Swahili
- Ukurasa Kuu    - Kumi Juu    - Mada Mpya    - Salimisha Habari    - Tafuta    - Kiswahili Jukwaa    - Kiswahili Wanachama    - Tathmini    - Ujumbe wa Kibinafsi    - Tafiti    - Majarida    - Hadithi Archive    - Maudhui    - Viungo vya Wavuti    - Vipakuliwa    - Maswali ya Kawaida    - Tunapendekeze    - Orodha ya Kuingia   

 

 
Haki Za Mume Na Mke: Nasaha Za Shaykh Kwa Wanandoa
 
 
bakom domstolens rättspraxis ya Kii الحقوق بين الزوجين: Haki Za Mume Na Mke
(Nasaha Za Shaykh Kwa Wanandoa)

Muftiy al-´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aal ash-Shaykh
Mfasiri:
Abu Bakr Khatwiyb al-Atrush

Himidi zote zi Zake Allaah. Tunamhimidi na kumtaka msaada na tunamuomba msamaha na tunatubia Kwake. Na tunajikinga Kwake na shari za nafsi zetu na matendo yetu maovu.
Hakika yule Aliyemuongoza Allaah hakuna wa kumpoteza. Na Aliyempoteza hakuna wa kumuongoza.
Nashuhudia ya kwamba hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Allaah wa pekee Asiyekuwa na mshirika. Na ninashuhudia ya kwamba Muhammad ni mja Wake na Mtume Wake swalah za salaam zimuendee na ahli zake na Maswahaba wake mpaka siku ya mwisho. Amma ba´ad:Enyi watu! Mcheni Allaah ukweli wa kumcha. Enyi waja wa Allaah! Hakika familia ndio msingi wa jamii; makazi ambayo Allaah Ameyafanya kwa mume kuwa ndio makazi yake na kukaa humo. Katika ndoa kuna utulivu wa nafsi, na kupumua, na mafanikio ya kutokufanya mapenzi na kuwa na usafi wa moyo. Na ndoa ni uhusiano uliyo imara, na mkataba madhubuti, [kama Asemavyo Allaah]:
وَأَخَذْنَ مِنكُم مِّيثَاقًا غَلِيظًا
“Na wao wanawake wamechukua kwenu ahadi iliyo madhubuti.” (04:21)
Na ni ahadi ya wanandoa, kutendeana mema, na ni kuyawekea nguvu maisha ya kindoa. Na Katubainishia Allaah katika Kitabu Chake na Mtume Wake (
صلى لله عليه وسلم ) ahkaam za ndoa wazi kabisa. Zipi haki za mwanaume na yapi
ya wajibu juu yake; na ni zipi haki za mwanamke na ni yapi ya wajibu juu
yake.

Wakati wanandoa [mume na mke]watachunga haki hizi na yaliyo yawajibu kwa kila mmoja, yanakuwa maisha yao - maisha mazuri.
Enyi wanandoa! Ikiwa kweli mnataka maisha mazuri yaliyo thabiti, yaliyojengeka katika misingi ya mahaba na mapenzi; mwatakiwa nyote wawili kumchungia [kumtekelezea] kila mmoja haki ya mwenzake kwa usawa katika maisha haya.
Ewe dada mwenye thamani! Hakika mume wako ana haki juu yako na ya wajibu; ni lazima kumtekelezea [kwa kufanya hivyo] ni utiifu kwa Allaah, na ni ukurubisho unajikurubisha kwao kwa Allaah. Katika haki kubwa za mume wako juu yako, ni kumtii katika mema. Hakika kumtii katika mema ni jambo la wajibu kwako. Anasema Allaah (Jalla wa ´Alaa):
فَإِنْ أَطَعْنَكُمْ فَلاَ تَبْغُواْ عَلَيْھِنَّ سَبِيلاً
“Wakikutiini msiwatafutie njia ya kuwaudhi bure.” (04:34)
Utiifu huwa katika mema tu. Hakuna utiifu kwa yeyote katika kumuasi Allaah. Anasema Allaah (Jalla wa ´Alaa):
وَعَاشِرُوھُنَّ بِالْمَعْرُوفِ
“Na kaeni nao kwa wema.” (04:19)
Ewe mwanamke wa Kiislamu! Hakika mume wako ana haki juu yako ya kumtii katika mema. Na Mtume ( صلي لله عليه وسلم ) anasema:

"Akimwita mume mke wake kitandani, [asije] na mume wake akamkasirikia, Malaika wanamlaani mpaka asubuhi."
Katika kumtii mume wako kuna thawabu kubwa mbele ya Allaah. Anasema Mtume ( :( صلي لله عليه وسلم
"Akiswali mwanamke [swalah zake] tano, na akafunga mwezi wake, akahifadhi tupu yake na akamtii mume wake ataingia Peponi katika mlango wowote aupendao [katika milango minane ya Peponi]."
Hii ni fadhila kubwa na neema kubwa kwa Allaah kwako, ewe dada wa Kiislamu kwa kumtii mume wako katika mema.
Na katika haki zake za wajibu juu yako, ni kumtekelezea haja zake atapotaka hilo. Hakika katika ndoa kuna kuzihifadhi tupu kwa halali, kuilinda na aliyomuharamishia Allaah kwake.Anasema Mtume ( :( صلي لله عليه وسلم
"Atapomwita mume mke wake juu ya kitanda na akakataa, akamghadhibikia, hivyo Malaika humlaani mpaka asubuhi."
Na kwa hili kaelekezwa mume kwa mkewe, na wakajaaliwa hilo kuwa ni swadaqah kwa wote wawili - mume na mke. Anasema Mtume ( صلي لله عليه وسلم
):
"Na kumuingilia mkeo ni swadaqah.” Wakasema (Maswahabah) na je, katika kupata raha binafsi mmoja wetu analipwa??! Mtume ( ( صلى لله عليه وسلم
akasema: “Je, mnaonaje lau mtu huyo angeingiza [tupu yake] katika haramu,
je, ingelikuwa ni shari juu yake [ya madhambi, maradhi, adhabu]?, wakasema:
ndio. Akasema Mtume ( صلى لله عليه وسلم ): “Hivyo ndivyo atakapoweka [tupu
yake] katika halali atalipwa.” [Muslim]
Na katika haki za mume wako juu yako, ni kuwa na adabu na kumheshimu, hii ni amaanah umeaminiwa kwayo.

Mwanamke mwema, mwenye mtazamo mzuri kumuangalia mume wake; mwenye kujihifadhi ili kudumisha sifa ya kitanda chake, hivyo ni bora.
لله فَالصَّالِحَاتُ قَانِتَاتٌ حَافِظَاتٌ لِّلْغَيْبِ بِمَا حَفِظَُّ
“Basi wanawake wema ni wale wenye kutii na wanaojilinda hata katika siri kwa kuwa Allaah Ameamrisha wajilinde.” (04:34)
Na katika Hadiyth, anasema ( :( صلي لله عليه وسلم
"Bora ya raha kwa mwanaume ni kupata mke mwema, [ambaye] akimtazama anafurahi, na akimuamrisha [kitu] anamtii, na [mume] akiwa mbali naye hujihifadhi mwenyewe [mwanamke] na mali [ya mumewe]."
Ewe dada ´Aziyzah! Hakika kumridhisha kwako mume wako na kumheshimu, ni jambo jema, na ni kitu kizuri, na ni jambo la wajibu juu yako Kishari´ah; Usidanganyike na hayo mafilamu machafu, ambayo yanakuweka mbali na heshima yako na fadhila zako na yaliyojaa maovu. Allaah Atusamehe sote kwa hayo.
Na katika haki za mume juu yako, usimruhusu yeyote kuingia nyumbani bila idhini [ruhusa] yake. Utaejua kuwa hatomridhia kuingia usimruhusu. Kwa kuwa Mtume ( صلى لله عليه وسلم ) anasema:
"Si halali kwa mwanamke kumruhusu yeyote kuingia nyumbani kwa mume wake ila kwa idhini [ruhusa] yake."
Na katika haki za mume juu yako, kuchunga nyumba yake na mali yake. Katika Hadiyth [anasema Mtume]:

"Mwanamke ni mchungaji katika nyumba ya mume wake na ataulizwa [na Allaah] kwa alichokichunga."
Na kakataza Mtume ( صلى لله عليه وسلم ) kutoa katika mali ya mume wako ila
kwa idhini yake [mume].
Na katika haki za mume juu yako, usimkalifishe kukuhudumia [kukupatia matumizi] kile asichokiweza na ni kizito kwake na hakiwezi. Hakika Allaah Anasema:
لله لِيُنفِقْ ذُو سَعَةٍ مِّن سَعَتِهِ وَمَن قُدِرَ عَلَيْهِ رِزْقُهُ فَلْيُنفِقْ مِمَّا آتَاهَُُّ
“Mwenye wasaa atoe kadiri ya wasaa wake, na mwenye dhiki atoe katika alichompa Allaah. Allaah Hamkalifishi mtu ila kwa kadiri ya alicho mpa.” (65:07)
Na katika haki za mume juu mke, ni kuwapa malezi watoto na kuwaongoza; nyote wawili mume na mke ni wenye kushiriki katika jambo hili muhimu sana. Kuwapa malezi vijana na kuwaandaa wawe vizuri, na kuwaamrisha mema na kuwatahadharisha na shari. Na kule baba kuwa kwake kiigizo bora kwa watoto wakiume, katika kheri na wema. Na mama ana jukumu lakuwa kiigizo bora kwa mabanati wake, kwa kujisitiri vizuri na usafi wa moyo, na dhamira ya maadili ya thamani.
Na katika haki za mume juu yako, ni wewe kubaki nyumbani na kutotoka ila tu kwa dharurah. Ama kutoka kwako nyumbani bila ya dharurah kunaifanya nyumba kuzorota na kukosekana mwenye kuilinda na kuihifadhi.
Na katika haki za mume juu yako ni wewe kutomuudhi kwa maneno mabaya. Mwambie [muongeleshe] maneno mazuri yenye baraka. Kuuachia ulimi hovyo, haimpasi mwanaume wala mwanamke. Na imepokelewa kutoka kwa Mtume ( صلى لله عليه وسلم ) kuwa amesema:
"Akimuudhi mwanamke mume wake duniani, anasema mke wake katika Huur al-'Iyin "Allaah Akuangamize usimuudhi, kwani huyo ni mtu wetu - imekaribia kuachana nawe na kuja kwetu."

Na katika haki za mume wajibu juu yako, usijikurubishe kwa Allaah kwaswalah za naafilah [sunnah] na swawm [za sunnah] ila kwa idhini [ruhusa] ya mume wako.
Hakika haki yake [mume] ni yenye kutangulia. Na kwa hili anasema Mtume (
:( صلى لله عليه وسلم
"Si halali kwa mwanamke kufunga, na mume wake yuko ila kwa idhini yake."
Katika haki za mume juu yako, aliyobainisha Mtume ( ( صلى لله عليه وسلم
kuwatahadharisha wanandoa [mume na mke] kutoa siri ya uhusiano wa
kindoa [yafanyikayo ndani], akasema kuwa mwenye kufanya hivyo ni katika
watu waovu sana. Kwa kuwa hii ni dalili ya ukosevu wa haya na adabu.
(Haki Za Mke Juu Ya Mume)
Ndugu mume karimu, hakika mke wako ana ya wajibu pia juu yako na haki zake. Lazima umtimizie - kama jinsi yeye kwako ana haki zake na ya wajibu, na wewe hali kadhalika una haki na ya wajibu juu yake. Lazima umtimizie.
Haki yake kubwa juu yako, ni wewe kumpa mahari kwa ukamilifu; sawa akiwa ni mwenye uwezo au si mwenye uwezo. Kwa kuwa Allaah Anasema:
وَآتُواْ النَّسَاء صَدُقَاتِھِنَّ نِحْلَةً فَإِن طِبْنَ لَكُمْ عَن شَيْءٍ مِّنْهُ نَفْسًا فَكُلُوهُ ھَنِيئًا مَّرِيئًا
“Na wapeni wanawake mahari yao hali ya kuwa nikipawa. Lakini wakikutunukieni kitu katika mahari - kwa radhi yao, basi kileni kiwashuke kwa raha.” (04:04)
Ni wajibu kumpa haki yake kamili. Katika haki zake juu yako, ni kumpa matumizi [kumuhudumia] chakula, mavazi na makazi. Anasema Allaah (Ta´ala):

وَعَلَى الْمَوْلُودِ لَهُ رِزْقُھُنَّ وَكِسْوَتُھُنَّ بِالْمَعْرُوفِ
“Na ni juu ya mzazi wa kiume kuwapatia chakula chao na nguo kwa ma’aruwf (mujibu wa ada).” (02:233)
Akasema tena:
أَسْكِنُوھُنَّ مِنْ حَيْثُ سَكَنتُم مِّن وُجْدِكُمْ وَلَا تُضَارُّوھُنَّ لِتُضَيِّقُوا عَلَيْھِنَّ
“Wawekeni humo humo mnamokaa nyinyi kwa kadiri yapato lenu, wala msiwaletee madhara kwa kuwadhiki.”(65:06)
Matumizi ni wajibu kwa mume kumpa mke wake, kwa mujibu wa mkataba wa ndoa baina yao. Na Mtume ( صلى لله عليه وسلم )anasema kumwambia Saad
bin Abi Waqqas kuhusiana na hili:
"Hakika hutotoa matumizi kwa kutaka Uso wa Allaah isipokuwa utapewa ujira kwalo, hata ikiwa ni kitu kidogo utachokiweka kwenye kinywa cha mkeo."
Na katika haki zake juu yako, ni kukaa nae kwa wema kwa adabu za Kishari´ah. Anasema Allaah (Jalla wa ´Alaa):
وَعَاشِرُوھُنَّ بِالْمَعْرُوفِ
“Na kaeni nao kwa wema.” (04:19)
Anasema tena:
وَلَھُنَّ مِثْلُ الَّذِي عَلَيْھِنَّ بِالْمَعْرُوفِ

“Na hao wanawake wana kama ile (haki) iliyo juu yao kwa ma’aruwf (mujibu wa shari’ah).” (02:228)
Na anasema Mtume ( :( صلى لله عليه وسلم
"Mbora [wa wanaume ni] aliye mbora kwa familia yake, na mimi ni mbora kwa familia yangu."
Na katika haki zake juu yako, ni kumlinda [asipatwe na] adhabu ya Allaah kwa kumuamrisha mema na kumtahadharisha na shari [maovu].
يَا أَيُّھَا الَّذِينَ آمَنُوا قُوا أَنفُسَكُمْ وَأَھْلِيكُمْ نَارًا وَقُودُھَا النَّاسُوَالْحِجَارَةُ
“Enyi mlioamini! Jilindeni nafsi zenu na ahli zenu na Moto ambao kuni zake ni watu na mawe.” (66:06)
Anasema tena:
وَأْمُرْ أَھْلَكَ بِالصَّلَاةِ وَاصْطَبِرْ عَلَيْھَا لَا نَسْأَلُكَ رِزْقًا نَّحْنُ نَرْزُقُكَ وَالْعَاقِبَةُ لِلتَّقْوَى
“Na waamrishe watu wako kusali, na uendelee mwenyewe kwa hayo. Sisi hatukuombi wewe riziki, bali Sisi ndio tunakuruzuku. Na mwisho mwema ni kwa mcha Mungu.” (20:132)
Katika haki zake juu yako, ni wewe kuwa na wivu kwake, wivu ambao ni wakweli [mzuri] - kwa kumtakia kheri, na kumuonya na kila shari uijuayo; bila ya kuwa na wasiwasi [katika wivu wako] na mashaka, na matarajio ya makosa; bali iwe ni wivu ulioubeba kwa ajili ya kumtakia kheri na kumlinda asipatwe na shari. Usiwe ni wivu wa wasiwasi na mashaka na kuangalia tu udhaifu [wake]. Ni watu wangapi wamekuwa na aina ya maradhi kama haya, na kuona wengine si kama yeye. Ni wajibu kumcha Allaah.

Kama inavyotakikana kwa mwanamke pia kuwa na wivu kwa mume wake. Lakini anapaswa kuwa na wivu uliojengeka katika mambo ya wazi; si kwa uchunguzi wa fujo na vurugu na kuchunguza namba za simu - ukaguzi nakadhalika, jambo ambalo linaweza kusababisha shari na balaa baina yao.
Na katika haki za mwanamke juu ya mume wake, ni kumfunza mambo ya dini yake asiyoyajua na yatamsaidia kufanya mema.
Na katika haki zake juu yako, ni [wewe] mwanaume kuwa mwadilifu baina ya wake [zako] ukioa wake wengi [ukewenza]. Anasema Mtume ( صلى لله عليه
:( وسلم
"Yule mwenye wake wawili, akamkandamiza mmoja zaidi kuliko mwengine, atakuja siku ya Qiyaamah na bega lake likiwa limepinda."
Na katika haki zake juu yako, usimkandamize na kumnyima haki zake kwa kumdhulumu na kumfanyia uadui, kwani hakika dhuluma ni gizo siku ya Qiyaamah. Usitumii udhaifu wake na ukosevu wake wa mabavu, ukamuonea [mkandamiza] bila ya hatia yoyote, ukamtusi na kumtuhumu kwa mambo ambayo kajitenga nayo mbali.
Katika haki zake juu yako, ni kumhifadhia mali yake na usimtumie na ukaitumia mali yake; ukawa unamtisha kwa talaka akiomba haki yake na ukawa unaitumia. Yote haya ni katika uonevu. Hakika wajibu wako ni wewe kumhudumia sawa na uwezo wako, umejiingiza katika [maisha ya] ndoa pambana na ndoa hii.
Wakati mke atapotekeleza [timiza] wajibu alionao juu ya mume wake, na wakati mume atapotekeleza [timiza] wajibu alionao juu ya mke wake; hivyo maisha na hali huwa nzuri. Na wakati nyumba itaachwa, wakati kila mmoja atapoacha kutekeleza haki ya mwenzake; wakati mke atapoacha kumtimizia mume haki zake, au mume akaacha kumtimizia mwanamke haki zake; hivyo hutokea shari na uharibifu.

Ama kila mmoja akichunga haki alionayo juu ya mwenzake, hakika hii ndio sababu ya furaha na kuwa na maisha mazuri na familia huishi katika muelekeo na usalama.
Enyi watu! Mcheni Allaah (Ta´ala) ukweli wa kumcha. Shari´ah ya Uislamu imekuja kutekeleza uadilifu kwa njia zote. Na katika hayo ni uadilifu baina ya wanandoa, kwa kila mwanandoa mmoja kumtimizia mwengine. Mwanamke atimize yaliyo ya wajibu juu yake kwa mume wake; na mume atimizeyaliyo ya wajibu juu yake kwa mke wake.
Hivyo ndivyo yalivyo maisha ya ndoa yaliyofanywa na Uislamu kwa wanandoa ili waishi maisha ya furaha; maisha ya furaha na ridhaa.
Tumcheni Allaah katika nafsi zetu [kwa kila mmoja kumtimizia mwenzake haki yake].
Ewe mume ´Aziyz! Hakika kutania [kucheza] na mke [wako], wacheza naye na huku wamuelekeza katika mema ni katika sababu zinazoimarisha misingi ya maisha ya ndoa. Na hakika utoaji onyo mara kwa mara pasina sababu za kueleweka, ni katika sababu ya kufarakana.
Tahadhari muwe na kukithirisha maonyo ya mara kwa mara bila sababu. Tahadhari na kufuatilia vijikosa vidogo vidogo ambavyo havina uziro wowote. Kuwa mwenye kupuuza vijikosa ilimraditu havina kasoro katika heshima na cheochako, ni juu yako kuwa na subira kwa baadhi ya makosa; hakuna yeyote aliyesalimika kutokana na makosa. Anasema Mtume ( لله صلى
:( عليه وسلم
"Mwanaume asimchukie muumini mwanamke [mkewe], akichukizwa na moja ya tabia yake atapendezwa na nyingine."
Anasema tena [Mtume]:
"Ninawahusieni kuwatendea wanawake wema."
Subira kwa kila mmoja kumvumilia mwenzake ni jambo linalotakikana. Mwanamke awe na subira kwa mume wake, na kwa baadhi ya makosa kunako tabia yake na mwenendo wake ilimradi haijafikia katika kumvulia cheo na heshima. Na mume awe na subira juu ya baadhi ya makosa ya mke

wake, ilimradi haijafika kumvulia cheo na heshima. Iwe wote wanasaidizana kutengeneza na kumezea [kasoro] za kila mmoja kwa mwenzake.
Na Mtume ( صلى لله عليه وسلم ) kamtahadharisha mwanamke wa Kiislamu kwa
kukufuru kwake wema na kumlalamikia sana mume. Akasema kuwa ameona
moto na wakazi wake wengi ni wanawake; kwa tuoacha kwao kulalama na
kukufuru kwao wema.
Lau utamtendea mmoja wao wema maisha yote, akaona kutoka kwako kitu [kasoro], atasema "Sijawahi kuona kheri [wema] wowote kutoka kwako katu."
Ndugu wapenzi! Matatizo ya kindoa yanakuwa wakati mwingine kwa sababu zisizokuwa na maana. Wakati wakutafakari na kuzingatia vizuri mtu anakuja kuona kuwa sababu [zilizoleta matatizo] ni za kijinga zisizo na maana yoyote.
Ni juu ya wazazi wa ndugu wa mume au mke kutatua matatizo haya ndani ya nyumba, na yasiendelee mambo kama haya hadi yakatoka nje ya nyumba. Mume amalize tatizo lake na mke wake au na famili yake. Na juu ya familia yake mwanamke kumkanya wakiona yeye ndo yuko makosani. Na familia ya mwanamume hali kadhalika wamkanye watapoona kuwa yeye [mume] ndo yuko makosani.
Familia zote mbili zikisaidizana pamoja na mume na mke kutatua tatizo hili, hupatikana ufumbuzi mzuri. Ama ikiwa hawatokuwa makini na kujichunga, huwaka fitna. Mwanaume [baba mkwe] akawa na kasumba kwa binti yake bila kujali makosa yake; au mwanamume akawa na kasumba ya kushikilia rai yake bila kujali makosa yake. Hakika huo ni msiba mkubwa.
Na Mtume wetu ( صلى لله عليه وسلم ) kamtahadharisha mwanamke wa Kiislamu
kuomba talaka pasina sababu ya msingi. Akasema:
"Mwanamke akimuomba mume wake talaka pasina sababu muhimu, ni haramu juu yake harufu ya Pepo."
Hivyo ni wajibu kwao mauqif yao iwe ya heshima, mauqif ya kutatua tatizo, na kumaliza mgogoro huu, na kuzingatia tatizo hili - liangaliwe vizuri. Iangaliwe sababu na itatuliwe, na qadhiya hii ishughulikiwe ndani ya

nyumba. Isende ikatoka nje, khabari ikawafikia watu nje wasiyokuwa na thamani kwao, na wasiyowapendea kheri - wakaja kuiharibu nyumba na kuingamiza katika msingi wake. Hukumsikia Allaah Akisema:
وَإِنِ امْرَأَةٌ خَافَتْ مِن بَعْلِھَا نُشُوزًا أَوْ إِعْرَاضًا فَلاَ جُنَاْحَ عَلَيْھِمَا أَن يُصْلِحَا بَيْنَھُمَا صُلْحًا وَالصُّلْحُ خَيْرٌ
“Na mwanamke akichelea kutupwa au kutojaliwa na mumewe, basi si vibaya kwao wakisikizana kwa suluhu.Na suluhu ni bora.” (04:128)
Kutafuta suluhu baina ya wanandoa ni kheri, suluhu inayohitaji kuhifadhi haki ya kila mmoja, suluhu ya kutaka kutatua tatizo na kumaliza ugomvi, suluhu kurudi katika hali ya kawaida, na maisha ya ndoa kuendelea utulivu wake, suluhu inayolengo kupata Uso wa Allah na Nyumba ya Aakhirah. Tumche Allaah katika nafsi zetu.
Na hakika wengi hawatafakari katika sababu ya talaka zilizoko kati ya wanandoa; unaweza kuona imejengeka katika misingi ya kukosekana kwa utulivu, na sababu ya talaka hii na mwenye kuiomba si kitu muhimu kwa kweli bali ni upumbavu wa baadhi ya wanaume au haraka za baadhi ya familia ya mwanamke; mambo ambayo badala yake yangeliweza kutatuliwa katika ngazi ya familia bila ya kutoka nje ya nyumba. Namuomba Allaah kwa sote Atupe Tawfiyq na Sadaad, na msaada wa mwongozo wa kila kheri. Hakika Yeye ni Muweza wa kila kitu.
Swalah za salaam zimuendee Mtume wetu Muhammad ( صلى لله عليه وسلم ) na
ahli zake na Maswahaba wake na watakaomfuata kwa wema mpaka siku ya
Qiyaamah.
Chanzo: http://www.mufti.af.org.sa/node/1757
Chanzo: http://www.youtube.com/watch?v=KiMB0LP_OWE
 
 
 Posted By Posted juu ya Wednesday, December 19 @ 12:50:19 PST na MediaSwahiliTeam
 
 
:-: Go Home :-: Go Top :-:
 
 
 
Comments & Debates :-: التعليقات والمحاورات

 
 
For Your Membership Comments And Registered Debates Please, See Below Or Register Here :-: للحصول على تعليقات عضويتك و مناقشات الأعضاء انظر من فضلك أدناه أو سجّل هنا
 
 
:-: Go Home :-: Go Top :-:
 

Kuhusiana Viungo

· zaidi bakom domstolens rättspraxis ya Kii
· Habari na MediaSwahiliTeam


Kweli kusoma hadithi kuhusu bakom domstolens rättspraxis ya Kii:
Haki Za Mume Na Mke: Nasaha Za Shaykh Kwa Wanandoa


Kifungu Rating

Wastani matokeo: 4
Kura: 2


Tafadhali chukua ya pili na kupiga kura kwa ajili ya makala hii:

bora Vizuri Sana Mema Kawaidar Mbaya

Chaguzi


 Chapa Rafiki Chapa Rafiki


Mada zinazohusiana

bakom domstolens rättspraxis ya Kii

 

 
EsinIslam The Muslim World Portal For Islamics, News, Fatwas, Audios, Videos, Muslim News, Quranic Islamic Articles, Radio, Audio Quran, TV Channels, Fatwa Rulings, Muslim News Newspapers Magazines Headlines Articles Forums Schools, Universities, Colleges, Mosques, Qur'an, Hadith, Sunnah, Fiqh, Prayers, Salat, Fasting Ramadan, Vidoes, Books On EsinIslam.Com And Muxlima.Com

  :-: Go Home :-: Go Top :-: