Swahili
- Ukurasa Kuu    - Kumi Juu    - Mada Mpya    - Salimisha Habari    - Tafuta    - Kiswahili Jukwaa    - Kiswahili Wanachama    - Tathmini    - Ujumbe wa Kibinafsi    - Tafiti    - Majarida    - Hadithi Archive    - Maudhui    - Viungo vya Wavuti    - Vipakuliwa    - Maswali ya Kawaida    - Tunapendekeze    - Orodha ya Kuingia   

 

 
Vazi Lipi Lililo Bora Mbele Ya Allaah?
 
 
Habari Idadi ya habari na hadithi Makala Bint Ahmadah

Amri kuu aliyopatiwa mwanamke wa Kiislamu inayomtofautisha na ndugu yake wa kiume ni ile inayosema: "Ee Mtume! Waambie wake zako, na binti zako, na wanawake wa Kiislamu wajiteremshie uzuri nguo zao. Kufanya hivyo kutapelekea upesi wajulikane wasiudhiwe." (Suratul-Ahzaab: 59)

Vipi kuvaa nguo leo hii imekuwa viroja kwa Waislam? Kwani wamesahau mavazi yao, leo imekuwa watafuta kila mavazi kisha tunasema yetu, kisa tumejisahau lipi lililotulazimu kwetu na lililo muhimu kwetu na kwa Mola wetu?

Kwani kuiga mavazi yaliyokuwa si yetu Waislam hayajatuhusu kabisa. Lakini kwa mtizamo wa leo ndio tunakwenda na wakati. Ati kuvaa nguo kwenye magoti ndio kustaarabika kwa ulimwengu wa leo, kumbe kinyume chake ni kupotoka kimaadili. Ustaarabu wa kweli tunaotakiwa kujinasibisha nao ni ule uliokuwepo zama za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Maswahaabah (Radhiya Allaahu ‘Anhum).

Wanawake katika zama hizo walikuwa ni wastaarabu wa maneno, vitendo na hata mavazi. Kwani akisimuliwa Bibi Faatwimah binti Rasuuli-Llaah vipi alivyokuwa mstaarabu si kwa watu wake tu, bali hata kwa ndugu zake wa kike pia anawagusa. Alijichunga ulimi wake, mwili wake, mpaka vitendo vyake hadi akawa mmoja kati ya wanawake bora duniani.

Pia tukitizama maana ya ustaarabu ni kuelimika kutokana na kitu fulani. Je wewe mwenzangu kuvaa mavazi yasiyostahiki mbele za watu ndio kustaarabika wakati dini yetu ya Kiislam imekwisha weka mavazi yanayotakiwa yavaliwe kwa mwanamke wa Kiislam. Elimu ya Qur-aan ndio ustaarabu wetu na tunalazimika kuitekeleza. Sio kuvaa kimini wala kijinzi. Je ikiwa wewe ni mama unavaa mavazi hayo mtoto naye avae vipi? Japo kuna baadhi yao huona fakhari kumuona mtoto wao amevaa jinzi na kitopu mbele ya watu. Na huwaonyesha marafiki zake kwa ufakhari.

Aya za Mungu tunazigeuza tunavyotaka sisi kwa kujitupia kitandio kichwani ukiambiwa useme si ushajisitiri. Kuna wengine wakiwa hawana vyeo huvaa vizuri tu, wakipata vyeo ndio huvua hijabu mpaka inafika wakati hata ule wa kujitupia haukai kichwani. Kwa hiyo Mungu ulimjua ulipokuwa na dhiki, wakati wa raha Hajulikani. Umesahau kwa kupata 'chako' kwenye dunia hii 'nzuri' iliyojaa starehe hatimaye ukamsahau Mungu. Je huu ndio uungwana tuliofunzwa na Uislamu? Tunashindwa na paka au mbwa anayefugwa na mwanaadamu. Paka au mbwa aliyefunzwa na akafunzika wanapoamrishwa na bwana wake hakaidi. Hata kama paka akifunzwa kukataa kula samaki asiyepikwa hatakula na atakula aliyepikwa tu.

Lakini wewe dada yangu unasahau kwamba kuna mafunzo maalum ya Qur-aan uliyopatiwa kuyafuata na kwamba hapa ulimwenguni umeletwa kwa lengo la kumuabudu Allaah tu. Lakini leo wasema unakwenda na wakati. Ole wako kwa kuifanya dunia ni yako kama alivyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) katika Qur-aan tukufu:

"Wala usifuate (ukipita ukiyasema au kuyafanya) usiyo na ilimu (ujuzi) nayo. Hakika masikio na macho na moyo; hivyo vyote vitaulizwa." (Suraatul-Israa: 36)

Ni juu yetu kina dada wenzangu kujikamata vilivyo kwenye mafunzo sahihi ya Uislam wetu. Tusione hayyaa kumrekebisha dada mwenzetu anayeporomoka kimaadili. Msimamo unahitajika kwenye kivazi hasa kwa wale wanawake wanaofanya kazi. Kibarua kisiwe ndio sababu ya kumuasi Mola Mlezi. Vazi la Uislam kwa mwanamke ndio heshima yake na yetu sote kwa ujumla. Shime tukamatane masikio dada zangu!
 
 
 Posted By Posted juu ya Wednesday, December 19 @ 12:54:26 PST na MediaSwahiliTeam
 
 
:-: Go Home :-: Go Top :-:
 
 
 
Comments & Debates :-: التعليقات والمحاورات

 
 
For Your Membership Comments And Registered Debates Please, See Below Or Register Here :-: للحصول على تعليقات عضويتك و مناقشات الأعضاء انظر من فضلك أدناه أو سجّل هنا
 
 
:-: Go Home :-: Go Top :-:
 

Kuhusiana Viungo

· zaidi Habari Idadi ya habari na hadithi Makala
· Habari na MediaSwahiliTeam


Kweli kusoma hadithi kuhusu Habari Idadi ya habari na hadithi Makala:
Vidokezo Muhimu Kwa Wazazi Wenye Wasichana Na Wavulana


Kifungu Rating

Wastani matokeo: 0
Kura: 0

Tafadhali chukua ya pili na kupiga kura kwa ajili ya makala hii:

bora Vizuri Sana Mema Kawaidar Mbaya

Chaguzi


 Chapa Rafiki Chapa Rafiki


Mada zinazohusiana

Habari Idadi ya habari na hadithi Makala

 

 
EsinIslam The Muslim World Portal For Islamics, News, Fatwas, Audios, Videos, Muslim News, Quranic Islamic Articles, Radio, Audio Quran, TV Channels, Fatwa Rulings, Muslim News Newspapers Magazines Headlines Articles Forums Schools, Universities, Colleges, Mosques, Qur'an, Hadith, Sunnah, Fiqh, Prayers, Salat, Fasting Ramadan, Vidoes, Books On EsinIslam.Com And Muxlima.Com

  :-: Go Home :-: Go Top :-: