Swahili
- Ukurasa Kuu    - Kumi Juu    - Mada Mpya    - Salimisha Habari    - Tafuta    - Kiswahili Jukwaa    - Kiswahili Wanachama    - Tathmini    - Ujumbe wa Kibinafsi    - Tafiti    - Majarida    - Hadithi Archive    - Maudhui    - Viungo vya Wavuti    - Vipakuliwa    - Maswali ya Kawaida    - Tunapendekeze    - Orodha ya Kuingia   

EsinIslam Media Swahili: Habari Idadi ya habari na hadithi Makala

Tafuta mada hii:   
[ Nenda nyumbani | Chagua Mada Mpya ]

Habari Idadi ya habari na hadithi Makala

Vidokezo Muhimu Kwa Wazazi Wenye Wasichana Na Wavulana
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

 Imefasiriwa na Ummu 'Abdil-Wahhaab Vidokezo Muhimu Kwa Wazazi Wenye Wasichana Na Wavulana

((ALHIDAAYA imerekebisha baadhi ya majina na usemi ili makala ifahamike vizuri na Jamii yetu))

NINI WAZAZI WAFANYE ILI VIJANA WAO WAWE NI WAISLAMU WENYE KUTEKELEZA UISLAMU KWA VITENDO?

1. Yatilie Bidii Malezi Kuliko Hata Kazi Yako Ya Kutwa NzimaHii ina maana kwamba wazazi wote wawili ni lazima waelewe kuwa watoto wao ni wa kweli kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala), na baba atakuja kuulizwa vipi kawalea watoto wake. Ikiwa watoto wao hawatokulia katika kuutekeleza Uislamu kwa sababu ya mapuuza ya wazazi wao, halitokuwa ni jambo la kukubalika kwa maisha ya hapa duniani na hata ya baadae.

2. Punguza Au Badilisha Masaa Ya Kazi Kwa Ajili Ya Kupata Muda Wa Kuwa Pamoja Na Familia YakoNi bora kuwa na kazi moja yenye muda wa kudumu, anasa chache katika nyumba (yaani sio magari mengi, nguo za gharama nyingi, nyumba kubwa ya fakhari, televisheni kila pahali), na muda zaidi wa kuwa pamoja na familia, kuliko kuwa na mambo mengi ya anasa na kukakosekana malezi. Haya yote yanawahusu mababa na mamama. Wazazi hawawezi kuwafunza watoto wao bila ya wao kuwepo nao kikawaida. Acha kazi za ziada kwenye siku za mwisho wa wiki au kazi za jioni na badala yake nenda na watoto msikitini kwa ajili ya Halaqah (darsa za dini) na shughuli nyenginezo. Au tilia maanani kugeuza nyakati za kazi ili uwe nyumbani wakati ambao watoto wapo.

(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
Habari Idadi ya habari na hadithi Makala

Vazi Lipi Lililo Bora Mbele Ya Allaah?
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

Bint Ahmadah

Amri kuu aliyopatiwa mwanamke wa Kiislamu inayomtofautisha na ndugu yake wa kiume ni ile inayosema: "Ee Mtume! Waambie wake zako, na binti zako, na wanawake wa Kiislamu wajiteremshie uzuri nguo zao. Kufanya hivyo kutapelekea upesi wajulikane wasiudhiwe." (Suratul-Ahzaab: 59)

Vipi kuvaa nguo leo hii imekuwa viroja kwa Waislam? Kwani wamesahau mavazi yao, leo imekuwa watafuta kila mavazi kisha tunasema yetu, kisa tumejisahau lipi lililotulazimu kwetu na lililo muhimu kwetu na kwa Mola wetu?

(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
Habari Idadi ya habari na hadithi Makala

Umuhimu Wa Kuchunga Wakati
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

Umuhimu Wa Kuchunga Wakati Kwa Muislamu

Abu Bakr Khatwiyb Al-Atrush

Namshukuru Allaah ambaye Ameniwezesha kuandaa makala hii muhimu ambayo itagusia sana umuhimu wa Muislamu kuchunga muda wake na kutokuuangamiza kwa kufanya mambo ya kipuuzi ambayo hayatomsaidia si duniani wala Akhera. Waislamu wengi tunashinda siku kutwa na kujishughulisha na mambo ya kipuuzi ambayo mengi katika hayo hayamridhishi Allaah.

(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
Habari Idadi ya habari na hadithi Makala

Zichume Sifa Kumi Njema - Sifa Ya Kumi (Ya Mwisho) Wanaume Na Wanawake Wanaomdhu
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

Zichume Sifa Kumi Njema - Sifa Ya Kumi (Ya Mwisho) Wanaume Na Wanawake Wanaomdhukuru sana Allaah

Anasema Allaah سبحانه وتعالى:
إِنَّ الْمُسْلِمِينَ وَالْمُسْلِمَاتِ وَالْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ وَالْقَانِتِينَ وَالْقَانِتَاتِ وَالصَّادِقِينَ وَالصَّادِقَاتِ وَالصَّابِرِينَ وَالصَّابِرَاتِ وَالْخَاشِعِينَ وَالْخَاشِعَاتِ وَالْمُتَصَدِّقِينَ وَالْمُتَصَدِّقَاتِ وَالصَّائِمِينَ وَالصَّائِمَاتِ وَالْحَافِظِينَ فُرُوجَهُمْ وَالْحَافِظَاتِ وَالذَّاكِرِينَ اللَّهَ كَثِيرًا وَالذَّاكِرَاتِ أَعَدَّ اللَّهُ لَهُم مَّغْفِرَةً وَأَجْرًا عَظِيمًا ﴿35﴾
((Hakika
Waislamu wanaume na Waislamu wanawake, na Waumini wanaume na Waumini wanawake, na watiifu wanaume na watiifu wanawake, na wasemao kweli wanaume na wasemao kweli wanawake, na wanaosubiri wanaume na wanaosubiri wanawake, na wanyenyekevu wanaume na wanyenyekevu wanawake, na watoao sadaka wanaume na watoao sadaka wanawake, na wanaofunga wanaume na wanaofunga wanawake, na wanaojihifadhi tupu zao wanaume na wanawake na wanaomdhukuru Allah kwa wingi wanaume na wanawake, Allah Amewaandalia msamaha na ujira mkubwa)) [Al-Ahzaab:35]

(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
Habari Idadi ya habari na hadithi Makala

Mtume (Swalla Llaahu ĎAlayhi Wa Sallam) Akiwa Madiynah
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

Mtume (Swalla Llaahu ‘Alayhi Wa Sallam) Akiwa Madiynah

Anasema Shaykh Abu Bakr Al-Jazairiy:

"Hakika ya miaka yote kumi na tatu aliloishi Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) pale Makkah tokea alipopewa utume mpaka siku ile aliyohama kwenda Madiynah, yote ilikuwa ni maumivu na machozi na huzuni. Hakupata kufurahi hata kwa muda wa saa moja au kustarehe angalau kwa siku moja.(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
Habari Idadi ya habari na hadithi Makala

Maslahi Ya Jamii Ndani Ya Shari'ah
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

'Abdun-Naaswir Hikmany

Utangulizi:
 
Uswuulul-Fiqhi yaani Maarifa ya Sheria ya Kiislamu inaweza kutafsiriwa kuwa ni utaratibu wa kutoa kanuni kutoka Shariah Kuu (Qur-aan na Sunnah).(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
Habari Idadi ya habari na hadithi Makala

Yampasayo Maiti
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

Imetayarishwa Na Sa’iyd Na Khamiys
 
Kila sifa njema anastahiki Allah na rehma na amani zimfikiye Mtume Muhamad na ahli zake na sahabaze na wenye kufuwata wayo kwa ihsani mpaka siku ya mwisho,
 
Ama baa’d(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
Habari Idadi ya habari na hadithi Makala

Mwito Kutoka Masjidul-Haraam Kwa Wanawake Wote Waislamu Ulimwenguni!
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

Sheikh 'Abdur-Rahmaan As-Sudaysi
Imefasiriwa kwa lugha ya kiswahili na  Ummu Ali

Mwito Kutoka Masjidul-Haraam Kwa Wanawake Wote Waislamu Ulimwenguni!

Sifa zote ni za Allah, Mwingi Wa Rehma Mwenye Kurehemu. Rehma na amani zimshukie Mtume Muhammad صلى الله عليه وسلم.
 
Dada zangu waislamu, hamutaweza kufikia ukamilifu munaotaka, hamutaweza kurudisha taadhima ya kale, wala kufikia daraja ya juu kabisa, isipokuwa mukifuata mafundisho ya Kiislamu na musipite mipaka ya sheria. Hii itawafanya nyoyo zenu zipende na kuthamini mitindo mizuri na kuepukana na mitindo mibaya.(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
Habari Idadi ya habari na hadithi Makala

Ingia Katika Milango Mingi Ya Kheri Ya Ramadhaan
(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )

Mwezi huu mtukufu umejaa fursa ya kujichumia mengi ya kheri ambayo thawabu zake huanzia tokea kumi hadi zaidi ya mia saba pamoja na malipo maalum yatokayo kwa Allaah kwa Mfungaji, kama alivyosema Mtume صلى الله عليه وآله وسلم

(Kusoma Zaidi Wa Habari Hii / Kukaa Bidhaa ... | More | Esin )
 
EsinIslam The Muslim World Portal For Islamics, News, Fatwas, Audios, Videos, Muslim News, Quranic Islamic Articles, Radio, Audio Quran, TV Channels, Fatwa Rulings, Muslim News Newspapers Magazines Headlines Articles Forums Schools, Universities, Colleges, Mosques, Qur'an, Hadith, Sunnah, Fiqh, Prayers, Salat, Fasting Ramadan, Vidoes, Books On EsinIslam.Com And Muxlima.Com

  :-: Go Home :-: Go Top :-: