Swahili
- Ukurasa Kuu    - Kumi Juu    - Mada Mpya    - Salimisha Habari    - Tafuta    - Kiswahili Jukwaa    - Kiswahili Wanachama    - Tathmini    - Ujumbe wa Kibinafsi    - Tafiti    - Majarida    - Hadithi Archive    - Maudhui    - Viungo vya Wavuti    - Vipakuliwa    - Maswali ya Kawaida    - Tunapendekeze    - Orodha ya Kuingia   

 

 
EsinIslam Media Swahili: Mkuu - teknolojia na taaluma

Tafuta mada hii:   
[ Nenda nyumbani | Chagua Mada Mpya ]

Mkuu - teknolojia na taaluma

Msamaha Na Ujira Mkubwa Tutakaopata Baada Ya Kuzichuma Sifa Kumi Njem
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

 
 
 Msamaha Na Ujira Mkubwa Tutakaopata Baada Ya Kuzichuma Sifa Kumi Njema Baada kukumbushana maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) katika Aayah tukufu iliyotaja sifa kumi njema, tumeona kwamba mwisho kabisa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema: ((أَعَدَّ اللَّهُ لَهُم مَّغْفِرَةً وَأَجْرًا عَظِيمًا)) ((Allah Amewaandalia msamaha na ujira mkubwa)) [Al-Hazab:35] Vile vile Anasema katika Aayah nyingine: ((وَعَدَ اللّهُ الَّذِينَ آمَنُواْ وَعَمِلُواْ الصَّالِحَاتِ لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَأَجْرٌ عَظِيمٌ)) ((Allah Amewaahidi waliomuamini na wakatenda mema kwamba watapata maghfira na malipo makubwa)) [Al-Maaidah]
Maana kwamba; Tutasamehewa Madhambi yetu ambayo hakuna aliyeepukana nayo, lakini Mola wetu ni Mkarimu Mwingi Wa Kurehemu na Mwingi wa Msamaha Hukubali toba zetu wakati wowote kama Anavyotuahidi katika Qur-aan na pia katika Hadiyth za Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):


(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
 


Mkuu - teknolojia na taaluma

Muenzi Mke Wako
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

 
 
Shaykh 'Abdullaah 'Adhamiy Imefasiriwa na Iliyaasa

Muenzi Mke Wako

Kwa kuoa huchukui tu mke, Bali unachukua ulimwengu wako mzima. Kuanzia hapo mpaka maisha yako yote mke wako atakuwa mwenzio, mwandani wako, na rafiki yako mpenzi. Atashiriki katika nyakati zako nzuri, siku zako, na miaka yako. Atakuwa pamoja nawe katika furaha na shida, katika mafanikio na tabu, katika ndoto zako na katika wakati wa hofu. Ukiumwa, atakupa huduma bora kabisa. Wakati unapohitaji msaada atafanya vyovyote awezavyo kwa ajili yako. Wakati una siri, ataitunza siri yako, wakati unahitaji ushauri, atakupa ushauri mzuri kabisa.  Atakuwa na wewe utakapoamka asubuhi kitu cha kwanza ambacho macho yako yataona ni macho yake. 

Wakati wa mchana, atakuwa na wewe, kama kuna wakati mchache hatokuwa na wewe kwa kimwili, atakuwa anakufikiria wewe, anakuombea dua kwa moyo wake wote, akili yake yote, na roho yake nyote. Ukienda kulala usiku, kitu cha mwisho macho yako kuona itakuwa ni yeye, na ukilala bado utakuwa unamuona katika ndoto zako. Kwa kifupi atakuwa ni ulimwengu wako mzima na wewe utakuwa ulimwengu wake mzima.


(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
 


Mkuu - teknolojia na taaluma

Ujumbe Kwa Mwanamke
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

 
 
رسالة إلى المرأة:  Ujumbe Kwa Mwanamke
'Allaamah Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri:
Abu Bakr Khatwiyb al-Atrush

Bismi Allaahi Ar-Rahmaani Ar-Rahiym. Alhamdu Allaahi Rabil 'Aalamiyn. Swalah na salaam zimwendee Mtume wetu Muhammad (swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) na ahli zake na Maswahaba wake kwa jumla (radhiya Allaahu ´anhum).
Tumesikia kwenye hizi khutbah mbili zenye baraka khayr nyingi kutoka kwa Khatwiyb wetu - Allaah Ampe mafanikio. Kazungumzia masuala ya khatari, nayo ni masuala ya mwanamke.
Mwanamke enyi ndugu! Allaah Kamuumba kwa lengo kubwa katika maisha haya, kama Alivyomuumba mwanaume. Na kila mmoja ana umuhimu [kazi] Yake. Mwanaume ana kazi yake na mwanamke ana kazi yake. Kila mmoja akishikamana na kazi yake na kuitimiza, jamii itafikia khayr kubwa. Na ikiwa nidhamu itayumbishwa, ndiyo kunatokea kasoro nyingi. Kama mlivyosikia jukumu la mwanamke wakati wa Ujaahiliyyah (kabla ya kuja Uislamu), na jukumu lake leo kwenye miji ya kikafiri na kwa Waislamu wenye misimamo.


(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
 


Mkuu - teknolojia na taaluma

Zichume Sifa Kumi Njema - Sifa Ya Tano - Wanaume Wanaosubiri Na Wanawake Wanaosu
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

 
 
Zichume Sifa Kumi Njema - Sifa Ya Tano - Wanaume Wanaosubiri Na Wanawake Wanaosubiri

Anasema Allaah سبحانه وتعالى :

((إِنَّ الْمُسْلِمِينَ وَالْمُسْلِمَاتِ وَالْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ وَالْقَانِتِينَ وَالْقَانِتَاتِ وَالصَّادِقِينَ وَالصَّادِقَاتِ وَالصَّابِرِينَ وَالصَّابِرَاتِ ))

((Hakika Waislamu wanaume na Waislamu wanawake, na Waumini wanaume na Waumini wanawake, na watiifu wanaume na watiifu wanawake, na wasemao kweli wanaume na wasemao kweli, wanaosubiri wanaume na wanaosubiri wanawake ….)) [Ahzaab:35]


(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
 


Mkuu - teknolojia na taaluma

Unavaa 'NIKE', Je, Unajua Maana Yake?
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

 
 
Imetayarishwa na Abu Bakr Khatwiyb

Unavaa 'NIKE', Je, Unajua Maana Yake?

Sifa zote kamilifu njema anastahiki Allah Aliyetukuka Mola Mlezi wa wa walimwengu wote ambaye hana mshirika katika Ufalme Wake. Swalah na salamu zimshukiye kipenzi chetu Muhamad (Swala Allaahu 'alayhi wa sallam) ahli zake, sahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Ishara ya “NIKE” ikiwa ni kwa alama kama ya kupata kama ilivyo hapo juu au kwa neno lenyewe la “Nike” ambalo hutumiwa mara nyingi kuwekwa kwenye nguo za kuvaa au kwenye viatu vya michezo na mazoezi. Waislamu tunatakiwa kujiepusha kununua bidhaa hii, vile vile tujiepushe na kuivaa kwa wale ambao tayari wameshakuwa nayo majumbani.(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
 


Mkuu - teknolojia na taaluma

Matumizi Ya Kunufaisha Ya Habbat-sawdaa-3 (habba Soda - Chembe Nyeusi ) Sunnah -
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

 
 
Imefasiriwa Iliyasa binti Maulana

Asidi (Acidness)

Motone kadhaa ya mafuta ya Habbat-Sawdaa yaliotiwa kwenye maziwa ya moto na asali; humaliza asidi.

Uvimbe Wa Tumbo

Atachukuwa unga wa Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kimoja na kijiko cha urkusus (licorice) hivyo atavichanganya na juisi ya pea iliotengenezwa pamoja na kokwa zake; halafu anywe; ataona nafuu kubwa.


(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
 


Mkuu - teknolojia na taaluma

Matumizi Ya Kunufaisha Ya Habbat-sawdaa-2 (habba Soda - Chembe Nyeusi ) Sunnah -
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

 
 
Imefasiriwa na Iliyasa binti Maulana
Matumizi Ya Kunufaisha Ya Habbat-sawdaa-2 (habba Soda - Chembe Nyeusi ) Sunnah - Siyrah

(Itumieni habba hii, hakika ndani yake muna shifaa (ponyo) ya kila aina ya ugonjwa isipokuwa mauti)). (Al-Bukhaariy)

Kunyonyoka Nywele

Ataukanda unga wa Habbat-Sawdaa katika juisi ya chirichiri pamoja na kijiko cha siki nyepesi na kikombe cha mafuta ya zeituni, halafu asugue kichwani kwa mafuta hayo kila siku jioni pamoja na kukiosha kichwa kwa maji na sabuni kabla ya kupaka.(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
 


Mkuu - teknolojia na taaluma

Matumizi Ya Kunufaisha Ya Habbat Sawdaa-1 (haba Soda - Chembe Nyeusi )
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

 
 
Imefasiriwa na Iliyasa bint Maulaanah
Matumizi Ya Kunufaisha Ya Habbat Sawdaa-1 (haba Soda - Chembe Nyeusi )

Al-Bukhaariy anasimulia kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu 'anhu) kwamba Mtume Muhammad (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema.

((Habbat-Sawdaa inatibu kila kitu isipokuwa mauti)).

Yafuatayo hapa chini ni baadhi ya matatizo na magonjwa ambayo yanaweza kutibika kwa kirahisi kwa kutumia Habbat-Sawdaa.(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
 


Mkuu - teknolojia na taaluma

Ukweli Kuhusu Mazishi Ya Kiislamu
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

 
 
Bismillaahir Rahmaanir Rahiim
 
Kwa hakika kila sifa njema ni Zake Allaah, tunamtukuza Yeye, na tunamtaka msaada Yeye na tunamuomba msamaha Yeye. Tunajilinda kwa Allaah kutokana na maovu ya nafsi zetu na udhaifu wa vitendo vyetu. Aliyeongozwa na Allaah hakuna wa kumpoteza na aliyepotezwa na Allaah hakuna wa kumuongoza. Nashuhudia kuwa hapana apasaye kuabudiwa kwa haki ila Allaah na nashuhudia kuwa Muhammad ni mja Wake na Mtume Wake.(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
 


Mkuu - teknolojia na taaluma

Hukumu Za Janaazah
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

 
 
Imekusanywa Na: Shani Ahmad

Bismillahir Rahmaanir Rahiym
 

AlhamdulilLlaah, was swalaatu wa salaam ‘alaa Muhammadin (Salla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

Anapokuwa Katika Hali Ya Kutoka Roho

·         Wanaohudhuria mauti ya Muislam wanatakiwa wamlakinie Shahadah.(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
 


Mkuu - teknolojia na taaluma

Maovu Yanaofanyika Katika Sherehe Za ‘Arusi (Harusi)
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

 
 
Muhammad bin ‘Abdillaah Al-Habdaan
 

BismiLlaahi Rahmaanir Rahiym
Shukrani ni za Allaah na rehma na amani zimfikie Mtume wa Allaah na watu wake na Maswahaba zake na wanaowafuata hadi Siku ya mwisho.

Amma ba’ad;
Hakika furaha ni utulivu wa mioyo yetu, ni kipumbazo cha macho yetu. Wakati tunaposikia habari ya ‘Arusi (Harusi) kuwa fulani anamuoa fulani, jambo hili ni sababu ya kusimamisha (Sunnah) mwendo Aliouweka Mola na kwa njia hii ndio kuendelea kizazi cha viumbe.(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
 


Mkuu - teknolojia na taaluma

Fataawa Za Wanachuoni Kuhusu Mavazi Ya Mwanamke ‘Arusini Na Wanapokuwa Na Wanawa
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

 
 
Fataawa Za Wanachuoni Kuhusu Mavazi Ya Mwanamke ‘Arusini Na Wanapokuwa Na Wanawake Wenzao

Swali:

Nini shari'ah ya kiislamu kwa wanawake kuvaa nguo za wazi kabisa wanapohudhuria harusi, Kama kanzu fupi zinazoonyesha miguu au mikono yote kuwa wazi au kuvaa bega na moja liko wazi, baadhi ya au kifua kuwa wazi, au kanzu kumbana (tight) hadi mwili wote viungo vyake vinaonekana, au mgongo kuwa wazi n.k.. Je inaruhusiwa kwa vile wako mbele ya wanawake wenzao? ipi mipaka ya mavazi baina Yao?


(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
 


Mkuu - teknolojia na taaluma

Hijaab - Kuwajibika Kwake
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

 
 
Imefasiriwa Na Ummu ‘Aliy
Nataka kulenga shabaha kwenye mojawapo ya vifaa vya stara. Kitu muhimu katika maisha ya mwanamke ni Hijaab. Nitaanza na Hijaab ya wanawake.(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
 


Mkuu - teknolojia na taaluma

Kauli Za Maimaam Wanne Kuhusu Kushikamana Na Sunnah Na Kuacha Kufuata Rai Zao
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

 
 
Shaykh Muhammad Naaswirud-Diyn Al-Albaaniy 

Kauli Za Maimaam Wanne Kuhusu Kushikamana Na Sunnah Na Kuacha Kufuata Rai Zao


Imefasiriwa na  Abu 'Abdillaah Muhammad Baawazir kutoka kitabu cha: 'Swiffatus-Swalaatin-Nabbiy (Sifa ya Swalah ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kilichoandikwa na Shaykh Al-Albaaniy (Rahimahu Allaah)

Itakuwa ni manufaa makubwa ikiwa tutazieleza baadhi ya kauli zao hapa, kwani labda hii itamuonya mtu au itawakumbusha wale ambao wanafuata rai za Maimaam au madhehebu maalum, bali wanaofuata kwa upofu wale Waalimu au Mashaykh na wale walio chini ya daraja ya hao Maimaam wanne wakubwa[1]wakishikilia madhehebu yao au rai zao kama kwamba zimeteremeshwa kutoka mbinguni! Na hali Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema:(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
 


Mkuu - teknolojia na taaluma

Hukmu Ya Kufuga Ndevu
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

 
 
  Hukumu Ya Kuachilia Ndevu
 

Swahiyhu Fiqhus Sunnah

 
Kuachilia ndevu ni wajibu kwa wanaume kwa dalili zifuatazo:
1- Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameamuru kuziachilia. Amri hii ni ya lazima, kwani hakuna kiashirio chochote kinachoigeuza na kuipeleka katika usunnah. Na kati ya amri hizo ni neno lake Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):


(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
 


Mkuu - teknolojia na taaluma

Makos Tanayohusu Twawaaf, Sa'y, Yanayotendeka Minaa, Katika Kisimamo Cha &#
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

 
 
Makos Tanayohusu Twawaaf, Sa'y, Yanayotendeka Minaa, Katika Kisimamo Cha 'Arafah, Katika Eneo La Muzdalifah, Katika Sehemu Za Kurushia Mawe Kuzuru Kaburi La Mtume


Mahujaji wengine wanavuka kituo kilichoteuliwa kwa ajili ya ihraam katika njia za msafara wao bila ya kuwa katika hali ya ihraam au bila ya kuwa katika ihraam hapo. Wanaendelea hadi wanafika Jiddah au sehemu nyingine katika mipaka ya vituo ambako huko ndio wanaingia  katika hali ya ihraam.


(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
 


Mkuu - teknolojia na taaluma

MATUMIZI YA KUNUFAISHA YA HABBAT SAWDAA-1 -- (HABA SODA - CHEMBE NYEUSI )
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

 
 
Imefasiriwa na Iliyasa bint Maulaanah

Al-Bukhaariy anasimulia kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu 'anhu) kwamba Mtume Muhammad (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema.

((Habbat-Sawdaa inatibu kila kitu isipokuwa mauti)).

Yafuatayo hapa chini ni baadhi ya matatizo na magonjwa ambayo yanaweza kutibika kwa kirahisi kwa kutumia Habbat-Sawdaa.

Kwa faida ya Afya kwa ujumla:(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
 


Mkuu - teknolojia na taaluma

MAELEZO KWA UFUPI KUHUSU UISLAMU
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

 
 
 
تعريف موجز بالإسلام (بللغة السواحلية)


بسم الله الرحمن الرحيم

MAELEZO KWA UFUPI KUHUSU UISLAMU 

Kila sifa njema ni zake Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe vyote, sala na amani ziwe juu ya Imamu wa Mitume, Nabii wetu  Muhammad, na jamaa zake, na Masahaba wake wote.

Ama baada:_
   UISLAMU:_ ni kushuhudia kuwa hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu mmoja, na Muhammad (rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu, (kushuhudia) kwa moyo, na kwa ulimi, na kwa viungo.

Na (huo Uislamu) unajumuisha kuamini nguzo sita za Imani kwa kutekeleza nguzo tano za Uislamu, na nguzo mbili za Ihsani.(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
 


 

 
EsinIslam The Muslim World Portal For Islamics, News, Fatwas, Audios, Videos, Muslim News, Quranic Islamic Articles, Radio, Audio Quran, TV Channels, Fatwa Rulings, Muslim News Newspapers Magazines Headlines Articles Forums Schools, Universities, Colleges, Mosques, Qur'an, Hadith, Sunnah, Fiqh, Prayers, Salat, Fasting Ramadan, Vidoes, Books On EsinIslam.Com And Muxlima.Com

  :-: Go Home :-: Go Top :-: