Swahili
- Ukurasa Kuu    - Kumi Juu    - Mada Mpya    - Salimisha Habari    - Tafuta    - Kiswahili Jukwaa    - Kiswahili Wanachama    - Tathmini    - Ujumbe wa Kibinafsi    - Tafiti    - Majarida    - Hadithi Archive    - Maudhui    - Viungo vya Wavuti    - Vipakuliwa    - Maswali ya Kawaida    - Tunapendekeze    - Orodha ya Kuingia   

 

 
Elimu Ni Wajibu Kwa Mwanamke Wa Kiislamu - ELIMU ANAZOPASWA KUSOMA MWANAMKE
 
 
Waislamu Wanawake - maisha yao na Famili  Mfumo Na Muelekeo Wa Nyaraka Hizi Umechukuliwa Kutoka Kwa Kijitabu Kinachoitwa 

“Al-Mar’at Al-Muslimah Fiy Twalabil ‘Ilm”  Elimu Ni Wajibu Kwa Mwanamke Wa Kiislamu - ELIMU ANAZOPASWA KUSOMA MWANAMKE (Mwanamke Muislamu Katika Kutafuta Elimu)

Kilichochapishwa Na Daarul Arqam,  Chapa Ya Pili,

ELIMU ANAZOPASWA KUSOMA MWANAMKE1 KUSAHIHISHA UFAHAMU MBAYA: 

Huenda wakaona baadhi ya watu kuwa mwanamke wa Kiislamu hana uwezo wa kusoma na kusomesha. Na kuwa kuna vikwazo vya kisheria ya dini ya Kiislamu vinavyozuia harakati zake katika jambo hili. Muono huu ni wa makosa unaotokana na ufahamu mbaya wa Uislamu, kwani Uislamu ni nidhamu kamili ya Maisha. Yule anayeangalia kwa kina hali ya mwanamke na harakati zake katika chimbuko la Uislamu na duru yake katika historia kuanzia hasa wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Makhalifa Waongofu (Radhiya Allaahu ‘anhum) ataona hayo. Kinachotakikana leo kutoka kwa mwanamke Muislamu ni kujinyanyua kwa kila njia ili atekeleze majukumu yake ya kihistoria na kuutengeneza Ummah. 

2 MASHARUTI YA MUAMKO: 

 Uislamu umempatia mwanamke na mwanamume amana ya Dini ambayo ni amana muhimu katika Maisha, bali ndio nguzo na msingi. Uislamu ulimjaalia kila mmoja ni mchungaji hasa katika kusahihisha na kuweka sawa ‘Aqiydah yake, ibadah zake, maadili yake na amali zake. Yule ambaye hatasoma hukumu za ‘ibadah na mafungamano na mahusiano na Allaah na mfumo wa utamaduni … na yule asiyesoma Misingi ya ‘aqiydah na asiye dhamini falsafa ya kweli na muelekeo wa jamii na ubora wa maadili na malengo ya maisha na misingi ya adabu, asiyesoma au kufundishwa haya na yote ni katika milango ya elimu na yenye kuondosha mateso ya ujinga na giza la hisia na maaddah ameingia katika dhambi la kupunguza. Na hapo ameitia nafsi yake katika kazi ya kubaki myuma katika ulimwengu na Akhera.


Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) Anasema:

“Enyi Mulioamini! Jiokoeni nafsi zenu na watu wenu, na moto ambao kuni zake ni watu na mawe”. 

Na neno ‘Mulioamini’ linajumlisha Waumini wanaume na wanawake kwa sifa ya mwisho. Hataweza mmoja wao (mume au mke) kujiepusha yeye na watu wake na Moto ila anapojifundisha au kusoma haki ya Mola wake na haki katika maisha yake.

Katika ulazima wa muamko kwa mwanamke wa Kiislamu leo ni kufundishwa mambo ya dini yake. Imepokewa na Mu‘awiyah bin Abi Sufyan (Radhiya Allaahu ‘anhu) kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Yeyote ambaye ametakiwa kheri na Allaah, Humfahamisha dini”.

Inabidi mwanamke afundishwe ‘ibadah na maamrisho ya Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) kama yalivyo katika Suratun Nuur na Ahzaab. Aya za hukumu ni wajibu kwa kila Muislamu mwanamke kuzifahamu wala sio kuzisoma tu, kwani maarifa ya mazingatio na ufahamu na utekelezaji unamfanya yeye ajiamini wakati wa fitna ambao tumeonjwa nao leo na wasiokuwa na dini na wenye kutia shaka na maadui na wanafiki. Hawa wote wanajitahidi kuwaingiza Waislamu katika ujinga usiokuwa na huja wala muongozo kutoka katika Kitabu na Sunnah. Wanajaribu kuukashifu na kuutia aibu na dosari Uislamu na sheria inayomhusu mwanamke. Kwa hivyo ni wajibu kwa wanawake wa Kiislamu kutafuta elimu ya mambo ya dini yake na sheria inayo wahusu wao katika Maisha yao na adabu zao na umbile lao.

Jukumu la mwanamke katika myumba na watoto sio sahali. Imepokewa na Ibn ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) kuwa amemsikia Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Kila mmoja ni mchunga na kila mchunga ataulizwa kwa alicho kichunga … na mwanamke ni mchungaji katika nyumba ya mumewe naye ataulizwa kwa alicho kichunga…” kazi hii ina pande nyingi, miongoni mwao ikiwa ni ya uchumi, siha na afya, ya jamii, ya malezi na ya idara.

Iliyo muhimu kabisa ni sehemu anayochukuwa ya kulea watoto nayo ni duru ya kunyonyesha kimawazo na adabu, fikra na maadili na huo ni msimamo hatari anaoutoa mwanadamu kwa mwanadamu mwenziwe. Inatakikana asome masomo ya kumuandaa na majukumu ya kukamilisha maarifa na ufahamu wake wa Uislamu mpaka awe kiigizo na uwezo kamili. Mwanamke anachukuliwa mwenye majukumu ambayo yan athari katika Maisha yake ya kifikra na ya kinafsi.

Mfumo huu wa Uislamu unamsaidia mwanamke, bali unamlazimisha kuwa na utamaduni na elimu ambayo hatuioni katika sheria na tamaduni nyenginezo na tunahesabu haya kuwa si maudhui ya khilafu. Kutafuta elimu sio tu haki ya mwanamke bali ni faradhi kwake na ni wajibu wake, ni juu yake au jamii kuchukua nafasi ya dola kumrahisishia hilo. 

Elimu inatakikana, nayo ni elimu ya dini yake na kila maarifa yanayofungua masikio yake na kuzindua dhamira yake. Kutengeneza maisha yake kwa ujumla na kuyaona kwa Misingi ya umuhimu wake na malengo ya ndoa na umama wa kiroho na kijamii. Na kutekeleza wajibu wake katika kutengeneza hali za hisia na za nafsi ili kutekeleza amali kwa mujibu wa kanuni za kindoa na za mama na hakika ya utu wake na kutekeleza risala ambayo amewajibika kuifikisha katika Maisha yake.

3 AINA ZA ELIMU:

Mambo yanayompatia Faida mwanamke Muislamu katika kutafuta elimu ni Hadithi inayofuata. Imepokewa na Ibn ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Elimu ni aina tatu, mbali na hizo ni fadhila: Ayah muhkamah, au Sunnah qaimah au faridhah ‘adilah”.

Hadithi hiyo juu inatufahamisha kwa uhakika elimu zilizo faradhi. Nazo ni kama zinazofuata:

· Ayah Muhakamah ni elimu ambazo zinazo bainisha halali na haramu katika Uislamu.
· As-Sunnah al-Qaimah ni ambazo zinaelezea Kitabu cha Allaah na kuzielezea kwa kina.
· Al-Faridhah al-‘Adilah ni elimu ambayo inampatia kila mwenye haki, haki yake. Inaingia faradhi hii kwa Muislamu yale mambo ambayo wanazuoni wameita Faradhi Kifaya. Nayo ni kusoma masomo yatakayokuwa na maslahi kwa Waislamu na Uislamu. Imaam al-Ghazali anatueleza yafuatayo: 

“Ama Faradhi Kifaya katika elimu ni masomo yote yanayosimamisha mambo ya kidunia, kama utabibu (udaktari) kwani ni dharura kuiweka miili katika siha mzuri na hesabu ambayo ni dharura katika mahusiano na kugawanya mirathi na wasia na nyenginezo. Na masomo haya lau yakiachwa na watu katika nchi basi watu wake watakuwa katika makosa. Lakini anaposimama mtu mmoja ambaye atatosheleza katika kutekeleza wajibu basi wengine watakuwa hawana makosa. Wala usione ajabu kwa maneno yetu kuwa udaktari na hesabu ni katika Faradhi Kifaya. Pia Misingi ya utengenezaji wa vitu (sinaa) na siyasa, ushonaji na kuumika (hajjamah), ukulima na kufuma ni miongoni mwa Faradhi Kifaya”.
Masomo aliyoyataja Imaam al-Ghazali ni kwa njia ya mfano wala sio yote. Kusoma kwa wanawake katika elimu hizi na nyenginezo ni miongoni mwa Faradhi Kifaya na zipo ndani ya fani muhimu. Msingi wa Fikihi unasema, “Isipotimia wajibu ila kwa jambo Fulani basi jambo hilo pia linakuwa ni wajibu”. Kwa hivyo, elimu ya Lugha ya Kiarabu inaingia katika kuufahamu Ayah Muhkamah na Sunnah Qaimah. Elimu ya hesabu inaingia katika kuufahamu Faradhi ‘Adilah.

Tukizungumzia ufahamu wa fani na mgawanyo wa Faradhi Kifaya tutaona masomo kadhaa yaliyotajwa na Imaam al-Ghazali yanaingia katika fani za kike. Nazo ni udaktari, ushonaji, kuumika na tunaweza kuongezea nyenginezo kama ualimu, biashara, ukunga, n.k. Tunatakikana tusisahau msingi wa pili unaosema: “Dharura inakadiriwa kwa kiasi chake”. Inayozidi kile kipimo cha dharura, ndio Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekiita fadhila au ziada, na hukumu yake katika Fikihi ni kuruhusiwa.

Ni vizuri zaidi awe daktari anayetibu wanawake, mwanamke mfano wao. Mwalimu wa wanawake na watoto wadogo awe mwanamke. Kusimama kwa mwanamke katika mambo haya muhimu kama kusomea udaktari, ualimu, malezi ya watoto na kufanya Da‘wah kwa wengineo. Pia wanatakiwa wajitahidi waingie katika nyanja za elimu za vitu hai (Zoology), utaalamu wa madawa (Pharmacy), saikolojia na elimu ya jamii, malezi ya kujenga utu wa watoto na elimu ya kutumia njia za kisasa na mawasiliano kuandaa magazeti, majarida, vipindi vya idhaa katika redio na runinga na kutumia kompyuta katika Da‘wah na kufundishia.

Uhandisi mekaniki haujaharimishiwa mwanamke katika Uislamu lakini si maslahi ukilinganisha na maumbile yake. Sisi hatutakikani tubadilike kwa kasi kubwa kama ilivyobadilika Bara Ulaya kitu kilichopelekea kuzorota kwa maadili. Tusibadilike kufuata mila na desturi za Wazungu zinazoenda kinyume na akhlaqi za Kiislamu.
 
 
 Posted By Posted juu ya Saturday, March 09 @ 17:35:58 PST na MediaSwahiliTeam
 
 
:-: Go Home :-: Go Top :-:
 
 
 
Comments & Debates :-: التعليقات والمحاورات

 
 
For Your Membership Comments And Registered Debates Please, See Below Or Register Here :-: للحصول على تعليقات عضويتك و مناقشات الأعضاء انظر من فضلك أدناه أو سجّل هنا
 
 
:-: Go Home :-: Go Top :-:
 

Kuhusiana Viungo

· zaidi Waislamu Wanawake - maisha yao na Famili
· Habari na MediaSwahiliTeam


Kweli kusoma hadithi kuhusu Waislamu Wanawake - maisha yao na Famili:
Elimu Ni Wajibu Kwa Mwanamke Wa Kiislamu - MIFANO YA WANAWAKE WATUKUFU


Kifungu Rating

Wastani matokeo: 0
Kura: 0

Tafadhali chukua ya pili na kupiga kura kwa ajili ya makala hii:

bora Vizuri Sana Mema Kawaidar Mbaya

Chaguzi


 Chapa Rafiki Chapa Rafiki


 

 
EsinIslam The Muslim World Portal For Islamics, News, Fatwas, Audios, Videos, Muslim News, Quranic Islamic Articles, Radio, Audio Quran, TV Channels, Fatwa Rulings, Muslim News Newspapers Magazines Headlines Articles Forums Schools, Universities, Colleges, Mosques, Qur'an, Hadith, Sunnah, Fiqh, Prayers, Salat, Fasting Ramadan, Vidoes, Books On EsinIslam.Com And Muxlima.Com

  :-: Go Home :-: Go Top :-: