Swahili
- Ukurasa Kuu    - Kumi Juu    - Mada Mpya    - Salimisha Habari    - Tafuta    - Kiswahili Jukwaa    - Kiswahili Wanachama    - Tathmini    - Ujumbe wa Kibinafsi    - Tafiti    - Majarida    - Hadithi Archive    - Maudhui    - Viungo vya Wavuti    - Vipakuliwa    - Maswali ya Kawaida    - Tunapendekeze    - Orodha ya Kuingia   

EsinIslam Media Swahili: Ulimwengu wa Kiislamu na masuala ya Kiis

Tafuta mada hii:   
[ Nenda nyumbani | Chagua Mada Mpya ]

Ulimwengu wa Kiislamu na masuala ya Kiis

Jinsi Ya Kumfurahisha Mumeo
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

   Shaykh Muhammad 'Abdul-Haliym Haamid Imetarjumiwa na Ummu Ummu Ayman Jinsi Ya Kumfurahisha Mumeo

1- Mapokezi mazuri 

a) Baada ya kurejea kutoka kazini, skuli, safarini, au popote pale palipowatenganisha, anza kwa maamkizi mazuri.

b) Mpokee kwa uso mchangamfu

c) Jipambe na ujitie manukato (Perfume)

d) Anza na habari nzuri na chelewesha habari yoyote mbaya mpaka atapokwisha pumzika

e) Mpokee kwa maneno ya mapenzi na hamu/shauku

f) Fanya jitihada kubwa katika mapishi mazuri na kitayarishe kwa wakati. 

(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
Ulimwengu wa Kiislamu na masuala ya Kiis

Jinsi Ya Kumfurahisha Mkeo
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

Shaykh Muhammad 'Abdul-Haliym Haamid Imetarjumiwa na Ummu Ummu Ayman..

Ili kusaidia familia za Kiislam na kueneza mafundisho ya Uislam katika kujenga familia, MSA (Muslim Students Association) katika Chuo Kikuu cha Alberta, Canada, kimetayarisha ufupisho wa tafsiri ya vitabu viwili. Vitabu katika lugha ya kiarabu vilivyotungwa na Shaykh Muhammad 'Abdul-Haliym Haamid. Mwanachuoni wa Kimisri, ambaye amemaliza masomo yake katika chuo cha Islamic University cha Madiyna An-Nabiwiyyah huko Saudi Arabia. Vitabu vyenyewe ni : 

1. Namna ya kumfurahisha Mkeo 

2. Namna ya kumfurahisha Mumeo Hivi ni vitabu vizuri kabisa vya Kiarabu ambavyo tumeviona katika somo hili. Vimekwenda mbali katika kuelezea, kuanzia haki na wajibu mpaka adaab (tabia njema) na kwenda mbali katika kutekeleza haki hizi katika maisha ya kila siku. Ufupisho ufuatao unamulika zaidi katika majukumu ya nini kinaweza au kinachotakiwa kifanywe. Kila jambo lililotajwa na muandishi limeegemezwa katika ushahidi wa Qur-aan, Sunnah au matendo ya Maswahaba, bali ushahidi haukuwekwa katika tafsiri hii. Ifuatayo ni tafsiri ya kitabu cha kwanza.

(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
Ulimwengu wa Kiislamu na masuala ya Kiis

Manufaa Na Matatizo Katika Ndoa
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

Manufaa Na Matatizo Katika Ndoa

Imefasiriwa Na: Ummu Ahmad MANUFAA KATIKA NDOA 1. Kupata kizazi ambacho kwanza kitasaidia katika ujengaji wa jamii, pili kueneza jinsia ya watu wa kila kabila au mataifa mbali mbali, na kubwa zaidi ni kuongeza idadi ya kizazi cha jamii ya kiislamu.
2. Kumridhisha Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) na Mtume Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), kwa kueneza idadi ya wafuasi wa dini ya Kiislamu.
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema katika hadithi sahihi:
“Oeni wake wema muwapendao na wataowapatia kizazi chema, kwani siku ya Qiyaamah nitajivunia ukubwa wa umati wangu.” [Ahmad]
3. Kupata baraka za mtoto mwema ambaye atakayemsomea dua mzee wake (atakapofariki). Maneno haya yamethibitishwa na Hadiyth maarufu inayosema kuwa:
“Binaadamu anapokufa, basi ‘amali zake nzuri hukatika au humalizika, isipokuwa mambo matatu makuu nayo ni: Sadaka yenye kuendelea, Elimu yenye kunufaisha na Mtoto mwema atakayemuombea du’aa mzee/wazee wake.” [Riyadhus-Swaalihiyn]
Faida nyenginezo zipatikanazo katika ndoa ni:

(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
Ulimwengu wa Kiislamu na masuala ya Kiis

Facebook Au Fitnabook
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

Ilyaasa bint Mawlaana

Facebook Au Fitnabook

Kwanza kabisa, ijulikane wazi kwamba kusudio la makala hii si kutoa fatwa wala hukumu. Lengo ni kuweka wazi manufaa na madhara ya Facebook ili mtu binafsi atoe hukumu yake mwenyewe.
Je, ni Facebook au Fitnabook? Hili ni suali ambalo watu wengi wameanza kujiuliza baada ya kujionea vitimbi na kashfa kadhaa katika huu mtandao ambao unazidi kujipatia umaarufu kila pembe ya dunia. Naam, kuna vitimbi kadhaa vinafanyika kwa jina la Facebook. Na ndio kuna vijana wengi ambao wametumbikia katika janga la fitna katika Facebook lakini nini suluhisho la hili?
Kabla hatujatazama hebu kwanza tuangalie manufaa na madhara ya Facebook.

(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
Ulimwengu wa Kiislamu na masuala ya Kiis

Zichume Sifa Kumi Njema - Sifa Ya Nane - Wanaume Na Wanawake Wanaofunga
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

Zichume Sifa Kumi Njema - Sifa Ya Nane - Wanaume Na Wanawake Wanaofunga

((إِنَّ الْمُسْلِمِينَ وَالْمُسْلِمَاتِ وَالْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ وَالْقَانِتِينَ وَالْقَانِتَاتِ وَالصَّادِقِينَ وَالصَّادِقَاتِ وَالصَّابِرِينَ وَالصَّابِرَاتِ وَالْخَاشِعِينَ وَالْخَاشِعَاتِ وَالْمُتَصَدِّقِينَ وَالْمُتَصَدِّقَاتِ وَالصَّائِمِينَ وَالصَّائِمَاتِ....))
Anasema Allaah سبحانه وتعالى:

((Hakika Waislamu wanaume na Waislamu wanawake, na Waumini wanaume na Waumini wanawake, na watiifu wanaume na watiifu wanawake, na wasemao kweli wanaume na wasemao kweli wanawake, na wanaosubiri wanaume na wanaosubiri wanawake, na wanyenyekevu wanaume na wanyenyekevu wanawake, na watoao sadaka wanaume na watoao sadaka wanawake, na wanaofunga wanaume na wanaofunga wanawake…)) [Al-Ahzaab:35]

Nini maana ya Swawm?(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
Ulimwengu wa Kiislamu na masuala ya Kiis

Tabia Za Mwenendo Wa Kiislamu
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

Tabia Za Mwenendo Wa Kiislamu
Imeandikwa Na ‘Abdur-Rahmaan A. Ash-Shiiha
Imetafsiriwa Na ‘Abdun-Naaswir Hikmany
Imechukuliwa Kutoka Kitabu Cha Mwandishi
“Ujumbe Wa Uislamu.”

Tabia Za Mwenendo Wa Kiislamu

Shari’ah ya Kiislamu imeasisi na kulingania ustaarabu mbali mbali wa jamii. Wakati huo huo, imetahadharisha kuwepo adhabu siku ya Qiyaamah pindipo mtu atakaposhindwa kushikamana na Shari’ah hizo. Imaam Muslim amepokea kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Je munamjua nani muflisi?)) Walijibu: ((Muflisi miongoni mwetu ni yule ambaye hana pesa wala mali.)) Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Muflisi ndani ya ummah wangu ni yule anayekuja siku ya Qiyaamah akiwa na Swalah, Zakaah na Swawm, hata hivyo alikuwa akivunjia heshima, kusengenya, kutukana na kuwapiga wengine.

(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
Ulimwengu wa Kiislamu na masuala ya Kiis

Yaliyokuwa Sunnah Na Bid'ah Katika Sherehe Za 'Iyd
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

Imefasiriwa na Ummu 'Abdil-Wahhaab
Yaliyokuwa Sunnah Na Bid'ah Katika Sherehe Za 'Iyd

BismiLLaahi wa AlhamduliLLaah wa swalaatu wa salaam 'alaa RasuliLLaah Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa aswahaabihi wa sallam.

“Kwa kila jamii ya watu kuna sikukuu, na hii ‘Iyd ndiyo sikukuu yetu” alisema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kumwambia Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu). [Al-Bukhaariy na Muslim].(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
Ulimwengu wa Kiislamu na masuala ya Kiis

Haki Hii Haki Gani Mbele Ya Allaah?
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

Haki Hii Haki Gani Mbele Ya Allaah?

Bint Ahmadah
Mwenyezi Mungu Anatusimulia moja ya visa vilivyomo katika Qur-aan Tukufu:

"Na Maryam mtoto wa 'Imraan aliyejihifadhi nafsi yake na Tukampulizia humo roho Yetu (inayotokana na Sisi), na akayasadikisha maneno ya Mola wake, na Vitabu Vyake; na alikuwa miongoni mwa wanyenyekevu (wakubwa)." (Suratu at-Tahrym: 12)(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
Ulimwengu wa Kiislamu na masuala ya Kiis

Baada Ya Kuhamia Madiynah: Mwenendo Wa Mitume ('Alayhimus Salaam)
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

Muhammad Faraj Saalim As-Sa’iy

Ndugu zangu Waislam, katika kalenda ya Hijri (Kalenda ya Kiislam) imeanza, na kwa ajili hiyo tutajikumbusha kidogo juu ya umuhimu wa siku hizi kwa ajili ya kuelewa umuhimu wake na kwa ajili ya kujifunza angalau machache juu ya Hijrah ya Mtume wetu mtukufu Muhammad (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) pamoja na Maswahaba wake watukufu (Radhiya Llaahu ‘anhu).

Mwaka jana katika mnasaba huu, tulisoma namna gani tukio la Hijrah lilivyokuwa muhimu kupita matukio yote yaliyopata kutokea katika historia ya Kiislam, na hii ni kwa sababu kutokana na Hijrah, taifa la mwanzo la Kiislam liliweza kuundwa, na Waislamu wakaweza kuweka miguu yao juu ya ardhi, madhubuti kwa ajili ya kuisimamisha dini yao, kuilinda itikadi yako, na kuweza kuieneza ulimwenguni kote.

(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
Ulimwengu wa Kiislamu na masuala ya Kiis

Makosa Ya Msingi Yaliyomo Ndani Ya Katiba Ya Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Kwa
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

Muhammad Baawazir

Makosa Ya Msingi Yaliyomo Ndani Ya Katiba Ya Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Kwa Mtazamo Wa Uislamu

Isbaal ni urefushaji wa kitu na makusudio hapa katika makala hii ambayo itazungumzia vazi la mwanamme, makusudio yake kishari’ah ni kuvaa kivazi chochote chenye kuvuka chini ya mafundo ya miguu kwa mwanamme; iwe ni kikoi, shuka, kanzu, joho au suruali.  Nalo ni jambo lenye kukatazwa na limeharamishwa kwa nuswuus (maandiko) mbalimbali ya kishari’ah kutoka katika Hadiyth za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
Ulimwengu wa Kiislamu na masuala ya Kiis

Isbaal Vazi La Mwanamme Lenye Kuvuka Mafundo Ya Miguu (Uburuzaji Au Kuburura)
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

Muhammad Baawazir

Hapa chini tutaona hoja au madai tata za wanaotetea kuburuza/ kuburura nguo na majibu dhidi ya madai hayo.

Hoja Mojawapo:

Kuwa Isbaal Inawahusu Wenye Kuvaa Kwa Kiburi Au Kwa Fakhari Tu

Baadhi ya watu wanarukhusu Isbaal kwa kudai kuwa makatazo yaliyokuja katika Hadiyth mbalimbali ni kwa wale tu wanaovaa kwa kiburi au kujifakharisha. Ima kwa wale wanaovaa tu bila kukusudia kiburi basi inafaa na hakuna ubaya wowote.(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
Ulimwengu wa Kiislamu na masuala ya Kiis

Wasiya Wa Kishari'ah Wa Muislamu Kabla Hajafariki
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

بسم الله الرحمن الرحيم

((وَاتَّقُواْ يَوْمًا تُرْجَعُونَ فِيهِ إِلَى اللّهِ ثُمَّ تُوَفَّى كُلُّ نَفْسٍ مَّا كَسَبَتْ وَهُمْ لاَ يُظْلَمُونَ))

((Ogopeni Siku Ambayo Mutarudishwa Kwa Allaah Kisha Kila Nafsi Italipa Kila Lile Ililochuma Na Wao Hawatadhulumiwa)) (Al-Baqarah: 281)
 
Utangulizi

Shukrani zote Anastahiki Allaah, Mola wa walimwengu wote. Swalah na amani ziwe juu ya aliyetumwa awe ni Rehma kwa ulimwengu wote Mtume Muhammad Mtume صلى الله عليه وآله وسلم    Ahli zake, Swahaba na wale ambao wamefuata Sunnah zake mpaka siku ya mwisho.

(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
Ulimwengu wa Kiislamu na masuala ya Kiis

Rudi Tena Ukaswali, Kwani Hukuswali Kwa jina la Allaah, Mwingi wa Rehma, Mwenye
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

Rudi Tena Ukaswali, Kwani Hukuswali

Imeandikwa na Muhammad Ash-Shariyf

Imefasiriwa na Ilyaasa Mawlaana

Sehemu Ya Kwanza

Kwa jina la Allaah, Mwingi wa Rehma, Mwenye KurehemuKatika usiku wa giza, Abu Lu’lu’ Al-Majuusi alijificha katika vivuli akijiandaa kwa ajili ya Swalaah ya Alfajiri, wakati ambapo ataendesha mipango yake ya kishetani kumuua Amiyr wa waumini – ‘Umar bin Al-Khattwaab (Radhiya Allahu ‘anhu).(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
Ulimwengu wa Kiislamu na masuala ya Kiis

Kazi Katika Uislam: UTANGULIZI, HADHI YA KAZI, KAZI ZILIZOHARAMISHWA,
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

Uislamu Na Shari'ah Zake
UTANGULIZI

Kulingana na Kamusi ya Kiingereza ya Collins, kazi imefafanuliwa kama juhudi za kimwili au kiakili zilizoelekezwa kufanya/ kutengeneza kitu, malipo anayopewa kwa amali, biashara, utaalamu, shughuli au ufahamu.(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
Ulimwengu wa Kiislamu na masuala ya Kiis

Hajj: Hatua Kwa Hatua: Tazama Televisheni Ya Saudi Arabia kujua wanayofanya Mahu
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

1 – 7 Dhul-Hijjah – Makkah au Madiynah

Kuzuru Msikiti wa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم  au kuweko Makkah kufanya 'Umrah (kwa Wanaofanya Hajjut-tamattu'u) na kuendelea kuswali hapo Masjidul-Haraam.(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
Ulimwengu wa Kiislamu na masuala ya Kiis

HADIYTH ARUBAINI ZA IMAAM AN-NAWAWIY NA TAFSIYR YA KISWAHILI
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

The Forty 40 Hadith Of Imam An-Nawawiyy Arabic Scripts And Full Swahili Translation

Example:

الحديث الأول

" إنما الأعمال بالنيات "

HADITHI YA 1

KILA KITENDO KWA NIA NIA YAKE(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
EsinIslam The Muslim World Portal For Islamics, News, Fatwas, Audios, Videos, Muslim News, Quranic Islamic Articles, Radio, Audio Quran, TV Channels, Fatwa Rulings, Muslim News Newspapers Magazines Headlines Articles Forums Schools, Universities, Colleges, Mosques, Qur'an, Hadith, Sunnah, Fiqh, Prayers, Salat, Fasting Ramadan, Vidoes, Books On EsinIslam.Com And Muxlima.Com

  :-: Go Home :-: Go Top :-: