Swahili
- Ukurasa Kuu    - Kumi Juu    - Mada Mpya    - Salimisha Habari    - Tafuta    - Kiswahili Jukwaa    - Kiswahili Wanachama    - Tathmini    - Ujumbe wa Kibinafsi    - Tafiti    - Majarida    - Hadithi Archive    - Maudhui    - Viungo vya Wavuti    - Vipakuliwa    - Maswali ya Kawaida    - Tunapendekeze    - Orodha ya Kuingia   

 

 
SUNNAH NZURI KATIKA UISLAM: Jibu la Sheikh 'Abdul 'Aziz bin Baaz
 
 
bakom domstolens rättspraxis ya Kii
SUNNAH NZURI KATIKA UISLAM: Jibu la Sheikh 'Abdul 'Aziz bin Baaz

Imetarjumiwa na Ummu Iyyaad

SWALI: 
 ((Atakayefanya Sunnah njema atapata ujira wake na ujira wa  

              yule atakayefanya kile kitendo mpaka siku ya Kiyama))

Je, kwanza hii ni Hadithi (Sahihi?) 

Pili, kama ni hadithi (Sahihi) je, Mtume صلى الله عليه وسلم aliacha jambo (la Sunnah) kwetu ambalo hakulifanya yeye ili mtu alifanye katika Uislam?? Tunaomba utufahamishe kwa kutufafanulia wazi jambo hili.SUNNAH NZURI KATIKA UISLAM: Jibu la Sheikh 'Abdul 'Aziz bin Baaz

Imetarjumiwa na Ummu Iyyaad

SWALI: 
 ((Atakayefanya Sunnah njema atapata ujira wake na ujira wa  

              yule atakayefanya kile kitendo mpaka siku ya Kiyama))

Je, kwanza hii ni Hadithi (Sahihi?) 

Pili, kama ni hadithi (Sahihi) je, Mtume صلى الله عليه وسلم aliacha jambo (la Sunnah) kwetu ambalo hakulifanya yeye ili mtu alifanye katika Uislam?? Tunaomba utufahamishe kwa kutufafanulia wazi jambo hili.

Anajibu Sheikh 'Abdul 'Aziz bin Baaz

Jibu: Hadithi hii ni Sahihi nayo inatuonyesha sheria (au kuruhusu) kuhuisha Sunnah na kuiitikia (kuifundisha) na kuhadharisha Bid'ah na shari. Kwa sababu Mtume صلى الله عليه وسلم amesema

((من سن في الإسلام سنة حسنة كان له أجرها وأجر من عمل بها من بعده لا ينقص ذلك من أجورهم شيئاً ومن سن في الإسلام سنة سيئة كان عليه وزرها ووزر من عمل بها من بعده لا ينقص من أوزارهم شيئاً)) خرجه مسلم في صحيحه

((Atakayefanya kitendo chema  katika Uislam atapata ujira wake na ujira wa yule atakayekitenda baada yake  bila ya kupungukiwa  thawabu zao. Na atakayetenda kitendo kibaya katika Uislam atabeba (mzigo wa) dhambi zake na dhambi za yule atakayetenda wala hapungukiwi kitu katika (mzigo wa) dhambi hizo)) (Muslim)

Mfano wa hadithi hii iliyotoka kwa Abu Hurayrah رضي الله عنه kwamba Mtume

صلى الله عليه وسلم kasema:

(( من دعا إلى هدى كان له من الأجر من أجور من تبعه لا ينقص من أجورهم شيئاً ومن دعا إلى ضلالة كان عليه من الإثم مثل آثام من تبعه لا ينقص ذلك من آثامهم شيئاً)) مسلم

((Atakayefanya daawa kuonyesha uongofu atapata thawabu (ujira) wa yule atakayemfuata bila ya kupungukiwa chochote katika thawabu zao na atakayeongoza katika upotofu atapata dhambi mfano wa dhambi zayule atakayefuata bila ya kupungukiwa chochote katika dhambi zao)) Muslim

Maana ya (Atakayefanya Sunnah katika Uislam) ni kuihuisha (kuifufua) Sunnah, kuidhihirisha na kuifichua Sunnah ambayo imefichika kwa watu (au imeghafiliwa na watu) basi huidhihirisha na kuibainisha, basi hupata thawabu kama za atakayetenda kitendo hicho na si maana kwamba ni kuzusha (kuanzisha) kitendo kipya. Kwa sababu Mtume صلى الله عليه وسلم kakataza kuzusha bid'ah akasema: “Kila uzushi ni upotofu” Na maneno ya Mtume

صلى الله عليه وسلم kutokana na Ahlul-Ilm yanawafikiana yote pamoja wala hayapingani au kugongana.

Kwa hiyo, ilivyokusudiwa katika hadiyth ni kuihuiisha Sunnah na kuidhihirisha. Kama mfano wa kuwepo mwenye elimu katika nchi ambayo hakuna mafunzo ya Qur’aan au hakuna mafunzo ya Sunnah za Mtume

 صلى الله عليه وسلم, yeye akayarudisha mafunzo hayo kwa kuwakalisha watu na kuwafundisha Qur’aan na Sunnah au kuwaekea walimu kuwandisha watu elimu hizo. Au mfano mwingine akakuta katika nchi watu wanayoa  ndevu zao au wanazikata akaamrisha wafuge na wasinyoe, hivyo atakuwa ameihuiisha  Sunnah hii tukufu katika nchi hiyo ambayo watu walikuwa hawaijui au imeachwa na hadi kusahaulika au kutojulikana, na akapata thawabu sawa na thawabu za watakaopata hidaaya  kutoka kwa Allaah سبحانه وتعالى kwa sababu yake.

Mtume صلى الله عليه وسلم kasema

(( قصوا الشوارب وأعفوا اللحى وخالفوا المشركين)) متفق على

 ((Kateni masharubu na wacheni ndevu, muwe tofauti na washirikina))

(Hadiyth hii imesimuliwa na Al-Bukhari na Muslim kutoka kwa Ibn 'Umar رضي الله عنهما) 

Na watu walipomuona huyo mwalimu yeye mwenyewe kaziweka ndevu zake wakamfuata, kwa hiyo anakuwa kawahuiishia wao hiyo Sunnah. Nayo ni Sunnah ya waajib haifai kuiacha kwa kufuata maamrisho ya hadiyth iliyotajwa hapo juu na maana yake, akawa kwa kufanya hivyo, kapata thawabu sawa na thawabu zao.  

Au mfano katika nchi watu hawaswali Swalah ya Ijumaa kutokana na kutokujua kwao (umuhimu wake) akawafundisha na kuwaswalisha akapata mfano wa thawabu zao pia. Na hivyo hivyo watu katika nchi nyingine hawatambui Swalah ya Witr akawafundisha wakamfuata au mifano kama hiyo katika vitendo vya ibada na sheria vinazojulikana katika Uislam, akazidhihirisha baada ya kufichika au kutokutambulika katika baadhi ya nchi au jamii ya watu.

Hivyo, atakayezifufua baina yao akazieneza na kuzibainisha ndiye yule aliyekusudiwa katika Hadithi kuwa 'kafanya Sunnah katika Uislam Sunnah njema’ kwa maana kwamba  ameidhihirisha (fundisho, hukumu ya sheria ya Kiislamu. Ndio akawa miongoni mwa wale ((atakayefanya kitendo cha Sunnah njema katika Uislamu ))

Na sio maana kwamba aanzishe (azushe) jambo katika dini lisiloamrishwa  na Allaah.  Kwani uzushi ni upotofu kutokana na kauli ya Mtume صلى الله عليه وسلم katika hadithi sahihi,

(( وأياكم ومحدثات الأمور فإن كل محدثة بدعة وكل بدعة ضلالة))

((Jihadharini na mambo ya uzushi kwani kila uzushi ni Bid'ah na kila Bid'ah ni upotofu))

Vile vile anasema Mtumeصلى الله عليه وسلم katika hadithi Sahihi:

(( من عمل عملاً ليس عليه أمرنا فهو رد)) البخاري

((Atakayetenda kitendo kisichokuwa chetu basi kitarudishwa.)) Al Bukhari.

Na katika kauli nyingine,

( من أحدث في أمرنا هذا ما ليس منه فهو رد) متفق عليه.

((Atakayezusha katika mambo yasiyokuwa yetu  basi kitarudishwa))

Al-Bukhaariy na  Muslim. 

Na Mtume صلى الله عليه وسلم alikuwa akisema katika Khutba ya Ijumaa,

((أما بعد فإن خير الحديث كتاب الله وخير الهدى هدى محمد صلى الله عليـه وسلم وشر الأمور محدثاتها وكل بدعة ضلالة)) خرجه مسلم في صحيحه

((Amma Ba'ad hakika lililokuwa bora kabisa la kuhadithia ni Kitabu cha Allaah, na uongofu ulio bora ni uongofu wa Muhammad صلى الله عليه  وسلم  na jambo la shari kabisa ni uzushi wake na kila uzushi ni upotofu))

Muslim katika Sahihi yake. 

Kwa hiyo aina ya ibada yoyote isiyoletwa na Allah, haifai (kuifundisha) kuifanyia daawa, wala anayeileta na kuifanya hapati thawabu bali itakuwa  kuitenda na kuileta kwa watu ni Bid'ah na huyo atakayeileta (kwa kuitangaza na kuieneza kwa watu) atakuwa ni katika yule anayeongoza katika upotofu na Allaah سبحانه وتعالى Amemlaumu na kumhoji huyo mtu mwenye kutenda hivyo kuwa je, 

{{Au hao wana miungu ya kishirikina waliowatungia dini asiyoitolea idhini Mwenyezi Mungu…}} Ash Shuura:21

 
Wa Allaahu A’alam

 
 
 Posted By Posted juu ya Tuesday, May 11 @ 22:42:33 PDT na MediaSwahiliTeam
 
 
:-: Go Home :-: Go Top :-:
 
 
 
Comments & Debates :-: التعليقات والمحاورات

 
 
For Your Membership Comments And Registered Debates Please, See Below Or Register Here :-: للحصول على تعليقات عضويتك و مناقشات الأعضاء انظر من فضلك أدناه أو سجّل هنا
 
 
:-: Go Home :-: Go Top :-:
 

Kuhusiana Viungo

· zaidi bakom domstolens rättspraxis ya Kii
· Habari na MediaSwahiliTeam


Kweli kusoma hadithi kuhusu bakom domstolens rättspraxis ya Kii:
Haki Za Mume Na Mke: Nasaha Za Shaykh Kwa Wanandoa


Kifungu Rating

Wastani matokeo: 0
Kura: 0

Tafadhali chukua ya pili na kupiga kura kwa ajili ya makala hii:

bora Vizuri Sana Mema Kawaidar Mbaya

Chaguzi


 Chapa Rafiki Chapa Rafiki


Mada zinazohusiana

bakom domstolens rättspraxis ya Kii

Sisi msamaha, Maoni hazipatikani kwa makala hii.
 

 
EsinIslam The Muslim World Portal For Islamics, News, Fatwas, Audios, Videos, Muslim News, Quranic Islamic Articles, Radio, Audio Quran, TV Channels, Fatwa Rulings, Muslim News Newspapers Magazines Headlines Articles Forums Schools, Universities, Colleges, Mosques, Qur'an, Hadith, Sunnah, Fiqh, Prayers, Salat, Fasting Ramadan, Vidoes, Books On EsinIslam.Com And Muxlima.Com

  :-: Go Home :-: Go Top :-: