Swahili
- Ukurasa Kuu    - Kumi Juu    - Mada Mpya    - Salimisha Habari    - Tafuta    - Kiswahili Jukwaa    - Kiswahili Wanachama    - Tathmini    - Ujumbe wa Kibinafsi    - Tafiti    - Majarida    - Hadithi Archive    - Maudhui    - Viungo vya Wavuti    - Vipakuliwa    - Maswali ya Kawaida    - Tunapendekeze    - Orodha ya Kuingia   

 

 
Zichume Sifa Kumi Njema - Sifa Ya Tano - Wanaume Wanaosubiri Na Wanawake Wanaosu
 
 
Mkuu - teknolojia na taaluma Zichume Sifa Kumi Njema - Sifa Ya Tano - Wanaume Wanaosubiri Na Wanawake Wanaosubiri

Anasema Allaah سبحانه وتعالى :

((إِنَّ الْمُسْلِمِينَ وَالْمُسْلِمَاتِ وَالْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ وَالْقَانِتِينَ وَالْقَانِتَاتِ وَالصَّادِقِينَ وَالصَّادِقَاتِ وَالصَّابِرِينَ وَالصَّابِرَاتِ ))

((Hakika Waislamu wanaume na Waislamu wanawake, na Waumini wanaume na Waumini wanawake, na watiifu wanaume na watiifu wanawake, na wasemao kweli wanaume na wasemao kweli, wanaosubiri wanaume na wanaosubiri wanawake ….)) [Ahzaab:35]

Sifa ya tano ni wanaosubiri wanaume na wanawake. Subira inahitajika katika kila ibaada na katika kila mambo hasa ya kuamiliana baina yetu. Ndio maana utakuta Allaah (Subhaana wa Ta'aala) Ametaja mara kwa mara subira katika Qur-aan na fadhila zake pia. Vile vile zimetajwa katika Hadiyth mbali mbali. Kuna aina nyingi za subira kama zifuatazo:

Subira katika kufanya ibada:
Nalo ni jambo zito kama Anavyosema Allaah (Subhaana wa Ta'aala):

((وَاسْتَعِينُواْ بِالصَّبْرِ وَالصَّلاَةِ وَإِنَّهَا لَكَبِيرَةٌ إِلاَّ عَلَى الْخَاشِعِينَ))

((Na tafuteni msaada kwa kusubiri na kwa kuswali; na kwa hakika jambo hilo ni gumu isipokuwa kwa wanyenyekevu)) [Al-Baqarah:45]

((يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اسْتَعِينُواْ بِالصَّبْرِ وَالصَّلاَةِ إِنَّ اللّهَ مَعَ الصَّابِرِينَ))

((Enyi mlioamini! Takeni msaada kwa subira na Swalah. Hakika Allah Yu pamoja na wanaosubiri)) [Al-Baqarah:153]

Ibada zote ni nzito kuzifanya kwani kila moja inahitajia subira. Swalah inahitajia subira kuwa na unyenyekevu, Swawm inahitajia subira kukaa na njaa, kiu na kujizuia na matamanio ya nafsi, Zakah inahitajia subira kutoa mtu mali yake aliyorundika, Hajj inahitajia subira na mashaka yanayompata mtu anapokwenda kutimiza fardhi hii, na kila aina ya ibada yoyote inahitajia subira.

Subira katika kujiepusha na maasi:

Nayo ni kufanya jihaad ya nafsi kugombana na matamanio maovu japokuwa lile jambo unalipenda sana. Mfano mwenye kupenda sana muziki, ambapo mara nyingi shaytwaan katika jambo hili humfanyia binaadamu liwe gumu kabisa kwake kuliepuka, kwani anaweza Muislamu kuacha maasi mengine makubwa lakini inapofika kutaka kuacha nyimbo (muziki) huwa ni jambo zito, kwa vile wengi wanafikiri kuwa nyimbo si maasi makubwa na hali Allaah (Subhaana wa Ta'aala) Amekataza katika Qur-aan Anaposema:

((وَمِنَ النَّاسِ مَن يَشْتَرِي لَهْوَ الْحَدِيثِ لِيُضِلَّ عَن سَبِيلِ اللَّهِ بِغَيْرِ عِلْمٍ وَيَتَّخِذَهَا هُزُوًا أُولَئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ مُّهِينٌ))

((Na miongoni mwa watu wapo wanaonunua maneno ya upuuzi, ili wawapoteze watu na njia ya Allah pasipokujua, na wanaichukulia ni maskhara. Hao watapata adhabu ya kuwafedhehesha)) [Luqmaan:6]

Ibn Mas'uud (Radhiya Allahu 'anhu) amesema kuhusu Aayah hii: "Naapa kwa Allah hii ina maana ni nyimbo" [At-Twabariy 20:127]

Subira katika kufanya da'awah:

Hii ni kazi ngumu kabisa ambayo mtihani wake umewafikia Mitume wote katika kuwaita watu kwenye Tawhiyd. Maudhi na kusumbuliwa sana na watu wao kuliwafanya Mitume wavumilie uvumilivu wa hali ya juu kabisa, hali hiyo ilimkabili vilevile Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), naye pia alipata maudhi makubwa ya kutukanwa, kupigwa na kutengwa, na ndipo kila mara Allaah (Subhaana wa Ta'aala) Alikuwa akimkumbusha kuwa si pekee mwenye kupata misukosuko ya watu, bali Mitume wenzake pia wamepitia maudhi na Akimsimulia visa vya Mitume katika Qur-aan.

Vile vile sisi kwa sisi tunapofanya da'awah kuwaita ndugu zetu wawe karibu na Mola wao, kwa kuacha maasi na kuwakumbusha wamche Mungu kwa kila aina ya mawaidha, nayo pia inataka subira. Na hii ndio kazi yetu Waumini, nayo ni miongoni mwa mambo manne ambayo kila mja anapaswa awe anayatimiza, au sivyo atakuwa ni mja mwenye khasara kama Anavyosema Allaah (Subhaana wa Ta'aala):

وَالْعَصْرِ ﴿1﴾ إِنَّ الْإِنسَانَ لَفِي خُسْرٍ ﴿2﴾ إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَتَوَاصَوْا بِالْحَقِّ وَتَوَاصَوْا بِالصَّبْرِ ﴿3﴾

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
1. Naapa kwa Zama!
2. Hakika binaadamu bila ya shaka yumo katika khasara,
3. Ila wale walioamini, na wakatenda mema, na wakausiana kwa haki, na wakausiana kusubiri [Al-'Aswr]

Subira katika Aayah hiyo imetanguliza kuusiana ya haki, na unapokataza mambo ambayo ni makosa katika dini wanayotenda watu, na ukawanasihi waache na ukawajulisha yale yaliyo ya haki, si wepesi watu kuyapokea na kuyakubali, isitoshe huenda wakakufanyia uadui au wakakutenga.

Tunaona jinsi Luqmaan alipompa nasaha mwanawe alivyotambua uzito wa jambo la da'awah:

((يَا بُنَيَّ أَقِمِ الصَّلَاةَ وَأْمُرْ بِالْمَعْرُوفِ وَانْهَ عَنِ الْمُنكَرِ وَاصْبِرْ عَلَى مَا أَصَابَكَ إِنَّ ذَلِكَ مِنْ عَزْمِ الْأُمُور)) ِ

((Ewe mwanangu! Shika Swalah, na amrisha mema, na kataza maovu, na subiri kwa yanayokupata. Hayo ni katika mambo ya kuazimiwa)) [Luqmaan:17]

Subira katika maafa:

Maafa ni aina nyingi; vifo vya wapenzi wetu, njaa, kupungukiwa na mali, magonjwa, maafa ya kidunia kama mtetemeko wa ardhi, mafuriko, ajali, vita n.k. Lakini kwa wenye kuwa na subira yanapowafikia mitihani hiyo, Allaah (Subhaana wa Ta'aala) Amewabashiria mema mengi nayo kama Anavyotaja katika Aayah zifuatazo:

((وَلَنَبْلُوَنَّكُمْ بِشَيْءٍ مِّنَ الْخَوفْ وَالْجُوعِ وَنَقْصٍ مِّنَ الأَمَوَالِ وَالأنفُسِ وَالثَّمَرَاتِ وَبَشِّرِ الصَّابِرِينَ))
((الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُم مُّصِيبَةٌ قَالُواْ إِنَّا لِلّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعونَ أُولَئِكَ عَلَيْهِمْ صَلَوَاتٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَرَحْمَةٌ وَأُولَئِكَ هُمُ الْمُهْتَدُونَ))


((Hapana shaka Tutakujaribuni kwa chembe ya khofu, na njaa, na upungufu wa mali na watu na matunda. Na wabashirie wanaosubiri))

((Wale ambao ukiwasibu msiba husema: Hakika sisi ni wa Allah, na Kwake Yeye hakika tutarejea))

((Hao juu yao zitakuwa baraka zitokazo kwa Mola wao Mlezi na Rehma. Nao ndio wenye kuongoka)) [Al-Baqarah:155-157]

Vile vile Huwapa waja Wake wema wenye kuwa na subira ya kila aina tulizozitaja hapo juu, ujira mwingi usiohesabika.

((إِنَّمَا يُوَفَّى الصَّابِرُونَ أَجْرَهُم بِغَيْرِ حِسَابٍ))

((Hakika wenye subira watapewa ujira wao bila ya hisabu)) [Az-Zumar:10]

Na Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametuelezea fadhila za subira vile vile katika Hadiyth nyingi, tunazitaja mbili tu zifuatazo:

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قال : قال رسول اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ : (( مَنْ يَتَصَبَّرْ يُصَبِّرْهُ اللَّهُ ، وَمَا أُعْطِيَ أَحَدٌ عَطَاءً خَيْرًا وَأَوْسَعَ مِنْ الصَّبْر)) البخاري ومسلم

Kutoka kwa Abu Sa'iydil-Khudriyyih (Radhiya Allah 'anhu) kwamba, amesema Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam: ((Atakayetaka kusubiri (kufanya subira) basi Allaah Atampa subira. Na hakupewa mtu jambo la kheri na pana kama subira)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

عَنْ أُمِّ سَلَمَةَ رضي الله عنها أَنَّهَا قَالَتْ : سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُول: ((مَا مِنْ مُسْلِمٍ تُصِيبُهُ مُصِيبَةٌ فَيَقُولُ مَا أَمَرَهُ اللَّهُ " إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ ، اللَّهُمَّ أْجُرْنِي فِي مُصِيبَتِي وَأَخْلِفْ لِي خَيْرًا مِنْهَا " إِلا أَخْلَفَ اللَّهُ لَهُ خَيْرًا مِنْهَا)) روى مسلم


Imetoka kwa Ummu Salamah (Radhiya Allahu 'anhaa) ambaye amesema: Nimemsikia Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Muislamu yeyote atakayepatwa na msiba akasema yale aliyoamrisha na Allah "Inna Lillahi Wa Innaa Ilayhi Raaji'uun, [Sisi ni wa Allah nasi Kwake tutarejea] Ewe Allah Nipe ujira katika msiba wangu na nibadilishie ulio bora kuliko huo" basi Allah Atampa ulio na kheri kuliko huo [msiba])) [Muslim]

Katika waja wa Allaah (Subhaana wa Ta'aala) waliokuwa na subira ya ajabu ni Nabii Ayyuub ('Alayhis-salaam). Kisa chake ni kirefu tutakielezea tukijaaliwa katika visa vya Mitume InshaAllah.

Kisa Cha Swahaabiyyah Al-Khansaa Aliyekuwa na Subira kubwa:

Jina lake hasa ni Tamaadhur Bint 'Amru bin Ash-Shariyd bin Rabaah As-Sulaymiyyah. Alijulikana kwa jina la Al-Khansaa na vile vile Umm Ash-Shuhadaa (mama wa mashahidi) kutokana na watoto wake waliofariki katika jihaad. Pia alijulikana kuwa ni mwanamke mwenye haiba nzuri iliyojaa fadhila, tabia njema njema, ushujaa na subira kubwa.

Alipokuwa kabla ya kuingia katika Uislam, alikuwa akitunga mashairi ya beti mbili tatu hadi walipofariki kaka zake Mu'aawiyah na Swakhar bin 'Amru, alifikwa na huzuni kubwa sana hata akawatungia mashairi. Yakawa maarufu, naye akawa mshairi maarufu kabisa. Inavyosemekana hakuweko mwanamke aliyekuwa hodari wa mashairi kama yeye.

Baada ya vifo vya kaka zake, alikuja kwa Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) pamoja na watu wake wa Bani Sulaym akasilimu.

Ilipofika wakati wa vita vya Qaadisiyyah alidhihirisha subira yake kubwa alipokwenda vitani pamoja na watoto wake wanne wa kiume na akawausia kwa kuwaambia maneno haya mazito:

"Enyi watoto wangu, naapa kwa Yule Ambaye hakuna Apasaye kuabudiwa ila Yeye, nyinyi ni watoto wa baba mmoja, sikumkhini baba yenu, mmesilimu kwa kutii, mmehama kwa khiari yenu, …" hadi akasema "Mtakapoamka kesho Insha-Allah kwa salama, nendeni vitani kupigana na adui zenu, kwani mnajua Aliyowaandalia Allaah (Subhaana wa Ta'aala) ya thawabu nyingi kwa kupigana na makafiri. Tambueni kuwa nyumba ya milele (Pepo) ni bora kuliko nyumba ya kutoweka (Dunia), Anasema Allaah (Subhaana wa Ta'aala):

((يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اصْبِرُواْ وَصَابِرُواْ وَرَابِطُواْ وَاتَّقُواْ اللّهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ))

((Enyi mlioamini! Subirini, na shindaneni kusubiri, na kuweni macho, na mcheni Allah, ili mpate kufanikiwa)) [Al-'Imraan: 200].

Wakaenda vitani na alipopata habari ya vifo vyao wote alisema: "Alhamdulillah kwa Yule Aliyenipa heshima ya kuuliwa kwao na namuomba Allaah (Subhaana wa Ta'aala) Aniunganishe nao kwa Rahma Zake".

Al-Khansaa (Radhiya Allahu 'anhaa) alifariki katika Ukhalifa wa 'Uthmaan bin 'Affaan (Radhiya Allahu 'anhu).

 
 
 Posted By Posted juu ya Tuesday, December 04 @ 00:03:49 PST na MediaSwahiliTeam
 
 
:-: Go Home :-: Go Top :-:
 
 
 
Comments & Debates :-: التعليقات والمحاورات

 
 
For Your Membership Comments And Registered Debates Please, See Below Or Register Here :-: للحصول على تعليقات عضويتك و مناقشات الأعضاء انظر من فضلك أدناه أو سجّل هنا
 
 
:-: Go Home :-: Go Top :-:
 

Kuhusiana Viungo

· zaidi Mkuu - teknolojia na taaluma
· Habari na MediaSwahiliTeam


Kweli kusoma hadithi kuhusu Mkuu - teknolojia na taaluma:
MATUMIZI YA KUNUFAISHA YA HABBAT SAWDAA-1 -- (HABA SODA - CHEMBE NYEUSI )


Kifungu Rating

Wastani matokeo: 0
Kura: 0

Tafadhali chukua ya pili na kupiga kura kwa ajili ya makala hii:

bora Vizuri Sana Mema Kawaidar Mbaya

Chaguzi


 Chapa Rafiki Chapa Rafiki


Mada zinazohusiana

Mkuu - teknolojia na taaluma

 

 
EsinIslam The Muslim World Portal For Islamics, News, Fatwas, Audios, Videos, Muslim News, Quranic Islamic Articles, Radio, Audio Quran, TV Channels, Fatwa Rulings, Muslim News Newspapers Magazines Headlines Articles Forums Schools, Universities, Colleges, Mosques, Qur'an, Hadith, Sunnah, Fiqh, Prayers, Salat, Fasting Ramadan, Vidoes, Books On EsinIslam.Com And Muxlima.Com

  :-: Go Home :-: Go Top :-: