Swahili
- Ukurasa Kuu    - Kumi Juu    - Mada Mpya    - Salimisha Habari    - Tafuta    - Kiswahili Jukwaa    - Kiswahili Wanachama    - Tathmini    - Ujumbe wa Kibinafsi    - Tafiti    - Majarida    - Hadithi Archive    - Maudhui    - Viungo vya Wavuti    - Vipakuliwa    - Maswali ya Kawaida    - Tunapendekeze    - Orodha ya Kuingia   

 

 
Makatazo Ya Kishari’ah Kwa Wanawake – 6
 
 
Waislamu Wanawake - maisha yao na Famili Imekusanywa Na: Abu Faatwimah

Makatazo Ya Kishari’ah Kwa Wanawake – 6

Katazo la Kuingia katika Hammamaat [sehemu za kuogea zilizojengewa kama vile mahodhi mabwawa na kadhalika na kuruhusiwa kutumiwa na kila mtu].

Jamii nyingi huweka sehemu ambazo huwa zinaruhusiwa kutumiwa na kila mtu kwa malengo tofauti kama vile mabustani, maduni na kadhalika; pia hutenga sehemu nyingine ili zitumike kwa malengo maalumu; kama vile sehemu za kuogea au kuogolea, au sehemu za kuumika, au sehemu za kukandwa, au sehemu za kutengenezwa nyuso au nywele, au sehemu za kupambwa, au sehemu za kubadilisha mavazi au kujilinga, au sehemu za kupumzika, au sehemu za kufua nguo na kadhalika.

Imekusanywa Na: Abu Faatwimah

Katazo la Kuingia katika Hammamaat [sehemu za kuogea zilizojengewa kama vile mahodhi mabwawa na kadhalika na kuruhusiwa kutumiwa na kila mtu].

Jamii nyingi huweka sehemu ambazo huwa zinaruhusiwa kutumiwa na kila mtu kwa malengo tofauti kama vile mabustani, maduni na kadhalika; pia hutenga sehemu nyingine ili zitumike kwa malengo maalumu; kama vile sehemu za kuogea au kuogolea, au sehemu za kuumika, au sehemu za kukandwa, au sehemu za kutengenezwa nyuso au nywele, au sehemu za kupambwa, au sehemu za kubadilisha mavazi au kujilinga, au sehemu za kupumzika, au sehemu za kufua nguo na kadhalika.
Sehemu hizi katika baadhi ya jamii huwa ziko zilizotengwa maalumu kwa wanawake na kutenganishwa na za wanaume, na katika jamii nyingine huwa hakuna mtengano katika sehemu kama hizo; hivyo utaona baadhi ya jamii hata katika hospitali zao huwa wanawaweka wagonjwa wa kike na wa kiume katika chumba kimoja na chenye kuwatenganisha huwa ni pazia tu, na wako wenye kudai kutaka kuweko choo cha wote [wake kwa waume] bila ya mtengano.

Dada yangu katika iymaan, ijapokuwa katazo hili linabeba jina la katazo la kuingia katika hammammaat [mahodhi], lakini linakusudia kueleza kukatazwa kwa Muumini wa kike kuingia katika sehemu yoyote ile ambayo atalazimika kujifunua mwili wake au kudhihirisha sehemu yoyote ile ya mwili wake isiyotarajiwa kudhihirika na kupelekea kuonekana na kila aliyepo katika sehemu hiyo ambae si maharimu wake au hata wanawake wenzake ambao si Waumini; au katika sehemu ambayo atalazimika kuvua au kujivua mavazi yake; iwe hijaab au nguo yake yoyote ile, au katika sehemu ambayo atalazimika kudhihirisha nywele zake.

Sehemu zote zile anazokatazwa Muumini kuingia awe wa kike au kiume huenda zikawa za burudani -kama wanavyodai wengi- na nyingine, kama vile kwenye *****we [mwambao wa bahari], au sehemu za kuogelea (swimming pool), au saluni za kujiremba na kutengeneza nyuso au nywele; ni sehemu ambazo kwa kweli Muislamu wa kawaida huwa hatarajiwi kufikiria kwenda au kuweko kwa yale yanayofungamana na sehemu hizo, au kwa yale atayokutana nayo huko kwani hizo kwa ujumla ni sehemu zenye kila lenye kupingana na ile dini na shari’ah anayoshikamana nayo Muumini. Hivyo, Muumini hatarajiwi kuwepo achilia mbali kuruhusu ahli zake na Waumini wenzake kuwepo, kama ilivyothibiti katika Hadiyth ya Jaabir (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
“Yeyote anayemuamini Allaah na Siku ya Mwisho asiingie kwenye hammaam isipokuwa [awe amevaa] nguo ya kiunoni, na yeyote yule anayemuamini Allaah na Siku ya Mwisho asimuingize –asimuachie kuingia- khaliylah [mke] wake hammaam, na yeyote yule mwenye kumwamini Allaah na Siku ya Mwisho asikae katika meza inayonywewa ulevi, na yeyote yule mwenye kumuamini Allaah na Siku ya Mwisho asikae faragha na mwanamke asiyekuwa mahramu wake, kwani watatu wao ni shaytwaan.” [Imepokelewa na Ahmad, katika Musnad wake, katika Musnad ya Kumi waliobashiriwa Jannah, Saadis ‘ashar Al-Answaar, Hadiyth ya Jaabir bin ‘Abdillaah (Radhiya Allaahu ‘anhu), Hadiyth namba 14356].

Dada yangu katika iymaan, katika utumiaji wa mahodhi au mabwawa kama inavyoeleweka kuna uvuaji au ubadilishaji wa nguo au baadhi ya nguo na kudhihirisha mwili wote au sehemu ya mwili, ili mhusika aweze kuoga au kuogelea au japo kukaa ndani ya maji na kuburudika; ndio shari’ah ikamkataza Muumini kwenda kwenye hammamaat kama ilivyothibiti katika Hadiythi ya mama wa Waumini bibi ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anhaa) kwamba:
“Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikataza kuingia kwenye hammamaat, kisha akaruhusu Waumini wa kiume kuingia wakiwa wamevaa nguo za kiunoni” [Imepokelewa na Abuu Daawuud, katika Kitabu cha Hammaam, Hadiyth namba 3497].

Na katika Hadiyth ya ‘Abdullaah bin ‘Amr (Radhiya Allaahu ‘anhu) Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
“Hakika zitafunguliwa kwenu nchi za kigeni, na mtakuta humo nyumba kwa jina zinaitwa hammaamaat, basi wasiziingie wanaume isipokuwa kwa izaar –-wamevaa nguo ya kiunoni (vikoi): nguo yenye kufunika kutoka kitovu mpaka magoti- na akawazuia -kataza kuingia kwenye hammamaat- wanawake isipokuwa wanawake wagonjwa au wenye damu ya uzazi.” [Imepokelewa na Abuu Daawuud, katika Kitabu cha Hammaam, Hadiyth namba 3499].

Hivyo asili ni kuwa mtu haruhusiwi kuingia kwenye hammaamaat au kwenda kwenye *****we na sehemu zenye kudaiwa kuwa ni za burudani kwani mwenye kuingia huko hulazimika kudhihirisha mwili au sehemu ya mwili wake kwa watu na kwa mwanamke huwa watu wasiokuwa maharimu zake, au hulazimika kuangalia watu wasio kuwa na nguo, na hili jambo limekatazwa kama ilivyothibiti katika Hadiyth ya Abu Sa’iyd Al-Khudriy (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema kwamba Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
“Mwanamme asitazame utupu wa mwanamme; na wala mwanamke asitazame utupu wa mwanamke; na wala mwanamme asilale na mwanamme mwenziwe katika nguo moja; na wala mwanamke asilale na mwanamke mwenzie katika nguo moja.” [Imepokelewa na Muslim, katika Kitabu cha Hedhi, mlango wa uharamu wa kutazama sehemu za siri, Hadiyth namba 517].

Dada yangu katika iymaan, na hata kama itakuwa hiyo sehemu imetengwa kwa wanawake pekee, ieleweke kuwa huenda kukawepo wanawake wenzako ambao si Waumini kama wewe, na wasiokuwa Waumini huwa hawana cha kuwadhibiti, kwani asiyekuwa na iymaan au aliyekosa iymaan katika moyo wake na maisha yake hatarajiwi kuwa na kheri wala hayaa, na asiye na hayaa huwa hakuna cha kumdhibiti wala kudhibiti ulimi wake. Hivyo, dada yangu katika iymaan, katika hali kama hiyo kwenye hodhi au bwawa huwa umejifedhehesha na kujiondoshea mengi ya heshima na kubwa kuliko yote huwa umejiondoshea sitrah baina yako na Muumba wako, si tu kwa kuingia kwenye hodhi au bwawa, bali kwa kuvua nguo zako pahala ambapo si kwenye nyumba yako, jambo ambalo limekemewa na kukatazwa na shari’ah.
Imethibiti katika Hadiythi kuwa baadhi ya wanawake kutoka Ash-Shaam waliingia kwa mama wa Waumini bibi ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anhaa); bibi ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anhaa) akawauliza: Mnatokea wapi nyiny?' Wanawake wakajibu: Sisi ni watu wa Ash-Shaam'. Bibi ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anhaa) akasema: Huenda nyinyi mnatoka katika kitongoji ambacho wanawake wake wanaingia katika hammamaat?' Wakasema: Ndio. Bibi ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anhaa) akasema: Hakika mimi nilimsikia Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:
”Mwanamke yeyote yule atakayevua nguo zake katika pasipokuwa nyumbani kwake -nje ya nyumba ya mumewe-, atakuwa amekwishachana kilichopo baina yake na baina ya Allaah.” [Imepokelewa na Abuu Daawuud, katika Kitabu cha Hammaam, Hadiyth namba 3498; na At-Tirmidhiy, katika Kitabu cha Adab, mlango wa yaliyokuja katika kuingia Hammaam, Hadiyth namba 2747].

Dada yangu katika iymaan, na katika yenye kufanana na hammaam ambayo wanawake huwa wanapenda kutembelea na kwenda ni saluni za kujiremba na kutengenezwa nyuso, mwili na nywele. Sehemu hizi kama zilivyo ndugu yao hammaam huwa hazikosi kuwa na mambo mengi tu yenye kwenda kinyume au kupingana na shari’ah; kama vile unyoaji na unyofowaji wa nyusi, upigaji wa chapa, uunganishaji wa nywele, uvuaji na ubadilishaji wa nguo wenye kusababisha kutazama tupu, utoaji au unyofoaji na unyowaji wa nywele kwenye sehemu nyingine, ukataji au utengenezaji wa nywele wenye kufanana na mitindo ya kikafiri au mitindo ya wanawake wasiokuwa na heshima wala tabia nzuri, kutengenezwa au kupambwa na wanaume jambo ambalo ni msiba mkubwa na chanzo cha faahishah (uchafu).

Dada yangu katika iymaan, mtihani uliopo ni kuwa wanawake wengi wa zama hizi huwa wanafadhilisha na kupendelea kwenda kwenye sehemu hizi bila ya kuelewa kuwa ni sehemu zilizokatazwa kwa Muumin wa kike kwenda, huku wakielewa kuwa wasimamizi karibu wote au wengi wao ni watu wasiochunga heshima kwa Waumini hasa Waumini wa kike na wala hawako tayari kuwahifadhia siri zao, wachilia mbali kuwasitiri na kuwahifadhi tupu zao, na ukweli ni kuwa wengi wao ni katika mafasiki na wenye maradhi ya shahwaaniyyah na malengo yasiyo na heshima.

Na wako katika wanawake wasiokuwa na hayaa wala heshima na wala hawajiheshimu nafsi zao, wenye kuwataka wanaume –wasiokuwa waume zao- kuwasugua, kuwakanda, kuwapamba, kuwatengeneza nywele, kuwapima na kuwalinga nguo na kadhalika; yote hayo ni katika vitangulizi vya faahishah.

Dada yangu katika iymaan, ni wajibu wako kuzihama sehemu hizi, sehemu zenye kuambatana na kupendwa na kila asiyekuwa na sehemu muhimu katika sehemu za iymaan ambayo ni hayaa, zihame sehemu zenye uvunjwaji wa heshima, sehemu zenye kusababisha mtu kukashifu tupu zake, sehemu zenye kumbaidisha mtu na kila lenye kupendwa na Allaah na Mjumbe Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kumkurubisha na kwenye kila lenye kuchukizwa na shari’ah; zihame na zihajiri mhamo na hijrah ya kishari’ah aliyokushauri Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kama ilivyothibiti katika Hadiyth ya ‘Abdullaah bin ‘Amru (Radhiya Allaahu ‘anhu) kuwa Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
“Muislamu ni yule waliyesalimika Waislamu kutokana na ulimi wake na mkono wake; na Muhaajir ni yule aliyeyahama yale yaliyokatazwa na Allaah.” [Imepokelewa na Al-Bukhaariy, katika Tafsiyr ya Qur-aan, Suurat Qul A’uwdhu bi Rabil Falq, Hadiyth namba 6032; na Ahmad, katika Musnad wake, katika Musnad ya Kumi waliobashiriwa Jannah, Musnad Al-Mukthiyriyna katika Swahaba (Radhiya Allaahu ‘anhum), Hadiyth ya ‘Abdullaah bin ‘Amru (Radhiya Allaahu ‘anhu), Hadiyth namba 6779].

Dada yangu katika iymaan, ni jukumu lako la kishari’ah kuwahadharisha wanawake wenzako katika iymaan, unaowaelewa miongoni mwa wale wenye tabia ya kutembelea sehemu hizo au kufikiria kuzitembelea, kwani hilo ni katika kuamrisha mema na kukataza munkari unalotarajiwa kujipamba nalo katika uhai wako; Allaah Anasema:
“Na uweko (watokeze) kutoka kwenu Ummah unaolingania kheri na unaoamrisha ma’aruwf (mema) na unaokataza munkar. Na hao ndio waliofaulu.” [Aal-‘Imraan 3:104].
 
 
 Posted By Posted juu ya Tuesday, December 04 @ 00:01:02 PST na MediaSwahiliTeam
 
 
:-: Go Home :-: Go Top :-:
 
 
 
Comments & Debates :-: التعليقات والمحاورات

 
 
For Your Membership Comments And Registered Debates Please, See Below Or Register Here :-: للحصول على تعليقات عضويتك و مناقشات الأعضاء انظر من فضلك أدناه أو سجّل هنا
 
 
:-: Go Home :-: Go Top :-:
 

Kuhusiana Viungo

· zaidi Waislamu Wanawake - maisha yao na Famili
· Habari na MediaSwahiliTeam


Kweli kusoma hadithi kuhusu Waislamu Wanawake - maisha yao na Famili:
Elimu Ni Wajibu Kwa Mwanamke Wa Kiislamu - MIFANO YA WANAWAKE WATUKUFU


Kifungu Rating

Wastani matokeo: 0
Kura: 0

Tafadhali chukua ya pili na kupiga kura kwa ajili ya makala hii:

bora Vizuri Sana Mema Kawaidar Mbaya

Chaguzi


 Chapa Rafiki Chapa Rafiki


Mada zinazohusiana

Waislamu Wanawake - maisha yao na Famili

 

 
EsinIslam The Muslim World Portal For Islamics, News, Fatwas, Audios, Videos, Muslim News, Quranic Islamic Articles, Radio, Audio Quran, TV Channels, Fatwa Rulings, Muslim News Newspapers Magazines Headlines Articles Forums Schools, Universities, Colleges, Mosques, Qur'an, Hadith, Sunnah, Fiqh, Prayers, Salat, Fasting Ramadan, Vidoes, Books On EsinIslam.Com And Muxlima.Com

  :-: Go Home :-: Go Top :-: