Swahili
- Ukurasa Kuu    - Kumi Juu    - Mada Mpya    - Salimisha Habari    - Tafuta    - Kiswahili Jukwaa    - Kiswahili Wanachama    - Tathmini    - Ujumbe wa Kibinafsi    - Tafiti    - Majarida    - Hadithi Archive    - Maudhui    - Viungo vya Wavuti    - Vipakuliwa    - Maswali ya Kawaida    - Tunapendekeze    - Orodha ya Kuingia   

 

 
Elimu Ni Wajibu Kwa Mwanamke Wa Kiislamu - MSIMAMO WA UISLAMU KATIKA KUSOMESHA W
 
 
Waislamu Wanawake - maisha yao na Famili  Mfumo Na Muelekeo Wa Nyaraka Hizi Umechukuliwa Kutoka Kwa Kijitabu Kinachoitwa 

“Al-Mar’at Al-Muslimah Fiy Twalabil ‘Ilm”  

Elimu Ni Wajibu Kwa Mwanamke Wa Kiislamu - MSIMAMO WA UISLAMU KATIKA KUSOMESHA WANAWAKE 

 (Mwanamke Muislamu Katika Kutafuta Elimu)

Kilichochapishwa Na Daarul Arqam,  Chapa Ya Pili, 

MSIMAMO WA UISLAMU KATIKA KUSOMESHA WANAWAKE 1 WAJIBU WA KUSOMESHWA WANAWAKE:

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Kutafuta elimu ni faradhi (lazima) kwa kila Muislamu”. Tunaona kuwa mwanamke yumo ndani katika ujumla wa Hadithi kwani Muislamu anakuwa mume au mke na wote ni sawa. Yeyote atakaye ingia katika hukumu za kisheria ataona kuwa kwa hakika wanawake ni ndugu za wanaume wala hawana hukumu hasa kwao wao ila baadhi ya hukumu zinazotofautisha baina ya maumbile ya wanaume na wanawake. Asili ni kuunganisha sheria na ujumla wa maneno wala haijathubutu utofauti ila kwa dalili. Mwanamke ni sawa na mwanamume katika majukumu ya ibadah za kinafsi (Dhikri, Swalah, Swaumu, Zakah, Hajj, n.k.) na katika maadili na mahusiano (ukweli, uadilifu, wema, taqwa na adabu) na Maisha kwa ujumla (subira, hijrah, kinyume cha ukafiri, twaa, kuwa pamoja na kikundi cha Waumini, urafiki na usaidizi).


Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) Anasema: 

“Bila shaka wanaume wenye kufuata vizuri nguzo za Uislamu na wanawake wanaozifuata vizuri nguzo za Uislamu, na wanaume wanaoamini vizuri nguzo za Imani na wanawake wanaoamini vizuri nguzo za Imani, na wanaume wanaotii na wanawake wanaotii, na wanaume wasemao kweli na wanawake wasemao kweli, na wanaume wanaosubiri na wanawake wanaosubiri, na wanaume wanaonyenyekea na wanawake wanaonyenyekea, na wanaume wanaotoa sadaka (na Zakah), na wanawake wanaotoa sadaka (na Zakah), na wanaume wanaofunga na wanawake wanaofunga, na wanaume wanaojihifadhi tupu zao na wanawake wanaojihifadhi tupu zao, na wanaume wanaomtaja Allaah kwa wingi na wanawake wanaomtaja Allaah kwa wingi. Allaah Amewaandalia msamaha na ujira mkubwa”.

Na kwa haya ni bayana kabisa kuwa mwanamke ana haki ya kupata elimu kama ilivyo haki ya kakake. Kama tunavyoona haki yake ya kufundisha. Tunaona kwa uwazi kabisa ile sheria ya taklifu iliyompatia uwezo haijapungua ya mwanamume hasa yanayohusu upande wa jamii na uchumi katika maisha yake. Haya yote hayatimu bila elimu hata lau kwa kadiri ya mambo ya sahali, anaweza kuendesha mambo yake kwa kushirikiana na mwanamume. 

Dalili nyengine iliyoonekana kuwa Uislamu unaita katika kumuelimisha mwanamke ni kuwepo wanawake wakati wa Utume, vikao vya elimu. ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha) alikuwa akisikika kwa fatwa zake na wanawake walikuwa wakijadili rai zake na huku Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) yupo pamoja na Makhalifa zake. Mwanamume anahitaji kulingania katika njia ya Allaah (Da‘wah) na wanawake wanalazimika kufanya hivyo. Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) Anasema: 

“Na ni nani asemaye kauli bora zaidi kuliko aitaye (viumbe) kwa Allaah na akafanya vitendo vizuri na husema: ‘hakika mimi ni miongoni mwa Waislamu”. Anasema tena Allaah, “Sema: Hii ndio njia yangu ninaita kwa Allaah kwa ujuzi na uoni wa ukweli, mimi na kila wanaonifuata”. 

Haya yanakusanya wanaume na wanawake sawa sawa.

Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) katika aya nyengine amelifanya jukumu la Da‘wah kwa wanaume na wanawake kwa kuwataja hasa. Anasema (Subhaanahu Wa Ta’ala):

“Na waumini wanaume na wanawake, ni marafiki na wasaidizi wao kwa wao. Huyaamrisha yaliyo mema na huyakataza yaliyo mabaya…”

Uislamu ni dini ya Da‘wah na utangazaji na Da‘wah ni faradhi kwa kila Muislamu mwanamume na mwanamke. Kila mmoja kwa uwezo wa nguvu zake na kwa kadiri ya amali yake na katika mipaka ya sheria iliyo sawa sawa.

Je, inawezekana kwa mjinga kutekeleza faradhi hii? Elimu ni sharuti katika kutekeleza na kufanya Da‘wah. Tunaporudia makaratasi ya Historia ya Kiislamu, tutaona nuru ya watukufu wa kike ambao walitekeleza amana ya Da‘wah katika njia ya Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) na Mtume Wake na kazi ya kuueneza Uislamu na kuulinda… kuanzia wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na karne zilizofuata mpaka leo.

2 FADHILA ZA KUMSOMESHA MWANAMKE:

Mkazo wa kuwapatia elimu watoto umechanganya wavulana na wasichana. Lakini Uislamu umeupatia fadhila kubwa zaidi kuwalea wasichana kinyume na ufahamu wa wajinga wa kale na wajinga mambo leo (wa sasa) ambao walichukia kupata watoto wasichana. Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliipandisha hadhi ya tunu hii inayotoka kwa Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala), kwa kuwakaribisha wasichana na kunyanyua umuhimu wa kuwalea kwa maneno yanayowapatia wazazi moyo mkunjufu na bashasha.

Amesema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), “Yeyote anayewaangalia vizuri wasichana wawili mpaka wafike utu uzima - yeye na mimi tutakua pamoja Siku ya kufufuliwa, Na hapo alizishikanisha vidole vyake (akimaanisha Peponi)”. 

Amesema tena, “Yeyote atakayekuwa na mabinti wa tatu au madada watatu au mabinti wawili au madada wawili, akaishi nao vizuri na kwa wema, akamuogopa Allaah kwa ajili yao - katika riwaya nyengine akawafanyia wema na akawaoza, basi Pepo ni yake”. 

Amesema tena (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Yeyote atakaye walea watoto wa kike watatu, akawafundisha tabia njema na maadili mazuri, akawaoza na kuwafanyia wema, Pepo ni yake”. Katika Hadithi nyengine inasema: “Wao (wasichana) watakuwa ngao kwake na Moto”.

Hii ihsani (wema) ambayo imetajwa katika Hadithi ni uzuri katika malezi na adabu na kukua. Hayapatikani hayo ila kwa elimu ambayo kwamba itahakikisha utamaduni wa kiakili na kuitohirisha nafsi.

3 ATHARI YA KUMSOMESHA MWANAMKE:

Aya tuliyoitaja hapo awali ya Surah Fussillat (41: 33 inatuonyesha duru ya mwanamke katika Da‘wah kwani ‘man’ inayopatikana katika aya hiyo 

“wa man ahsanu qawlan mimman da‘aa” inachang’anya wanawake na wanaume. Na mwanamke katika kutekeleza Da‘wah ya kutengeneza jamii yoyote haikosi watu wema. Hawa wema kwa maumbile si wanaume pekee bali na wanawake wamo katika kuleta islahi. Jamii ni kama jengo sehemu moja inasaidia sehemu nyengine. Hapa tutaonyesha wajibu wa kumsomesha mwanamke. Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) Anasema, 

“Basi waandalieni nguvu mziwezao (silaha), na mafarasi yaliyofungwa tayari tayari, ili kwazo muogopeshe maadui wa Allaah na maadui zenu…” 

Nguvu hapa zinachanganya idadi na kutayarisha watu, pesa na maadili. Nguvu zote zitakazo tumika dhidi ya maadui, miongoni mwazo ni kumtayarisha mwanamke Muislamu vizuri ili atekeleze wajibu wake. Miongoni mwa nguvu ni silaha, kwani maadui wa Allaah wanawatumia wanawake katika mipango yao yote ikiwa ni kama askari au kwa njama. Kwa hivyo ni wajibu kwa Waislamu kuwaandaa wanawake matayarisho sahihi. Matayarisho hayo yalipokuwa katika njia hiyo Da‘wah yake ilikuwa ni wajibu na ya sawa na sahihi. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amewahimiza wanawake kutoa sadaka inapotokea haja hiyo. Nao walitekeleza Da‘wah kwani hizo njia mbili (sadaka na Da‘wah) zinawasaidia madhaifu na masikini na kuitangaza dini ya Uislamu.

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimtaka Ummu Sulaymaan Shafaa (Radhiya Allaahu ‘anha) amfundishe mkewe, Hafsah bint ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anha) kuandika kama alivyomtaka amfundishe Ruqyah khasa ya kutibu ugonjwa unaoitwa Daan Namlah.
 
 
 Posted By Posted juu ya Saturday, March 09 @ 16:58:32 PST na MediaSwahiliTeam
 
 
:-: Go Home :-: Go Top :-:
 
 
 
Comments & Debates :-: التعليقات والمحاورات

 
 
For Your Membership Comments And Registered Debates Please, See Below Or Register Here :-: للحصول على تعليقات عضويتك و مناقشات الأعضاء انظر من فضلك أدناه أو سجّل هنا
 
 
:-: Go Home :-: Go Top :-:
 

Kuhusiana Viungo

· zaidi Waislamu Wanawake - maisha yao na Famili
· Habari na MediaSwahiliTeam


Kweli kusoma hadithi kuhusu Waislamu Wanawake - maisha yao na Famili:
Elimu Ni Wajibu Kwa Mwanamke Wa Kiislamu - MIFANO YA WANAWAKE WATUKUFU


Kifungu Rating

Wastani matokeo: 0
Kura: 0

Tafadhali chukua ya pili na kupiga kura kwa ajili ya makala hii:

bora Vizuri Sana Mema Kawaidar Mbaya

Chaguzi


 Chapa Rafiki Chapa Rafiki


Mada zinazohusiana

Waislamu Wanawake - maisha yao na Famili

 

 
EsinIslam The Muslim World Portal For Islamics, News, Fatwas, Audios, Videos, Muslim News, Quranic Islamic Articles, Radio, Audio Quran, TV Channels, Fatwa Rulings, Muslim News Newspapers Magazines Headlines Articles Forums Schools, Universities, Colleges, Mosques, Qur'an, Hadith, Sunnah, Fiqh, Prayers, Salat, Fasting Ramadan, Vidoes, Books On EsinIslam.Com And Muxlima.Com

  :-: Go Home :-: Go Top :-: