mosques, Qur'an, Hadith, Sunnah, Fiqh, Prayers, Salat, Fasting Ramadan, Vidoes, Books On EsinIslam.Com And Muxlima.Com

  :-: Go Home :-: Go Top :-: