Swahili
- Ukurasa Kuu    - Kumi Juu    - Mada Mpya    - Salimisha Habari    - Tafuta    - Kiswahili Jukwaa    - Kiswahili Wanachama    - Tathmini    - Ujumbe wa Kibinafsi    - Tafiti    - Majarida    - Hadithi Archive    - Maudhui    - Viungo vya Wavuti    - Vipakuliwa    - Maswali ya Kawaida    - Tunapendekeze    - Orodha ya Kuingia   

 

 
Ujumbe Kwa Mwanamke
 
 
Mkuu - teknolojia na taaluma رسالة إلى المرأة:  Ujumbe Kwa Mwanamke
'Allaamah Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri:
Abu Bakr Khatwiyb al-Atrush

Bismi Allaahi Ar-Rahmaani Ar-Rahiym. Alhamdu Allaahi Rabil 'Aalamiyn. Swalah na salaam zimwendee Mtume wetu Muhammad (swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) na ahli zake na Maswahaba wake kwa jumla (radhiya Allaahu ´anhum).
Tumesikia kwenye hizi khutbah mbili zenye baraka khayr nyingi kutoka kwa Khatwiyb wetu - Allaah Ampe mafanikio. Kazungumzia masuala ya khatari, nayo ni masuala ya mwanamke.
Mwanamke enyi ndugu! Allaah Kamuumba kwa lengo kubwa katika maisha haya, kama Alivyomuumba mwanaume. Na kila mmoja ana umuhimu [kazi] Yake. Mwanaume ana kazi yake na mwanamke ana kazi yake. Kila mmoja akishikamana na kazi yake na kuitimiza, jamii itafikia khayr kubwa. Na ikiwa nidhamu itayumbishwa, ndiyo kunatokea kasoro nyingi. Kama mlivyosikia jukumu la mwanamke wakati wa Ujaahiliyyah (kabla ya kuja Uislamu), na jukumu lake leo kwenye miji ya kikafiri na kwa Waislamu wenye misimamo.

Mwanamke ni mtu muhimu sana na ndiyo maana Mtume (swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) katuusia kuhusu wao.
Alisema kwenye khutbah yake, Hijjatul wadaa [ya kuaga] 'Arafah:
"Ninawausia kuwatendea wanawake khayr [wema]. Kwani wao ni wafungwa wenu." (Ibn Maajah (1851))
Mtume (swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) katuusia kuwatunza wanawake, kutokana na umuhimu wa mwanamke katika jamii. Si kuwatunza tu, na kuwapa haki zao tu. Hili ni wajibu, lakini zaidi na muhimu ni kumlinda na uchafu - kwa kuwa mwanamke ni mtu (kiumbe) dhaifu - uchafu, fitnah na kumuacha akafanya apendavyo.

Haya ndiyo yalikuwa (makusudio) muhimu aliyotuusia nayo Mtume (swalla Allaahu 'alayhi wa sallam), tuwahifadhi. Na Allaah (Jalla wa 'Aala) Anasema:
الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاء بِمَا فَضَّلَ للهُّ بَعْضَھُمْ عَلَى بَعْضٍ وَبِمَا أَنفَقُواْ مِنْ أَمْوَالِھِمْ فَالصَّالِحَاتُ قَانِتَاتٌ حَافِظَاتٌ
لِّلْغَيْبِ بِمَا حَفِظَ للهُّ

“Wanaume ni wasimamizi wa wanawake, kwa kufadhiliwa na Allaah baadhi yao juu ya baadhi, na kwa mali yao wanayo yatoa. Basi wanawake wema ni wale wenye kutii na wanaojilinda hata katika siri kwa kuwa Allaah Ameamrisha wajilinde.” (4:34)
Nini maana wanaume ni wasimamizi wa wanawake? Je, makusudio ni kuwahudumia na kuwa muadilifu kwao tu? Makusudio siyo hayo. Jukumu lake ni katika kitu ambacho ni muhimu zaidi ya hayo. Amlinde huyu mwanamke ili asije kupotea, akajiachia huru na kuchukulia sahali mambo ya haya na usafi wa moyo. Haya ndo majukumu muhimu kwa mwanaume juu ya mwanamke.
Na mwanaume katika Aayah hii haikusudii mume tu. Mwanaume sawa akiwa ni baba yake, kaka au walii wake yeyote yule ndiyo msimamizi wake na anatakiwa amuhifadhi. Hata mambo yakifika mbali kukahitajika kumuadhibu, amuweke adabu. Allaah Anasema:
وَاللاَّتِي تَخَافُونَ نُشُوزَھُنَّ فَعِظُوھُنَّ وَاھْجُرُوھُنَّ فِي الْمَضَاجِعِ وَاضْرِ
“Na [wanawake] ambao mnachelea kutoka katika utiifu wanasihini, muwahame katika malazi na wapigeni.” (4:34)
Mwanamke anahitaji kuangaliwa. Maadui wa Uislamu leo, macho yao yote wameyatupilia kwenye masuala ya mwanamke. Kwa kujua kwao ni kitu cha khatari katika jamii. Macho yote wametupilia kwake. Wanapiganisha chini juu ili waweze kumuondoshea usafi wake na heshima yake kwa kutumia kwao hoja mwanamke anakandamizwa.
Ikiwa mwanamke atashikamana na usafi na heshima yake, wanasema yuko chini ya uhuru wake. Ilihali uhuru wake umehifadhiwa.

Uhuru wake uko katika kumtii Allaah, uhuru wake uko katika kuwalea vizuri watoto na aweze kutimiza wajibu aliopewa na Allaah kwani yeye ni mchungaji. Ni mchungaji wa nyumba ya mume wake na ataulizwa kwa alichokichunga. Huu ndiyo uhuru wake Sahihi.
Ama uhuru wake kwa kujiachia uchi, uhuru wake kwa kujianika juu mbele ya watu, kujitembeza kwenye masoko, kwenda anapotaka - huu ni utumwa na siyo uhuru. Huu ni utumwa wa shahawa (matamanio), utumwa wa Shaytwaan.
Uhuru enyi waja wa Allaah! Ni katika kumtii na kumuabu Allaah. Huko ndiko kuna heshima ya nafsi na karamu ya mtu na mafanikio yake hapa duniani na huko Aakhirah. Ama kwa yule anayemuasi Allaah na amri Zake, sawa wakiwa ni wanawake au wengineo - mtu kama huyu ni mtumwa dhalimu wa Shaytwaan. Huu ni utumwa wala siyo uhuru.
Ni juu yetu kujua masuala haya. Na tuwahifadhi wanawake wetu pakiweno wake zetu, mabanati zetu na ndugu zetu. Tusaidizane baina yetu katika kuwalinda na tusisikie propanganda hizi (za makafiri). Hakika Makafiri wanataka kutokomeza Uislamu kwa kutumia njia zote. Na njia kubwa ya kuuharibu [Uislamu] ni kumuharibu mwanamke. Kwa kuwa mwanamke ndiyo msingi wa familia na nyumba, akiharibika nyumba nayo itaharibika na familia nayo itaharabika. Mabanati wataharibika kwa kumuiga mama yao na ndugu zao.
Ni wajibu wetu kuwahifadhi wanawake wetu. Makafiri wamefanikiwa kufedhehesha baadhi ya miji ya Kiislamu, hawatoweza Inshaa Allaah - kufanikiwa kuharibu mji huu mtukufu wenye Misikiti miwili mitukufu ambapo Wahyi uliteremshwa kwa Mtume (swalla Allaahu 'alayhi wa sallam). Kuko Wanawaume wanahifadhi heshima yake, hata kama baadhi ya wadanganyifu wanaume na wanawake watachukulia mambo rahisi. Mji huu uko na wanaume wanahifadhi heshima yake na heshima ya wanawake wao.
Na nyinyi - Inshaa Allaah - ni miongoni mwao na mtalifanyia kazi hilo. Ni juu yetu kumcha Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) na tuishi juu ya hii amanah kubwa.

Amanah ambayo tukiihifadhi tutakuwa tumehifadhi nyumba zetu, watoto wetu, familia yetu na jamii yetu. Yeye mwanamke ndiye msingi.
Ndio maana maadui wamemlenga sana mwanamke. Macho yote wamemtupia yeye. Wamemlenga kabisa; kwenye vitabu, suhuf, magazeti, vyombo vya habari, internet na sehemu nyengine zote. Wanataka mji huu uwe kama miji mingine, ili tabia na heshima indoke. Ili iwe rahisi kwa makafiri kuuharibu Uislamu kuanzia kwenye msingi wake.
Anasema mshairi:
“Ummah bado upo ilihali tu tabia ipo. Wakati tu tabia zao zitatoweka, watatoweka nao.”
Tabia ikitoweka, hakuna kinachobaki. Makusudio ya tabia ni heshima, malezi, haya na hadhi. Hii ndio tabia.
Mashairi mwingine anasema:
“Mimi sisemi mwanamke aachwe aende uso wazi kama mwanaume aendavyo kwenye masoko. Kwenye manyumba yao (wanawake) wana shughuli nyingi sana kama shughuli aliyo nayo mwanaume ya upanga na mkuki.”
Mwanamke ana kazi yake na mwanaume ana ya kwake. Ikiwa kila mmoja atashikamana na kazi yake, jamii itatengemaa na mafanikio yatatimia. Na nidhamu ikiyumbishwa - Ummah unaharibika. Ndio maana Mtume (swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kawalaani wanaume wanaojifananisha na wanawake na wanawake anaojifananisha na wanaume. Yote haya ni ili kumuhifadhi mwanamke, na ili abaki kwenye asili yake (ya kike), dini yake, tabia yake na heshima. Heshima yake na hadhi yake iangaliwe na kuhifadhiwa.

Soma Surat "an-Nuur". Mtakuta mambo makubwa na ajabu ya kumuhifadhi mwanamke; kwa kujisitiri na kuomba ruhusa kabla ya kutoka nyumbani. Hali kadhalika Sunnah. Mtume (swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kakataza mwamamke kusafiri peke yake bila ya kuwa na Mahram na akasema:
"Si halali kwa mwanamke anaemwamini Allaah na siku ya mwisho kusafiri bila ya yeye kuwa na Mahram." (Bukhaariy (3006) na (Muslim (1341))
Kakataza mwanamke kuwa na mwanaume faragha ambaye siyo Mahram wake. Akasema:
"Mwanaume hawi na mwanamke faragha isipokuwa watatu wao huwa ni Shaytwaan." (Tirmidhiy (1171))
Amekataza mchanganyiko wa wanawake na wanaume. Ndio maana wanawake walikuwa wakiswali na Waislamu kwenye Msikiti wa Mtume (swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) na nyuma ya Mtume (swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) wakiwa nyuma ya wanaume wamejisitiri vizuri. Hakuna hata mmoja aliekuwa anawajua. Walikuwa wanaswali nyuma ya wanaume.
Hii ni dalili ya kutojuzu mchanganyiko. Ikiwa mwanamke haijuzu kuchanganyika na mwanaume msikitini mahali pa 'ibaadah na taqwa, tusemejemchanganyiko wa kwenye maofisi, sehemu za furaha, masherehe, masoko?!
Jambo hili ni khatari sana. Na sisi tumezungukwa na maadui hivi sasa na fikra za kipotofu. Makafiri wanashambulia kwenye miji ya Kiislamu kwa silaha, fikra potofu kwa kutumia kila njia. Tumezungukwa na Maadui kama nilivyosema.
Ni juu yetu tuwe macho kwa hili. Lakini ikiwa sisi tutakuwa na Allaah, Allaah Atakuwa na sisi.

قَالَ لَا تَخَافَا إِنَّنِي مَعَكُمَا أَسْمَعُ وَأَرَى
“Akasema: Msiogope! Hakika Mimi ni pamoja nanyi. Nasikia na ninaona.” (20:46)
Tukiwa na Allaah, Allaah Atakuwa nasi. Na Allaah Akiwa nasi, hakuna hata mmoja awezaye kutudhuru.
لاَ تَحْزَنْ إِنَّ للهَّ مَعَنَا
“Usihuzunike. Hakika Allaah yu pamoja nasi.” (4:40)
Lakini nani ambaye yuko na Allaah? Allaah yuko na wanaomcha, wanaofanya mema na waumini. Ni wajibu wetu tuwe na Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala).
Kama alivyosema Mtume (swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kumwambia Ibn 'Abbaas:
"Ewe kijana! Muhifadhi Allaah, naye Atakuhifadhi. Muhifadhi Allaah, utamkuta mbele yako." (Tirmidhiy (2516))
Ni wajibu wetu kuwa na Allaah, kumtii, kufuata maamrisho Yake na kuachana na makatazo Yake mpaka Allaah awe nasi (Subhaanahu wa Ta'ala) kwa nusra Yake na msaada Wake.
Ninamuomba Allaah msahama na kutubu Kwake.
Swalah na salaam nimwendee Mtume wetu Muhammad (swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na ahli zake na Maswahaba wake (radhiya Allaahu ´anhum).
Chanzo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/5405
 
 
 Posted By Posted juu ya Wednesday, December 19 @ 12:51:35 PST na MediaSwahiliTeam
 
 
:-: Go Home :-: Go Top :-:
 
 
 
Comments & Debates :-: التعليقات والمحاورات

 
 
For Your Membership Comments And Registered Debates Please, See Below Or Register Here :-: للحصول على تعليقات عضويتك و مناقشات الأعضاء انظر من فضلك أدناه أو سجّل هنا
 
 
:-: Go Home :-: Go Top :-:
 

Kuhusiana Viungo

· zaidi Mkuu - teknolojia na taaluma
· Habari na MediaSwahiliTeam


Kweli kusoma hadithi kuhusu Mkuu - teknolojia na taaluma:
MATUMIZI YA KUNUFAISHA YA HABBAT SAWDAA-1 -- (HABA SODA - CHEMBE NYEUSI )


Kifungu Rating

Wastani matokeo: 0
Kura: 0

Tafadhali chukua ya pili na kupiga kura kwa ajili ya makala hii:

bora Vizuri Sana Mema Kawaidar Mbaya

Chaguzi


 Chapa Rafiki Chapa Rafiki


Mada zinazohusiana

Mkuu - teknolojia na taaluma

 

 
EsinIslam The Muslim World Portal For Islamics, News, Fatwas, Audios, Videos, Muslim News, Quranic Islamic Articles, Radio, Audio Quran, TV Channels, Fatwa Rulings, Muslim News Newspapers Magazines Headlines Articles Forums Schools, Universities, Colleges, Mosques, Qur'an, Hadith, Sunnah, Fiqh, Prayers, Salat, Fasting Ramadan, Vidoes, Books On EsinIslam.Com And Muxlima.Com

  :-: Go Home :-: Go Top :-: