Swahili
- Ukurasa Kuu    - Kumi Juu    - Mada Mpya    - Salimisha Habari    - Tafuta    - Kiswahili Jukwaa    - Kiswahili Wanachama    - Tathmini    - Ujumbe wa Kibinafsi    - Tafiti    - Majarida    - Hadithi Archive    - Maudhui    - Viungo vya Wavuti    - Vipakuliwa    - Maswali ya Kawaida    - Tunapendekeze    - Orodha ya Kuingia   

 

 
Elimu Ni Wajibu Kwa Mwanamke Wa Kiislamu - ELIMU ANAZOPASWA KUSOMA MWANAMKE
 
 
Waislamu Wanawake - maisha yao na Famili  Mfumo Na Muelekeo Wa Nyaraka Hizi Umechukuliwa Kutoka Kwa Kijitabu Kinachoitwa 

“Al-Mar’at Al-Muslimah Fiy Twalabil ‘Ilm”  Elimu Ni Wajibu Kwa Mwanamke Wa Kiislamu - ELIMU ANAZOPASWA KUSOMA MWANAMKE (Mwanamke Muislamu Katika Kutafuta Elimu)

Kilichochapishwa Na Daarul Arqam,  Chapa Ya Pili, ELIMU ANAZOPASWA KUSOMA MWANAMKE 1 SEHEMU YA ELIMU: Elimu katika Uislamu ina sehemu na daraja ambayo haijapatiwa na dini nyengine yeyote. Hii tunaiona wazi katika aya tukufu inayosema, “Soma kwa jina la Mola wako Aliyeumba”. Kama alivyosema tena Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala),  “Sema: ‘Je, wanaweza kuwa sawa wale wanaojua na wale wasiojua?” Dini ambayo maagizo yake ya kwanza ni kusoma na elimu ni dini ambayo inataka wafuasi wake wawe msitari wa mbele katika kusambaza elimu. Huu kwa hakika ni mfumo wa Mola, Ambaye ameifanya elimu kuwa faradhi (lazima) kama ilivyokuja katika Hadithi. Imepokewa na Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema, “Kutafuta elimu ni faradhi kwa kila Muislamu”. Lafdhi ya Muslim (Muislamu) ina makusudio ya wanaume na wanawake kwani imewachang’anya wote bila kubagua.

2 FADHILA ZA ELIMU:

Uislamu unahimiza elimu na kubainisha ajra kubwa na thawabu kwa mwenye kuitafuta au kusimama katika kuifikisha. Hivi ndivyo alivyofahamu Abu Dardaa (Radhiya Allaahu ‘anhu) aliposema, “Mwalimu msomi na mwenye kusoma (mwanafunzi) ni sawa katika ajra na wala hakuna kheri kwa watu wote baada yao”. Bila shaka hakuna kheri kwa mujibu wa maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwani imepokewa na Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba amesema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), “Dunia yote imelaaniwa na zimelaaniwa zilizoko ndani yake ila kumtaja Allaah Aliyetukuka na Twaa ya Allaah au msomi au mwenye kusoma”.

Qur’ani imetilia mkazo sana elimu na imetumia maneno mengi yenye kuhimiza shughuli hiyo. Kwa mfano ‘Ilm (yenye maana ya sayansi, elimu na kujifundisha) imetajwa mara 80 na maneno yanayotokana na neon hilo zaidi ya mara mia tatu. Al-Albaab (ufahamu) mara 16, an-Nuha (ufahamu) mara mbili, ‘Aql (akili, ubongo na hisia) mara 49, Fikr (fikiri na tafakari) mara 18, Fiqh (fikihi, ufahamu, elimu) mara 21 na Hikmah (hekima na uoni) mara 20.

Wahyi wa kwanza alioteremshiwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ilikuwa ni kumuhimiza kusoma japokuwa alikuwa ni Ummy katika pango la Hira. Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) Anasema,

“Soma kwa jina la Mola wako Aliyeumba. Amemuumba mwanadamu kwa pande la damu. Soma, na Mola wako ni Karimu sana. Ambaye Amemfundisha (binadamu) kwa wasita (msaada) wa kalamu. Amemfundisha mwanadamu (chungu ya) mambo aliyokuwa hayajui”

Sayyid Qutb anatueleza kuwa katika wahyi huu wa mwanzo tunapata mafundisho yafuatayo: “Allaah ndiye chimbuko la elimu na neema nyingi. Alalah (Subhaanahu Wa Ta’ala) Amemtukuza mwanadamu kwa kumteremshia wahyi. Hii inatupatia umuhimu kwani elimu imefaradhishwa kabla ya Swalah, Zakah, Swaum, Hajj na Jihaad. Nne, ni kuwa Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) hakuweka mgawanyo wa elimu - ya dini na dunia. ya mwisho ni kuwa unachosoma chochote usome kwa ikhlasi na kutaka radhi za Allaah”.

Katika aya ya kwanza na ya tatu Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) Ametumia neno la Iqraa kwa tensi ya lazima. Kwa hivyo shughuli hiyo ya kusoma ni faradhi kwa wanaume na wanawake. Umuhimu wa jambo hilo la ziada ni kuwa katika hizo aya tano za mwanzo Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) ametumia maneno sita kati ya ishirini kuhimiza na kutilia mkazo elimu (yaani 30%).

Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) Anasema tena, 

“Na wale waliozama katika elimu husema: ‘Tumeziamini, zote zimetoka kwa Mola wetu’. Na hawakumbuki isipokuwa wenye akili”.
Anasema tena (Subhaanahu Wa Ta’ala),

“Allaah Atawainua wale walioamini miongoni mwenu. Na waliopewa elimu watapata daraja zaidi”.

Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) Ametufundisha Du’aa ambayo inatakikana tuiombe kila wakati, “Rabbi zidni ‘ilman - Na (uombe) useme: ‘Mola wangu, nizidishe elimu”.

Ni lazima tufahamu kuwa elimu kwa Muislamu haijagawanywa, ya dini na ya dunia. Bali Uislamu unawahimiza wanawake washindane na wanaume katika kutafuta elimu kwa sababu elimu ni jambo jema na zuri. Kwa hivyo, kushindana na mwenzako katika hasanati (mambo mema) ndio lengo na mulekeo wa shari‘ah ya Kiisalamu. Tunapotafuta elimu ni lazima tuzingatie maneno ya Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala), 

“Kwa hakika wanaomuogopa Allaah ni miongoni mwa waja Wake ni wale wataalamu (wanavyuoni)”. 

Ubora wa elimu ya Misingi sio tu inamleta msomi karibu na ukweli, bali humyanyua hadhi yake katika jamii ya Kiislamu na utamaduni wake. Pia tizama aya ya 9 ya sura ya 39 tuliyoitaja kabla.

Kuna Haduthi nyingi zinazotilia mkazo suala la elimu. Elimu ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliipata kupitia kwa wahyi. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikihuzunika sana wahyi ulipokuwa unasangaa na alikuwa na pupa ya kutaka kuhifadhi maneno ya Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) pindi Jibriyl ('Alayhis Salaam) anapomaliza kisomo. Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) Anatuelezea, 

“Usiutikise ulimi wako kwa (kuufanyia haraka wahyi) Kwa hakika ni juu yetu kuukusanya na kuusomesha. Wakati Tunapokusomea, basi fuata kusomwa kwake. Kisha ni juu yetu kukubainishia”.

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwahimiza watu kusoma kwa dhati, kwa maneno na kuonyesha mfano.

Imepokewa na Ibn Mas‘ud (Radhiya Allaahu ‘anhu) kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema, “Hakuna hasadi ila kwa mambo mawili: Mtu aliyepatiwa mali na Allaah na akayatumia katika haki na mtu aliyepatiwa na Allaah hekima naye akaitumia na kuifundisha”.

Imepokewa na Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema, “Mwenye kufuata njia ya kutafuta elimu, Allaah atamsahilishia njia ya Peponi”. Amesema tena (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema, “Yeyote anayeita katika njia ya uongofu atakuwa na ujira mfano wa wale wenye kufuata bila kupunguzwa kitu chochote katika ujira wao”. Amesema tena (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Pindi anapofariki mwanadamu amali yake yote hukatika isipokuwa mambo matatu: sadaka yenye kuendelea, au elimu yenye manufaa au mtoto mwema atakaye kuombea”.

Imepokewa na Anas (Radhiya Allaahu ‘anhu) kuwa, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Yeyote anayetoka kwa ajili ya kutafuta elimu, yupo katika njia ya Allaah mpaka atakapo rudi”. 

Imepokewa na Abi Umamah (Radhiya Allaahu ‘anhu) kuwa, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Fadhila za mwanachuoni juuu ya mwenye kuabudu ni kama ubora yangu juu ya aliye chini miongoni mwenu”. Kisha akasema: “Kwa hakika Allaah, Malaikah zake na viumbe vya mbinguni na ardhini hata chungu katika shimo lake na nyanguni humsalia mwenye kufundisha watu kheri”. 

Imepokewa na Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) kuwa, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Yeyote anayeulizwa kuhusu elimu na akaficha, atazuiliwa Siku ya Kiyama ndani ya Moto”.

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akimuomba Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) amlinde kutokana na elimu isiyo na manufaa. Imepokewa na Zayd bin al-Arqam (Radhiya Allaahu ‘anhu) kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Ee, Mola wangu! Najilinda Kwako kutokana na elimu isiyo na manufaa, na moyo usio ogopa na nafsi isiyo shiba na du‘aa isiyo jibiwa”.

Qatadah alisema Ibn Shahir amesema: “Fadhila ya elimu ni bora kuliko fadhila ya ibadah (Sunnah katika ibadah) na ubora wa dini yenu ni kumwogopa Allaah”. Maneno haya hakuyazua bali yametoka kwa maswahaba (Radhiya Allaahu ‘anhum). Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) alisema: “Kukaa kwangu saa moja ili kupata ufahamu wa dini ni bora kwangu kuliko kukesha usiku mzima katika ibadah”. Yote haya ni kuwa amali bila ya elimu inaharibika. Haya aliyaweka wazi ‘Umar bin ‘Abdul-‘Aziz aliposema: “Yeyote atakaye tenda pasi na elimu anakuwa ni mwenye kuharibu zaidi kuliko kutengeneza”.

Neema ya elimu ni tunu na zawadi kutoka kwa Allaah aliyetukuka. Kwa kupita wakati inaonekana kuwa mwanadamu amesahau na Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) Anamkumbusha: 

“Amemuumba binadamu. Akamfundisha kunena”.

Baada ya kuumbwa kwake tunamuona mwanadamu anazungumza, anaweka mambo wazi, anafahamiana na kujibiana na wengine. Haya yote ni utukufu ambao binadamu ameusahau kwa kupitiwa na karne nyingi na Qur-aan ikaturudisha ili kutuamsha katika maudhui kadhaa”.

Elimu ni fadhila kutoka kwa Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) aliyowapatia waja wake. Hapa haifai kukataa mmoja wetu kufadhilisha watu wema waliotangulia elimu juu ya amali za Sunnah. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika hadithi tuliyo itaja mbeleni kuwa: “Fadhila za mwanachuoni juu ya mwenye kuabudu ni kama ubora wangu juu ya aliye chini miongoni mwenu”. Angalia jinsi alivyolinganisha elimu na Utume na vipi alivyoiweka chini daraja ya bila matendo. Hata hivyo mwenye kuabudu anaabudu kila wakati na hangefanya hiyo ibadah kama hangekuwa na elimu. Wasomi wanastahiki daraja hii. Ni rehema kwa Ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuliko baba na mama zao. Ikasemwa vipi? Akasema kuwa baba na mama zao wanawahifadhi na moto wa dunia na wao wanawahifadhi na moto wa Akhera.

Ali bin Abi Talib (Radhiya Allaahu ‘anhu) alimpatia wasia Kumayl bin ziyad akimwambia: “Ewe Kumayl! Hii mioyo inahifadhi basi bora kati yao ni yenye elimu. Hifadhi kutoka kwangu ninayo kwambia: Watu ni aina tatu, Msomi kwa ajili ya Mola wake, mwanafunzi katika njia ya kufaulu na wasio na elimu wenye kufuata mkumbo wa mwenye kuwika. Ewe Kumayl elimu ni bora kuliko mali. Elimu inakulinda lakini wewe unailinda mali. Elimu inatoa uadilifu lakini mali inahitaji uadilifu. Mali yanapungua unapoyatumia lakini elimu inaongezeka. Maarifa ya elimu ni dini inayotegemewa na kwayo anapata mwanadamu twaa katika uhai wake na matokeo mazuri baada ya kufa kwake. Elimu ni hakimu na mali ni yenye kuhukumiwa”. ‘Ali alitoa mashairi kuonyesha ubora wa elimu na wasomi aliposema:

Fakhari ya wasomi pekee Wameongoka na ni dalilikwa wanaotaka uongofu.

Kila mmoja anatukuzwa kwa kadiri ya elimu Lakini wajinga kwa wasomi ni maadui.

Tafuta elimu nawe utaishi milele Watu wote wamekufa isipokuwa wanavyuoni.
 
 
 Posted By Posted juu ya Saturday, March 09 @ 16:54:32 PST na MediaSwahiliTeam
 
 
:-: Go Home :-: Go Top :-:
 
 
 
Comments & Debates :-: التعليقات والمحاورات

 
 
For Your Membership Comments And Registered Debates Please, See Below Or Register Here :-: للحصول على تعليقات عضويتك و مناقشات الأعضاء انظر من فضلك أدناه أو سجّل هنا
 
 
:-: Go Home :-: Go Top :-:
 

Kuhusiana Viungo

· zaidi Waislamu Wanawake - maisha yao na Famili
· Habari na MediaSwahiliTeam


Kweli kusoma hadithi kuhusu Waislamu Wanawake - maisha yao na Famili:
Elimu Ni Wajibu Kwa Mwanamke Wa Kiislamu - MIFANO YA WANAWAKE WATUKUFU


Kifungu Rating

Wastani matokeo: 0
Kura: 0

Tafadhali chukua ya pili na kupiga kura kwa ajili ya makala hii:

bora Vizuri Sana Mema Kawaidar Mbaya

Chaguzi


 Chapa Rafiki Chapa Rafiki


Mada zinazohusiana

Waislamu Wanawake - maisha yao na Famili

 

 
EsinIslam The Muslim World Portal For Islamics, News, Fatwas, Audios, Videos, Muslim News, Quranic Islamic Articles, Radio, Audio Quran, TV Channels, Fatwa Rulings, Muslim News Newspapers Magazines Headlines Articles Forums Schools, Universities, Colleges, Mosques, Qur'an, Hadith, Sunnah, Fiqh, Prayers, Salat, Fasting Ramadan, Vidoes, Books On EsinIslam.Com And Muxlima.Com

  :-: Go Home :-: Go Top :-: