Swahili
- Ukurasa Kuu    - Kumi Juu    - Mada Mpya    - Salimisha Habari    - Tafuta    - Kiswahili Jukwaa    - Kiswahili Wanachama    - Tathmini    - Ujumbe wa Kibinafsi    - Tafiti    - Majarida    - Hadithi Archive    - Maudhui    - Viungo vya Wavuti    - Vipakuliwa    - Maswali ya Kawaida    - Tunapendekeze    - Orodha ya Kuingia   

 

 
Elimu Ni Wajibu Kwa Mwanamke Wa Kiislamu - UTANGULIZI
 
 
Waislamu Wanawake - maisha yao na Famili  Mfumo Na Muelekeo Wa Nyaraka Hizi Umechukuliwa Kutoka Kwa Kijitabu Kinachoitwa

Elimu Ni Wajibu Kwa Mwanamke Wa Kiislamu - UTANGULIZI

“Al-Mar’at Al-Muslimah Fiy Twalabil ‘Ilm”  (Mwanamke Muislamu Katika Kutafuta Elimu)

Kilichochapishwa Na Daarul Arqam, Chapa Ya Pili,

1.0 UTANGULIZI 

 Sifa zote njema anastahiki Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala), ambaye Ameumba wanadamu, Akawaongoza na Kuwafundisha kwa kutumia kalamu. Akawaongoza pia kwa yale wasio yajua. Swalah na salamu zimshukie yule Aliyetumwa kuwa rehema kwa walimwengu Nabii wetu Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na juu ya ahli zake na swahaba zake na waliomfuata miongoni mwa watu.


Hakika Ummah wa Kiislamu leo unahitaji waliotakasa amali na nyoyo zao kwa kutengeneza yaliyo haribiwa na kurudisha safu pamoja. Hilo halipatikani kwa kuandika vitabu vingi, lakini kwa juhudi, amali na matendo. Bila shaka! Uchapishaji wa vitabu umekithiri na makabati yamejaa kwa mijalada, umekuja wakati ambao tunatamani kuona matendo yenye kuzaa matunda kwa kizazi kitakacho jenga utukufu wa mababu zetu. Hili litapatikana kwa kuchapisha vitabu vya msingi katika elimu ya ufasiri ili kunyanyua bendera ya Uislamu na kutekeleza amana ambayo ametukalifisha Mola Mwenye nguvu na Utukufu pale Aliposema,  “Kisha Tukakufanyeni nyinyi ndio wenye kushika mahala pao baada ya (kuangamizwa) hao katika ardhi ili Tuone jinsi mutakavyotenda”. 

Huku kupatiwa Ukhalifa (uongozi) ni kwa Waislamu sio wengineo, kwani viongozi wa upotevu miongoni mwa makafiri na mushrikina wataupeleka ulimwengu kuvunjika na kuharibika, haya tunayaona leo. Mpaka wajue Waislamu wajibu wao na kuwa ni wenye kuchukua madaraka hawana budi kuwa na elimu na muamko, waondoshe ujinga na kutowachukulia wasiokuwa wao. Kwa hakika elimu aliyotunukia Muumba wetu Aliyetukuka inatutajirisha kuliko yale yaliyoko katika mikono mwa maadui zetu kwa kanuni na hukumu. Bali ni nuru ambayo kwamba huyafunua yaliyo chini yake katika elimu. Nao ni msingi ambao kwamba ni lazima tujenge juu yake ustaarabu wa mataifa kwani Uislamu ni dini ya ulimwengu. Ni juu ya Waislamu kufanya kazi ili kurudi katika uongozi wa mataifa na kutumia njia zifaazo katika kurudi kwao. Ummah ni mkusanyiko wa familia, nguzo yake ni vijana na wasichana, kina baba na kina mama, watoto kwa wazee na wanaume kwa wanawake. Na juu yao ni wajibu kuamka na kujizatiti katika huo Ummah ili yasiachwe hayo kwa wanaume peke yao. 

Uislamu umekuja kubainisha hayo katika aya zilizo wazi na Hadithi swahihi. Katika nyaraka hizi hataki kutoa bayana kuhusu haki za mwanamke katika Uislamu kwani huo ni mlango mwengine. Lakini hapa hatuna budi kuonyesha umuhimu wa majukumu ya mwanamke ubavuni mwa mwanamume katika kujenga Ummah na kujizatiti kwayo. Tunaona Qur-aan Tukufu inamkirimu mwanamume na mwanamke sawa sawa, kwa maneno ya Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala), “Na hakika Tumewatukuza wanadamu na Tumewapa vya kupanda barini na baharini, na Tumewaruzuku vitu vizuri vizuri, na Tumewatukuza kuliko wengi katika wale Tuliowaumba, kwa utukufu ulio mkubwa (kabisa)”. 

 Haya yanachanganya waume na wake barabara na bila ubaguzi wowote. Kama vile jazaa na thawabu kwa amali ni sawa baina ya mwanamume na mwanamke. Hii ni kwa sababu ya kuwa ‘Ibadah zote zinatakikana zifanywe bila ubaguzi wa kijinsia. Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) amesema, “Mola wao Akawakubalia (maombi yao kwa kusema): ‘Hakika Mimi sitapoteza juhudi (amali) ya mfanya juhudi miongoni mwenu, akiwa mwanamume au mwanamke; kwani nyinyi ni nyinyi kwa nyinyi”.  Pia, “Na watakaofanya vitendo vizuri, wakiwa wanaume au wanawake, hali wao ni wenye kuamini, basi hao wataingia Peponi wala hawatadhulumiwa hata tundu ya kokwa ya tende”.  Pia, “Wafanyaji mema, wanaume au wanawake, Tutawahuisha Maisha mema, na Tutawapa ujira wao (Akhera) mkubwa kabisa kwa sababu ya yale mema waliokuwa wakiyatenda”. Majukumu ni ya wote katika kila jambo wala sivyo kama wanavyodai Mayahudi na Manasara katika Vitabu vyao vilivyobadilishwa kuwa mwanamke ndio sababu ya kutolewa kwa baba yetu Nabii Aadam ('Alayhis Salaam) Peponi na yeye ni mchafu. Bali Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) Anasema,  “Lakini shaytwaan aliwatelezesha wote wawili (wakakhalifu amri ile, wakala katika mti huo waliokatazwa) na akawatoa katika ile hali ya waliokuya nayo. Tukawaambia: ‘Nendeni, hali ya kuwa maadui nyinyi kwa nyinyi”.  

 Bali katika aya nyengine, Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) anamfanya mwanamume, Nabii Adam ('Alayhis Salaam) kuwa ndiye mkosa. Amesema (Subhaanahu Wa Ta’ala),  “Basi wakaula wote wawili, na uchi wao ukawadhihirikia na wakaanza kujibadika majani ya Peponi. Na Aadam akamkosea Mola wake na akapotea kidogo njia. Kisha Mola Wake Akamchagua na akamkubalia toba yake na Akamuongoa”. Lakini kitu muhimu ni kuwa baada ya kukosa, walitubia na Mola wao akawasamehe. Imepokewa na ‘Aishah (Radhiya Allaahu ‘anha) kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema, “Kwa hakika wanawake ni ndugu za wanaume”. Mwanamke ana jukumu la kutengeneza uchumi kwa kufanya kazi au biashara. Kwa Uislamu ulimpatia haki ya kumiliki mali, haki ambayo haibadiliki hata anapoolewa. Haki hii anaipata kupitia kwa kurithi, zawadi kutoka kwa wazazi, mume, watoto, jamaa zake wengine, kufanya kazi au biashara. Kitu kinajulikana kabisa katika Shari‘ah. Kuhusu haki zao za kurithi, Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) Anasema,  

 “Wanaume wana sehemu katika mali wanayoyaacha wazazi na jamaa wakaribu. Na wanawake pia wanayo sehemu katika yale wanayoyaacha wazazi na jamaa wakaribu. Yakiwa kidogo au mengi. Hii ni sehemu zilizofaridhiwa (na Allaah)”. Hata baada ya kuolewa, anachopata mke kwa kufanya kazi au njia nyengine ya halali ni chake na hawezi kupokonywa kwa njia yeyote ile. Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) Anasema, “Wanaume wanayo sehemu (kamili) ya vile walivyovichuma na wanawake nao wanayo sehemu (kamili) ya vile walivyovichuma”.

Khalifa wa pili muongofu, ‘Umar bin al-Khattab (Radhiya Allaahu ‘anhu) alimuachia idara ya kuangalia masoko Shaf‘aa bint ‘AbdAllaah bin ‘Abd Shams (Radhiya Allaahu ‘anhu). ‘Umar alikuwa akitaka ushauri wake, akimheshimu na kumueka katika daraja na cheo cha juu. Zaynab ath-Thaqafiyyah (Radhiya Allaahu ‘anha) mke wa ‘AbdAllaah bin Mas‘ud (Radhiya Allaahu ‘anhu) alimuuliza Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kupitia kwa Bilaal (Radhiya Allaahu ‘anhu) kama inafaa kuwapatia sadaka na Zakah waume zao. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema, “Watapata ujira (thawabu) mara mbili, moja ya kuunga kizazi na ya pili ni sadaka”. Katika zama zetu hizi, mbali na tuhma zote walizokuwa wakirushiwa serikali ya Taliban huko Afghanistan, bado wanawake walikuwa wakifanya kazi. Sayyid Rahmatullah Hashemi, katika hotuba yake kama Balozi wa Mambo ya nje, mnamo tarehe 10 Machi 2001 katika Chuo Kikuu cha Southern California, Los Angeles huko Marekani alisema, “Wanawake wanafanya kazi katika Wizara za Elimu, Afya, Mambo ya ndani, Mambo ya jamii, n.k.” Wanawake wanacheza duru muhimu sana katika kuboresha maadili na malezi bora ya watoto. Ndipo mshairi mmoja wa Kiarabu aliposema, “Mama ni madrasa, ukimuandaa vyema basi umeandaa jamii mzima”. Jukumu la Jihadi katika aina zake zote, wanawake hawakuachwa nyuma kabisa. Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) Anasema, “Allaah Amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali yao (watoe nafsi na mali yao katika kupigania dini) ili na Yeye awape Pepo. Wanapigana katika njia ya Allaah; wanaua na wanauawa”.  

 Historia ya Uislamu ina mifano mingi ya ushujaa wa wanawake ambao walicheza duru muhimu katika vita. Kawaida wao walibaki nyuma ya safu za mapambano kwa kuwatibu na kuwatizama majeruhi, kuwaangalia farasi, kuwatia moyo na hima Waumini wa kiume na mujahidina, kuchukua silaha za makafiri waliokufa, kuwalinda mateka, kupika chakula na kupigana hasa inapo bidi.  ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha) alichukua kiriba cha maji kuwanywesha majeruhi. 

Alisaidiwa katika kazi hiyo na Ummu Sulaym (Rumaysaa bint Milhaan) na Ummu Salit (Radhiya Allaahu ‘anha). Ummu ‘Ammarah Nusaybah bint Ka‘b (Radhiya Allaahu ‘anha) alimlinda Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) vilivyo katika Vita vya Uhud. Alipigana katika vita vya Yamamah na kupata majeraha kumi na mbili. Mwana-historia Waqidi alisema kuwa wanawake walikuwa nguzo muhimu katika kutekwa nchi za Shaam, hasa Ummu Hakim, Hind Asmaa, Ummu Katheer, Ummu Abban, Ummu ‘Ammarah, Khawlah, Lubna na Afira. Katika karne ya ishirini, wanawake wamekuwa msitari wa mbele kwa kupinga serikali za kidhalimu. Wengi wao walifungwa na kuadhibiwa vikali kwa mfano Zaynab al-Ghazali, Hamida Qutb, Aminah Qutb, n.k. wakati wa Gamal ‘Abdun-Naasir. Leo Palestina, wanawake wanacheza duru muhimu na ya msingi katika kupinga udhalimu wa Israili. Mfano mzuri ni wa Ummu Muhammad ambaye watoto wake watatu wa kiume walifungwa katika magereza tofauti na serikali haramu ya Israili na wengine wawili kupelekwa Marj al-Zuhuur nje ya Palestina mwaka 1992 - 3. Yeye mwenyewe aliumizwa kichwani na afisa wa polisi wa Israili mwaka 1981 walipotaka kumshika mtoto wake Muhammad. Mama huyu alisema, 

“Natamani matumbo yangu yazae watoto ambao wataendelea na jihadi”. Jukumu jengine ni siasa na kutoa maoni. Kiini cha siasa ni mambo ya watu katika jamii na mambo kwa ujumla wake yanayo husu jamii. Pia ni serikali na idara. Maumbile ya muundo wa Uislamu katika jamii ni muhimu na inawavuta watu wake kujihusisha katika elimu ya kisiasa na kutoa maoni. Shura (kushauriana), Istihsan (ubora/ kipao mbele) na Ijma‘ (kukubaliana) ni mabo ambayo yanawafanya watu kutoa maoni katika mambo yote ya upangaji na masuala muhimu na nyeti. Waislamu, wanaume na wanawake ni lazima washirikiane kutoa maoni katika mambo ya kuamrisha mema na kukataza mabaya. Kuhusu shura, Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) Anasema, “… na ushauriane nao katika mambo”. Na pia, “Na wale waliomuitikia Mola wao na wakasimamisha Swalah na wanashauriana katika mambo yao…”  kushiriki huku si kwa wanaume pekee. Baada ya sulhu ya Hudaybiyah, Waislamu waliona kuwa masharti ya mkataba huo yanawabana wao sana. Walikasirika sana, hata baada ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwaamuru wachinje wanyama na wanyoe nywele na kukariri hayo mara tatu hakuna hata mmoja aliyeinuka kutekeleza wakifikiriya kuwa masharti hayo huenda yakafutwa. 

 Walipomuona yeye (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametekeleza hayo baada ya kufuata ushauri wa mkewe Umm Salamah Hind binti Abi Umayyah Hudhayfah al-Makhzumy (Radhiya Allaahu ‘anha) wote waliinuka kutekeleza maagizo hayo. Mfano mwengine ni uchaguzi wa Khalifah wa tatu, ‘Uthman bin ‘Affan (Radhiya Allaahu ‘anhu), kamati ya watu sita iliyochaguliwa na Khalifah wa pili, ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) ilichukua maoni kutoka kwa wanaume na wanawake kuhusu wanayemtaka awe khalifah. Wanawake wa Uswizi walipata haki hii miaka ya 1950. Jukumu jengine muhimu na kubwa ni kutafuta elimu, nalo ndio maudhui ya nyaraka hizi. Haya ni baadhi ya majukumu ya wanawake ambayo yanaonyesha umuhimu wake. 

Huenda haya yakachosha masikio kwa kuwa maudhui ya wanawake na pande zake zote yamechukua nafasi kubwa. Lakini hakika ya maneno juu ya wajibu wa mwanawake kuelekeza kwa nafsi yake, dini yake na jamii yake inatufanya tuyakumbuke kwa kuyarudia kwa ukumbusho unawafaa Waumini. Kisha pia tunasikia makelele yakiita katika kumwacha huru, kumsomesha na kutaka usawa na mwanamume bado yana wafuasi. Inatakikana sisi tupumue kidogo na kutizama: Je, yuko wapi mwanamke wa Kiislamu leo? Vipi tutayafahamu kila yaliyopitika ubavuni mwake? Je, wajibu wake ni upi na yale makelele ya nguvu na mikusanyiko ya wanawake yanayoita katika kumtumikia mwanamke na jamii kwa elimu na amali ya kuieneza elimu?
 
 
 Posted By Posted juu ya Saturday, March 09 @ 16:38:20 PST na MediaSwahiliTeam
 
 
:-: Go Home :-: Go Top :-:
 
 
 
Comments & Debates :-: التعليقات والمحاورات

 
 
For Your Membership Comments And Registered Debates Please, See Below Or Register Here :-: للحصول على تعليقات عضويتك و مناقشات الأعضاء انظر من فضلك أدناه أو سجّل هنا
 
 
:-: Go Home :-: Go Top :-:
 

Kuhusiana Viungo

· zaidi Waislamu Wanawake - maisha yao na Famili
· Habari na MediaSwahiliTeam


Kweli kusoma hadithi kuhusu Waislamu Wanawake - maisha yao na Famili:
Elimu Ni Wajibu Kwa Mwanamke Wa Kiislamu - MIFANO YA WANAWAKE WATUKUFU


Kifungu Rating

Wastani matokeo: 0
Kura: 0

Tafadhali chukua ya pili na kupiga kura kwa ajili ya makala hii:

bora Vizuri Sana Mema Kawaidar Mbaya

Chaguzi


 Chapa Rafiki Chapa Rafiki


Mada zinazohusiana

Waislamu Wanawake - maisha yao na Famili

 

 
EsinIslam The Muslim World Portal For Islamics, News, Fatwas, Audios, Videos, Muslim News, Quranic Islamic Articles, Radio, Audio Quran, TV Channels, Fatwa Rulings, Muslim News Newspapers Magazines Headlines Articles Forums Schools, Universities, Colleges, Mosques, Qur'an, Hadith, Sunnah, Fiqh, Prayers, Salat, Fasting Ramadan, Vidoes, Books On EsinIslam.Com And Muxlima.Com

  :-: Go Home :-: Go Top :-: